Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Tuliwaambia sisi tusio wapenzi na wafurukutwa wa vyama tatizo la chadema ni Mbowe, Walimfanyia fitina marehemu Chacha wakamuita anatumiwa na ccm.Sitoshangaa tena leo Zitto naye kupewa kilemba hicho.

Mchawi huwa halogi mara moja akastaafu,ama wahenga wanasema ukishaonja nyama ya mtu huishii kuonja mara moja.

Lakini waswahili wanasema siku ya mbwa kufa pua huziba.

Ni maoni yangu
 
hisia zako tu, na kinachokusumbua ni INFERIORITY COMPLEX kwa wachagga, siyo peke yako ni watu wengi sana
kipofu haambiwi tazama,haihitaji uwe umekwenda univesiti kugundua kuwa CHADEMA ni sacos ya baadhi ya wachaga
 
Ndugu Sikonge Tamko lako hili tuu "Naona na sisi Wanyamwezi tuwe na chama chetu........." Linanipa mashaka juu ya ufahamua wako wa mambo na hasa Siasa

Mimi naamini kigezo cha nanikuchanguli au kutochanguliwa kisiwe baba na mtoto au mtu na rafiki Kiwe utendaji kama utandaji wa mtu(watu) ni mzuri then wachaguli na ndo walivyofanya wajumbe

Kwahiyo CHADEMA utendaji uko kwa Wachaga tu? Mkuu hili la CHADEMA na Uchaga limejadiliwa mno ila tu they don't get it!

Ndugu yangu Sikonge wewe jiunge na CUF tu chama cha Mapalala na Prof. Lipumba.

Mimi nasubiri prof. Mwandosya aanzishe chama chake na sisi tubebe bango letu. Kama kuna wabunge wanawake wa kuteuliwa tunachagua Wanyakyusa wa Tabora walioenda kulima Tumbaku, wanyakyusa wa Tanga walioenda kulima Mkonge. Vinginevyo tunawapa hizo nafasi mashemeji zetu. Kama yule mke wa Mwakalinga tunampa ubunge wa kuteuliwa kisha tunasema huyo mtu wa Tanga. Mke wa Dr. Mwakyembe tunampa ubunge pia na kusema huyo mtu wa Kilimanjaro. Mke wa Prof. Mwandosya naye anapeta ila tutasema yeye ni Mganda au Mhaya Diaspora.
 
Una mapenzi na Wachaga mpaka umekuwa kipofu.

Hii ya CHADEMA kuwa SACCOS ya Wachaga fulani hivi imetulia.

Na Wewe ni Mmojawapo? hii inathibitisha kauli yangu kwamba si First Lady peke
 
Michango yetu ingekuwa mizuri kama tungejua issues zilizowashawishi wapiga kura. Hili la ukabila naona ni agenda inayoingia mara kwa mara badala ya issues. Wanaozungumzia ukabila wanaona kila kitu kwa jicho la ukabila. Hilo naomba tuliangalie lisituondoa kwenye kuona mafanikio na sababu za watu kugombea. Hata la Zitto sina uhakika kama tumepata undani wa yote yaliyojili. Kama mtu ana undani atuarifuu/atuelimishe
 
Wakuu kama bado hauna chama sahihi hadi sasa hv kama mm basi tujiunge tuanzishe chetu ambacho hakitakuwa na unyamwezi,uhehe au uchaga!
 
Una mapenzi na Wachaga mpaka umekuwa kipofu.

Hii ya CHADEMA kuwa SACCOS ya Wachaga fulani hivi imetulia. Akina Zitto ni vibarua tu hata siku moja hawawezi kumilikishwa hii SACCOS.

