Tuchukulie Juma ana mke lakini juma ni mhuni anachukuwa wake wengine na akatokezea Paulo huyu paulo kamwambia mke wa juma jinsi juma anavyofanya,paulo kaenda mbali mpaka kafanikisha mke wa juma kumshika juma ugoni.
Na baada ya tendo hilo paulo anaanza kumshawishi mke wa juma ,kwamba ili ngoma iwe droo ama malipizi naye atembee na paulo,paulo anajinadi yeye ni mtu mzuri kwa sababu amefanikisha kumsika ugoni bwana wake, hivyo yeye paulo ana mapenzi mema na anamtakia mambo mazuri sana mke wa juma hivyo anaomba mke wa juma ampe uroda.
JF huwa mafumbo hayasaidii, weka wazi kati ya mbowe na zitto nani kapata umaarufu kupitia kwa mwingine?? Siyo unazunguka mbali sina muda wa kuanza kujiuliza hasa unafumba nini.