Na Wewe ni Mmojawapo? hii inathibitisha kauli yangu kwamba si First Lady peke yake
 
Wewe wasema

Huwezi kuwa first lady halafu una mawazo finyu hivyo jamani tunaomba tuwe makini jamani na kauli zako. kama ni kweli ni chama cha wachaga toa hoja yako lakini mambo ya kufanya utani kwa sababu tu internet huko ni bei nafuu lazima ujue utani wako kuna watu wanaumia na wataendelea kuumia .Wakati wewe unapoongea pumba zako zisizo na kichwa wala miguu lazima ujue kuwa kuna mama mmoja amejifungulia nyumbani na anabreed mpaka anakufa bila ya msaada (wewe unaleta utani), mtoto aliye chini ya miaka mitano anakufa kwa maleria amabyo ingetibika kwa Tzs 3000.

Halafu baadaye unapata laana unaanza kujiuliza imetoka wapi!
 
First lady na ndege acheni malumbano, CHADEMA wamelikoroga na lazima walinywe. Tusubiri tu mwakani tumpe kura zetu JK mambo mswano, japo kuwa CCM ni kama kikundi cha wauza unga.

Kabla CCM haija pasuka hapata kuwepo na wapinzani wa kweli, labda Mrema tu.
 
Wazee wa Chadema wasiozidi watano walipohojiwa na vyombo vya habari mbali mbali walisema kuwa Zitto ana haki ya kugombea pia anatimiza demokrasia kama Chadema inavyosimama.

wazee hawa jana wamemzuia Zitto kugombea uenyekiti.kamati kuu na mkutano mkuu wa Chadema una maana gani wakati wazee wa Chadema wameshafanya maamuzi yao? bnaona kazi za kamati kuu na mkutano mkuu wameshazifanya hawa wazee wa Chadema,okoeni pesa hakuna haja ya kuwa na mkutano mkuu.


Ukisikia Chama kina wenyewe, basi uelewe maana yake. Hao unaowasema ndiyo wenye chama. Hayo mambo ya Kamati Kuu na Mkutano Mkuu ni kupoteza maboya tu!
 
Matatizo ya CHADEMA yapo kwenye vyanzo vya fedha. Hapo ndipo tatizo lilipo. Nani atachaguliwa kuwa mwenyekiti kwenye uchaguzi huu, ndiye atakaye peleka chama kwenye uchaguzi 2010.

CHADEMA inategemea kushinda majimbo zaidi ya haya ya sasa, hivyo mapato yao yataongezeka maradufu…usimamizi wa mapato hayo ndio chanzo cha haya yote.

Natumaini watamaliza hizi tofauti zao kwenye uchaguzi huu. Taifa linawahitaji watu kama Dr Slaa wame behind strong institutions.

Come on CHADEMA….
 
Cahama mbadala teh teh teh teh teh

Kitila
Kuna siku ulimshangaa Mwakalinga kugombea kupitia ccm keo wasema je?.

Pengo,katumwa kutuambieni si wote wanaosema ufisadi wna nia njema ni kwasababu wamekosa nafasi za kufisadi.

Na mimi nasema kuhangaika kukitoa chama kwa chama mbadala ni aproach feki .

Mbowe nilisha sema siku nyingi anakitumia chama kufanya biashara ,pale anapokikopesha chama masikini fedha za kuzunguka na helkopita na kwenye helkopita anazunguka yeye na harafu chama kinakuja kumlipa fedha hiyo na cha juu.

Pia nilisema ukiona mtu anapata umaarufu kwa kupitia mtu mwoovu huyo mtu mwangalieni mara mbili mbali mara nyingi watu wa namna hii si wema.
 
Nafikiri tumetoa mawazo yetu ya kutosha kuhusu hili. Na nafikiri watu wameishiwana hoja mpya sasa wanaanza kutukanana, siyo busara bora msichangie. Mambo muhimu yaliyojitokeza ktk mjadala huu, wapo waliosema zitto angeruhusiwa tu agombee kwani ndo demokrasia, wapo wanaosema hakutakiwa kugombea kuwa alitakiwa avute subira kidogo kwani hana uzoefu, wapo waliotoa mawazo ya jumla kwa pande zote mbili, lakini wakionyesha wasi wasi wa uadilifu wa zitto hasa kuhusiana na issue ya DOWANS, na wakaonya kuwa huenda anatumiwa na CCM.

Hoja zilikuwa nzuri na nadhani CHADEMA wamepata cha kuweza kufanyia kazi. Masuala ya uchaga na nini, haya ni mambo ya kupuuzwa kwa sababu huwezi kumpata mtu/kiongozi yoyote asiye na kabila, hata mzanaki kama nyerere bado uzanaki ni kabila, kwa hiyo malumbano ya ukabila hayana nafasi hapa.
 
owenya%281%29.jpg

Lucy Owenya.

Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo na mtoto wake, Lucy Owenya, wamechaguliwa bila kupingwa kukiongoza chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Kilimanjaro kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ndesamburo alichaguliwa tena kukiongoza chama hicho mkoani hapa baada ya kuibuka na ushindi wa kura
49 kati ya 50 za wajumbe wa mkutano huo wakati mtoto wake, Lucy, aliibuka na ushindi wa idadi ya kura kama hizo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana mjini hapa.

Katika uchaguzi huo,
Basil Lema, alichaguliwa kuwa Katibu wa chama hicho huku Deogratius Munishi, akichaguliwa kuongoza Baraza la Vijana wa chama hicho na Seranus Mushi alichaguliwa kuongoza Baraza la Wazee wa chama hicho.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Ndesamburo alisema ushindi wake ni ishara kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwamba bado anakubalika na kamwe hata katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu hapo mwakani, atajitahidi kutetea kwa udi na uvumba kiti chake cha ubunge.

Alisema anashangazwa na propaganda za viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakidai kuwa yeye ni mzee na hivyo hatagombea tena kiti cha ubunge Jimbo la Moshi Mjini jambo ambalo si la kweli.

"Eti wanasema mimi ni mzee, kibabu nimechoka sitagombea tena ubunge...Huo ni uzushi wao na ushindi wangu wa leo ni indiketa ya kwamba uchaguzi mkuu ujao nitatetea jimbo langu na kumbwaga mgombea wa CCM,” alisisitiza Ndesamburo.

Naye Lucy Owenya ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) akizungumza na waandishi wa habari baada ya ushindi huo, alitoa wito kwa wanawake mkoani Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Owenya alisema wanawake hawana budi kuacha woga wa kuwania nafasi za uongozi kuanzia serikali za mitaa, madiwani na hata ubunge ili kuweza kufikisha uwakilishi wa asilimia asilimia 50 bungeni na halmashauri.





CHANZO:

Ndesamburo na Mtoto wake hawakuwa na wapinzani kama itakavyokuwa kwa Mbowe hatakuwa na Mpinzani.

kingine wagombea wote ni wachagga kwani Kilimanjaro si kuna wapare pia?

Mkuu ungekuwa Fair kama ungekuja na Matokeo ya Viongozi wa Mikoa yote against Makabila yao, No Wonder ungekuta kwa Mbeya Mwenyekiti na katibu wote ni Wanyakyusa, so do mikoa mingine
 
Sija kuelewa hapa

Tuchukulie Juma ana mke lakini juma ni mhuni anachukuwa wake wengine na akatokezea Paulo huyu paulo kamwambia mke wa juma jinsi juma anavyofanya,paulo kaenda mbali mpaka kafanikisha mke wa juma kumshika juma ugoni.

Na baada ya tendo hilo paulo anaanza kumshawishi mke wa juma ,kwamba ili ngoma iwe droo ama malipizi naye atembee na paulo,paulo anajinadi yeye ni mtu mzuri kwa sababu amefanikisha kumsika ugoni bwana wake, hivyo yeye paulo ana mapenzi mema na anamtakia mambo mazuri sana mke wa juma hivyo anaomba mke wa juma ampe uroda.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom