Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Chama chenu ci kafu au?kile chama cha mapalala

CUF na Wanyamwezi wapi na wapi?

Yule Lipumba kawekwa pale PICHA tu. Kwa Tabora anakotoka Picha Lipumba ni kwamba hakuna hata mbunge mmoja kutoka CUF. Hata mwenyewe hana ubunge. CUF ni Pemba na Maalim Seif Hamad , hiyo inajulikana kwa wote ila naona siyo wote.....
 
Mkuu Invisible, inawezekana kuwa uko sahihi. Lakini kuna mambo ya mbali sana tunayotakiwa kuangalia kuhusu uamuzi wa wazee kumshinikiza au kumuomba Zitto aondoe jina lake. Naamini kuwa wanafahamu nini maana ya Demokrasia, nini maana ya uchanguzi na wanafahamu uwezo, upungufu na manufaa yanayotokana na mmoja kati ya wanachama hao wawili kuwa mwenyekiti wa Chama.
Zitto mwenyewe amesema anakiri kuwa Mbowe ametoa mchango mkubwa kwa Chadema, na sisi wenyewe tumeona mchango za Zitto kwenye jimbo lake na kwa taifa. No doubt kuwa wowte wanauwezo.

Lakini, ukiangalia jinsi jamii yetu ilivyo na siasa zetu zinavyokwenda, naona kwa sasa Zitto can serve us better asipokuwa mwenyekiti wa chama. Ana uwezo mkubwa wa kuwa mwenyekiti lakini tukiangalia alama za nyakati na hali ya siasa za sasa inaonekana kama yeye anatakiwa front line, na sio kwenye desk, he is more of a fighter, and can serve the nation better as a fighter than kuwa mwenyekiti wa chama. By the way CHADEMA inatakiwa ioneshe muendelezo wa kipindi kilichopita, kujenga chama na kujitahidi kuwafikia zaidi wananchi na kutetea zaidi maslahi ya wananchi. Sina hakika kama hilo linaweza kufanikishwa vizuri na Zitto akiwa mwenyekiti.

By the way, kama kuna wazee CHADEMA that is a very good sign, kama kuna wazee ambao Zitto ameweza kuwasikiliza ni jambo zuri sana. Na ikumbukwe kuwa Zitto alisema ameombwa na wanachama agombee uenyekiti, sioni kama kuna ubaya aksema ameondoa jina lake kutokana na ombo la hao hao wanachama.

Problem ni pale huyo fighter anapokuwa hathaminiwi, na kwa namna moja au nyingine hana watu wa kuwasimamia.

Kama kuna migongano kati ya Mbowe na Zitto, basi hakuna cha fighter wala mwenyekiti! Zitto hana pa kukimbilia akikosea au akiharibu kibinadamu na hapa ndio tatizo nadhani

Mbowe Yes ana damu ya Nyerere anaweza uongozi, lakini asipokuwa ktika mapatano na akina zito ataanguka
 
Ndugu zanguni naona sasa tumeongea hata tunafika mahali nadhani inakuwa shida .Tatizo la Chadema sasa katika uongozi si la kwanza katika medani za Siasa Tanzania nahata Afrika .Lugha za kusema chama kina wenyewe nao ni wachaga ni kupotosha .Wazee walio kaa na Zitto na Mbowe ni hawa

Bob Makani
Mtei E
Ngaiza
Slaa
Pro.Baregu
na nadhani kuna 2 nimewasahau.

Hebu tuanze kuangalia wachaga ni wangapi hapa na familia moja ni ipi hapo .

Kuna jambo moja kwamba watu wanusuru Chama sasa tuombee mema maana hata Mbowe na Zitto wanajua nini tunataka , Mtei bahati njema anakuja humu anajua na si kwamba hawapati mijadala. Jana hawaja lala wote wanafuatilia tunasema nini ni wazi wamesha ujua msimamo wetu .Sote kabisa tuna nia njema kwamab Chadema iende mbele nadhani tuweke nguvu katika hilo na siamini kwamba mtu akusema turudi CCM ndiyo jibu sahihi .Lazima mambo mengine tuyasimamie kwa nguvu zetu bila kila kitu kurudi nyuma na kurusha lawama .
 
Kwani lidhiwani kikwete na kiwete inakuwaje au umemuona Lucy peke yake. Makamba na mwanae pale ikulu vipi?


Lidhwani, JK na Salma wote wako ndani ya CCM na wote viongozi .

Mleta habari umesema Ndesa alipata kura 49 na hakuwa na mpinzani , sasa kama hakutokea mtu kupingana naye je ? Ukiona mzee anapita means anakubalika ambao ndiyo ukweli .Kwamba wapare hawakusimama sasa hii ni shida kubwa ya ukabila naona unakubana sana kaka .Sisi twende tukalazimishe makabila kuingia Siasa nakuoma kugombea ?
 
Lunyungu said:
Ndugu zanguni naona sasa tumeongea hata tunafika mahali nadhani inakuwa shida .Tatizo la Chadema sasa katika uongozi si la kwanza katika medani za Siasa Tanzania nahata Afrika .Lugha za kusema chama kina wenyewe nao ni wachaga ni kupotosha .Wazee walio kaa na Zitto na Mbowe ni hawa

Bob Makani
Mtei E
Ngaiza
Slaa
Pro.Baregu
na nadhani kuna 2 nimewasahau.

Hebu tuanze kuangalia wachaga ni wangapi hapa na familia moja ni ipi hapo .

Kuna jambo moja kwamba watu wanusuru Chama sasa tuombee mema maana hata Mbowe na Zitto wanajua nini tunataka , Mtei bahati njema anakuja humu anajua na si kwamba hawapati mijadala. Jana hawaja lala wote wanafuatilia tunasema nini ni wazi wamesha ujua msimamo wetu .Sote kabisa tuna nia njema kwamab Chadema iende mbele nadhani tuweke nguvu katika hilo na siamini kwamba mtu akusema turudi CCM ndiyo jibu sahihi .Lazima mambo mengine tuyasimamie kwa nguvu zetu bila kila kitu kurudi nyuma na kurusha lawama .

Lunyungu,

..ukikwepa shutuma za UCHAGA unaangukia kwenye shutuma za UDINI.

..wangemuachia tu Zitto na shutuma kwamba Chadema ni mali ya Wachaga na Wakristo zingekwisha.

NB:

..lakini pia namshangaa sana Zitto kuingia kwenye kinyanganyiro cha Uenyekiti kwa madai ya kutaka kukinusuru chama.

..halafu anageuka na kujitoa, akidai anataka kukinusuru chama.

..kwanza Zitto alidai anataka kupumzika ubunge na kwenda kusoma mpaka afikie PhD. siyo zaidi ya miezi mitatu iliyopita when that happened. sasa amebadilika anataka kutetea kiti chake cha ubunge, then amejaribu kugombea uenyekiti wa chama, na sasa amejitoa.

..kwa wanaomshauri wamwambie atulie anawachanganya wananchi.
 
Lunyungu,

..ukikwepa shutuma za UCHAGA unaangukia kwenye shutuma za UDINI.

..wangemuachia tu Zitto na shutuma kwamba Chadema ni mali ya Wachaga na Wakristo zingekwisha.

NB:

..lakini pia namshangaa sana Zitto kuingia kwenye kinyanganyiro cha Uenyekiti kwa madai ya kutaka kukinusuru chama.

..halafu anageuka na kujitoa, akidai anataka kukinusuru chama.

..kwanza Zitto alidai anataka kupumzika ubunge na kwenda kusoma mpaka afikie PhD. siyo zaidi ya miezi mitatu iliyopita when that happened. sasa amebadilika anataka kutetea kiti chake cha ubunge, then amejaribu kugombea uenyekiti wa chama, na sasa amejitoa.

..kwa wanaomshauri wamwambie atulie anawachanganya wananchi.


Unajua mie nachoka sana kila mara watanzania mnapo kuja hoja nyepesi .Huko CCM kuna ujinga kibao ikiwa ni pamoja udini kumea hadi nje lakini no talking about it .CCM ina miaka mingapi ukilinganisha na Chadema ? Jamani we all know kwamba wakati vyama vina anzishwa watu wengi kama ilivyo walikuwa ni watu w akudharau kwaba wapinzani ni wapuuzi hawawezi kufika popote .Leo wamefika mahala pamoja na shida zao na uchanga nk bad utasikia Michaga mara wadini .Hivi kama watu hawaendi kwenye Chama na kugombea nafasi mnataka kesho kitokee nini ?
Nadhani this is to low hakika .Uongozi wa Chadema juu kuna Mbowe hadi sasa haya tuje chini huku tuona kuna wachaga wangapi akina Zitto ni wakristo ama wachaga akina Slaa ? Hebu tuangalie shida iliyoko mezani muda huu na si zaidi ya kuleta habari za akina Tambwe .CCM ina ukabila udini na hata ukanda kama wabisha angalia viongozi wote wakubwa wa CCM wakwepo akina Tambwe wanatokea wapi linganisha na Chadema.

Chadema they made a mistake kwenye viti maalumu nadhani hawatakaa warudie lakini pia lazima watu wajitolee kushiriki siasa wapate hizo nafasi na si kulalama tu.
 
Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.

Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...

Article ya Kibanda ilitosha kuwa shinikizo kwa Zitto...Kibanda si Mtu mdogo...

I'm speechless kwa haya yanayotokea Chadema...Bado tuna safari ndefu mno kufikia Demokrasia ya kweli....Kwa mwendo huu bado tutakuwa na taabu sana ya kuing'oa CCM!!

Zitto na vijana wengine wa Chadema... Karibuni CCM

Wakati CHADEMA mnapandishiana, ndipo CCM inapata nafasi ya kutia propasganda, na hata kuyeyushilia mbali skendo za ufisadi ambazo zimekuwa zinaibuliwa na CHADEMA hao hao: Pakacha kuvuja ndiyo nafuu kwa mchukuzi.

yote yana mwisho

Upinzani wa KWELI utatokea CCM.Period.

Hizi siasa za bongo miyeyusho tu

Tuliwaambia zamani sana ila hamkusikia, sasa yanatokea ndo mnashtuka.

Ansbrt Ngurumo said:

Nataka kumtetea Zitto kidogo. Naamini kwamba hatumiwi na CCM bila kujua. Kwangu mimi, Zitto ameshavuka viwango vya kutumiwa bila kujua. Zitto ni mjanja vya kutosha, kiasi kwamba akiamua kutumika, atafanya hivyo kwa hiari yake.

Kama wanakerwa na vikao vya siri anavyofanya na vigogo kadhaa wa CCM, waseme; na watutajie majina. Kama ni Joseph Sinde Warioba au Dk. Ahmed Salim au Rostam Azizi au Edward Lowassa au Rais Jakaya Kikwete au Lawrence Masha au William Ngeleja; waseme wazi.

Maana kinachozungumzwa sasa ni kwamba mojawapo ya ajenda za Zitto kuutaka uenyekiti ni ahadi aliyopewa na baadhi ya vigogo wa CCM kwamba wanatamani kujiengua na kujiunga na CHADEMA iwapo tu, ataweza kumwangusha Freeman Mbowe katika nafasi ya uenyekiti.

Uongo wanaotumia ni kwamba wakishajimega kutoka CCM wataiwezesha CHADEMA kupata wabunge wengi mwaka 2010, na hata kuipa uwezekano wa kuwa na waziri mkuu kutoka chama cha upinzani.

Lakini hapa kuna mambo mawili. Zitto anajua kuwa mwaka 2005, chama chake kilikuwa na mpango kama huo wa kuwashawishi watu maarufu kutoka CCM wajiunge na CHADEMA kwa malengo hayo hayo.

Na mmoja wa watu waliokuwa wanawindwa katika hatua za awali kabisa ni Jakaya Kikwete na kundi lake, wakati wanamtandao wakiwa hawana uhakika wa mtu wao kupitishwa katika vikao vya CCM kutokana na tuhuma walizojua zinamwandama mtu wao, lakini pia kutokana na hujuma za kisiasa kutoka kwa vigogo kama Philip Mangula, Benjamin Mkapa, John Malecela, Frederick Sumaye na wengine ambao walikuwa wameshikilia chama na serikali; huku pia ukiwapo woga na hofu juu ya Dk. Salim Ahmed Salim.

Wanamtandao walikuwa tayari kuhama kama wangekataliwa CCM, na chama walichotaka kukimbilia ni CHADEMA.

Zitto mwenyewe anakumbuka jitihada zake za kuwanasa wanasiasa wa aina ya Zakia Meghji zilivyoshindikana, hasa baada ya yeye mwenyewe kutoboa siri hiyo kwa vyombo vya habari.

Na kikubwa zaidi, waliweza kutumia vema mbinu zao chafu, wakapenya katika kinyang’anyiro na kumpitisha mtu wao. Wakaanza mkakati na wakala yamini kumshughulikia Mbowe kisiasa na kibiashara, wakijua kuwa nguvu yake inategemewa sana kuikuza CHADEMA, na kwamba wakifanikiwa kumdhoofisha Mbowe, CHADEMA itadhoofika pia na kuwapisha kirahisi mwaka 2010.


Zitto amekuwa mmoja wa mashujaa katika vita dhidi ya ufisadi, lakini akiwa mkweli atatuambia bila kificho kuwa watu wale wale waliokuja kufahamika baadaye kuwa mafisadi, ndio waliokuwa wanaomba CHADEMA iwape nafasi walipokuwa hawajaipata CCM.

Ndiyo maana wengi wetu tunatarajia kwamba Zitto angepaswa kuwa mwangalifu sana anapoletewa masharti ya namna hii na vigogo wa CCM wanaomuahidi kujiunga CHADEMA kwa kishindo iwapo atamuondoa Mbowe.

Ndiyo maana Zitto alipojisahau akaanza kutetea ununuzi wa mitambo ya Dowans, akidhani umaarufu wake ungeweza kubadili mjadala wa kitaifa na upepo wa kisiasa, wapambanaji wenzake walimsikitikia sana, na tuhuma za waziwazi zikaanza kurushwa dhidi yake kwamba ‘kuna waliomharibu.’

Na katika siku za hivi karibuni, Zitto amesikika akizungumza katika Radio Sauti ya Ujerumani akidai kwamba tofauti ya msingi kati yake na Mbowe katika kinyang’anyiro cha uenyekiti ni kwamba ‘Mbowe ni bepari, Zitto ni mjamaa!’

WEWE Ansbert Ngurumo UMELIPIWA ADA YA SHULE na Mbowe. Chochote utakachosema humu kwa mshindani wa Mbowe ni CONFLICT OF INTEREST.

Bado natafakari suala la DOWANS, Kujitoa na kurudi tena kuwania ubunge na hili la mwenyekiti.

Kimsingi sijawahi kukutana wala kuongea na Zitto, namwona tu magazetini, JF but sisi wafuasi wake tunapata shida kumsafisha kuhusu suala la Dowans. Siasa mtaji wake ni watu, Kumbuka kupigiwa makofi sio umaarufu.

Something is seriously wrong somewhere.

Nashindwa kuilewa misimamo ya Zitto! Siku si nyingi alikuja hapa ukumbini akizungumzia kustaafu siasa ili aweze kutumikia profession aliyoisomea, mara anagombea uenyekiti wa Taifa Chadema, sasa amejitoa sijui atakuja na lipi?

By the way CHADEMA inatakiwa ioneshe muendelezo wa kipindi kilichopita, kujenga chama na kujitahidi kuwafikia zaidi wananchi na kutetea zaidi maslahi ya wananchi. Sina hakika kama hilo linaweza kufanikishwa vizuri na Zitto akiwa mwenyekiti.

Kama mafisadi wana mkono wao katika hili la sasa la kugombea uongozi Chadema basi wana-Chadema wawe makini sana.

It can be plainly seen that Zitto's head is getting to big and he is unknowingly being used, by the few elites, to demolish Chadema.
Wakuu, nimeamua kuchukua summary kwa ajili ya reference ya ambao wameanzia mjadala katikati...

Wasiwasi wangu ni kama watu mmemsoma kwa karibu Ansbert Ngurumo!
 
Ndugu zanguni naona sasa tumeongea hata tunafika mahali nadhani inakuwa shida .Tatizo la Chadema sasa katika uongozi si la kwanza katika medani za Siasa Tanzania nahata Afrika .Lugha za kusema chama kina wenyewe nao ni wachaga ni kupotosha .Wazee walio kaa na Zitto na Mbowe ni hawa

Bob Makani
Mtei E
Ngaiza
Slaa
Pro.Baregu
na nadhani kuna 2 nimewasahau.

Hebu tuanze kuangalia wachaga ni wangapi hapa na familia moja ni ipi hapo .

Hao wawili ni mzee jafari kasisiko, mwenyekiti wa kigoma na mzee victor kimesera aliyegombea ubunge kiteto.

this means wazee hao wanatoka

kilimanjaro 1 (mchaga)
arusha 1 (miraq?)
manyara 1 (masai)
shinyanga 1 (msukuma)
kigoma 1 (mha)
kagera 2 (wahaya)
 
Lakini na mimi japo nilimwamini zitto ktk hoja zake naanza kuingiwa na wasiwasi hasa nikijaribu kukumbuka alivyo handle issue ya dowans.

Magezi nakubaliana na wewe hata mimi nafurahi mno kama kajitoa.Kitendo cha yeye kushupalia kutetea suala la Dowans kwenye kichwa changu litanichukua muda kulisahau na kumsahau Zito Kabwe.Mimi ni mmojawapo wa walioshauri kwa nguvu zote na mbinu zote Kabwe asikubaliwe nafasi ya uenyekiti.Ni mapema mno tusubiri akae kwanza tumwone.Mgeni hawezi tu kuingia siku ya kwanza ujamkaribisha hadi chumbani.

Tunapopambana na ufisadi si tu na mafisadi bali pia na wapiga filimbi wao walioko ndani ya CCM,nje ya CCM kwenye vyama vingine kama CHADEMA na kwenye vyama vingine ambao wakipata nafasi nao huimba wimbo wa kusifia Dowans na hawara yake Richmond.

Mbowe ana uwezo mkubwa wa ku-organize resources. Huwezi kulinganisha na Zitto kabwe when it comes to resources mobilization and fund raising.Chama hakihitaji mwenyekiti wa kutoa tu hotuba kama ilivyo CCM ambako resources zinakuwa mobilized na watu nje ya mwenyekiti ambao baadaye wanatumia fursa hiyo kumfunga mdomo naye anaogopa kuwakemea wakifisadi au kutetea ufisadi kwa kuhofu 2010 atapata wapi resources za kampeni.

Mbowe asiondoke aendelee kuwa mwenyekiti.Kama ana udhaifu tunaujua lakina uwezo wake ni mkubwa kuliko udhaifu wake ukiweka kwenye mizani hivyo aendelee.Ni mtunzaji wa siri za chama na mpiganaji asiyeyumba wala kuyumbishwa.
 
Wanabodi,
Sina hakika na utaratibu wa Chadema na vyama vinginevyo ktk Uchaguzi wa viongozi ngazi ya juu ktk chama..
Binafsi nilitegemea sana viongozi kuwa selected na Caucus badala ya watu kujiandikisha kugombea nafasi za Uongozi ndani ya chama..
I Mean, Chadema kama chama kinaweza kuongozwa na mtu mfano wa kina Rostam ambaye kwa kutumia tu kadi ya chama ana uwezo wa kugombea nafasi kubwa ya uenyekiti kwa kutumia fedha au Umaarufu..
Wakuu zangu nitaendelea zaidi kupingana hili neno Domkrasia linavyotumika, kwa sababu Nijuavyo mimi Demokrasia itakuwa Demokrasia tu ikiwa kuna Upinzani wa kimawazo baina ya wagombea wawili na sii lazima kila sehemu neno hili litumike..Kwa mfano Huwezi gombea nafasi ya Uongozi Chadema ikiwa wewe sii mwanachama, sasa kuna mtu anaweza kusema hiyo sii Demokrasia.. kwa nini wasiachie mtu yeyote agombee nafasi ya Uongozi..
Ni kwa sababu Demokrasia inatanguliwa na mgongano wa kimawazo na ushindani huo unapokomaa na kuwa unahitaji kura za wahusika ndipo ushindani huo wa kimawazo hupewa uhuru na nafasi sawa kujitangaza kwa wahusika ili uchaguzi (election)ufanyike.. Sasa Ikiwa Zitto hakubaliani na Uongozi wa Mbowe na amekuja ya mfumo tofauti wa kimawazo mathlan hakukubaliana na wazo la chama kutoka Mrengo wa kati Kulia na kuwa mrengo wa Kati, basi hizo fikra zake ndizo zitatangulia Kuwakilishwa na sii haki na Uhuru wa demokrasia kama inavyotangzwa hapa..

Mwenyekiti wa chama ni nafasi nyeti sana ya chama na binafsi naamini kabisa sii nafasi inayostahili kila mtu kugombea bali ni nafasi ambayo Kila Mwanachama atapenda kuongozwa na mtu fulani. Mathlan Katika mkutano mkuu wa chama majina hupendekezwa na wanachama kisha moja likachaguliwa kuchukua nafasi hiyo badala ya kila mtu kuchukua form na kujiandikisha kugombea nafasi ambayo kwa nchi maskini kaa Tanzania inaweza pokonya nguvu ya haki na uhuru wa wananchama. Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK ni Wenyeviti waliopitia mfumo unaokubalika zaidi ya huu wa Chadema na hii Demokrasia yenu..

Naomba kuwakilisha, na sina sababu ya kumchukia mtu yeyote kati ya hawa ndugu zetu lakini sidhani kama hata CCM hufanya election kuchagua Mwanyekiti wa chama chao yaani JK alichuana na baadhi wanachama waliochukua form kugombea nafasi hiyo hiyo ya Uenyekiti wa chama.
Kifupi sioni sababu kabisa ya nafasi nyeti ya chama kama Mwenyekiti Igombewe na wanachama kwa kutumia Demokrasia, bila kuzingatia ethics na hatua za makuzi ya fikra zinazokiongoza chama.. Yaani kwa mtazamo wangu huwezi kuwa Sheikh au Padre kwa kutumia Demokrasia isiyokuwa na kipimo cha elimu, umri na wokovu wa mhusika ktk imani hiyo. Na wala sii haki kutumia mtazamo wetu finyu kukosoa Uongozi wa Kanisa au msikiti kwa madai ya Demokrasia ikiwa utaratibu wa dini hiyo unahitaji elimu, umri au kupitia ngazi fulani kabla hujafikia kuchukua kiti cha Upadre au Kuongoza Msikiti...

Hivyo ikiwa Chadema wanasdema Zitto hana Umri unaotakiwa na pengine kasoro fulani fulani ni jukumu letu kuangalia masharti ya Uongozi ndani ya chama hicho kwani sii lazima mfumo wa Uongozi Chadema ufanane na ule wa CCM, CUF au TLP..Katiba ya chama Chadema inasema nini katika kugombea kiti hicho..
 
Last edited:
Mnajua ndo maana namba wani (CCM) wataendelea kutamba miaka nenda rudi, Wa wapi NCCR, wa wapi CUF? Yaani, kila chama cha upinzani kinachoanza kujipatia jina wanaanza kurogana wenyewe kwa wenyewe ndani kwa ndani. Na wakati huo huo CCM wakiwa pembeni wanagongeana tano kwani kazi ambayo wangetakiwa waifanye wao inafanywa na watu wa hivyo vyama bila hata wakati mwingine CCM kutia mkono wao.
Sababu kama hizi ndo zinanesha jinsi gani bado CCM watandelea kuwa kidedea kwa miaka mingi.

Pia sitashangaa Zitto out of frustration akihamia CCM!, watch this space!!
 
Mnajua ndo maana namba wani (CCM) wataendelea kutamba miaka nenda rudi, Wa wapi NCCR, wa wapi CUF? Yaani, kila chama cha upinzani kinachoanza kujipatia jina wanaanza kurogana wenyewe kwa wenyewe ndani kwa ndani. Na wakati huo huo CCM wakiwa pembeni wanagongeana tano kwani kazi ambayo wangetakiwa waifanye wao inafanywa na watu wa hivyo vyama bila hata wakati mwingine CCM kutia mkono wao.
Sababu kama hizi ndo zinanesha jinsi gani bado CCM watandelea kuwa kidedea kwa miaka mingi.

Pia sitashangaa Zitto out of frustration akihamia CCM!, watch this space!!

Mkuu usiseme hivyo ni mkono wa CCM/mafisadi wamemrubuni zitto na nadhani zitto hafai tena kuwa hata mbunge, kaisha vimba kichwa lakini la DOWANS analo tu mpaka mwisho wake.
 
Mimi nimesikitishwa na nikiwa kama mwamanchama wa CHADEMA nitarudisha kadi yangu rasmi, nimechoka kuona hivi vitimbi. Sasa kama uenyekiti wa chama tu inakua ni kwa kukwaruzana kihivi, je tukiwapa nchi si ndio watagoma kung'atuka madaraka na kuanza kubadilisha katiba ili watawale milele?

Kwani mbowe ameshushwa kutoka mbinguni kuja kuwa mwenyekiti wa CHADEMA? Je huo umri unaozungumziwa hapo, je katiba ya CHADEMA hapo wazi kusema umri ni miaka mingapi?

By the way, nini maana ya neno uchaguzi kama atagombea mtu mmoja, huo uchaguzi wa kuchagua utatokea wapi sasa? Je tunaweza kuita huo ni uchaguzi au ni kumsimika Mbowe "to annoit"? Na je kama watu hawataki kumchagua Mbowe watamchagua nani sasa? Hapa ndipo utaona dhahiri sasa ugumu wa kufikiria, ufinyu wa mawazo na upeo mdogo tulionao sisi watu wenye ngozi nyeusi...!

Kwa manufaa ya CHADEMA na kwa manufaa ya demokrasia ningeshauri hao CHADEMA wondokane na hio aibu kubwa kabisa ya kumnyima mtu kugombea madaraka. Infact, kama nia ni kugombea Uraisi ambao mbowe ndio anautolea macho sio lazima mwenyekiti wa chama tu ndio awe na uwezo wa kuteuliwa na chama kugombea uraisi, chama kinaweza kikamchagua mtu yoyote yule kusimama na kugombea uraisi endapo kitaamua kuweka mgombea, lakini kwa sasa naona itakua ni upotevu wa rasilimali endapo vyama vya upinzani vitasimamisha mgombea wa uraisi kwani bado hata Ubunge tu umewashinda, sembuse uraisi?

Vyama vya siasa vinataka kupoteza maana ya kuwepo. Haya ni mambo yasingechukua muda. Na pili kinachotakiwa siyo uenyeketi bali kuwa na wabunge wengi zaidi ya CCM. Upinzani utakapoelewa hili watakuwa wamejipanga sawa sawa. Kwa sasa hata hao wenyeviti wagombee ubunge!
 
Lunyungu said:
Unajua mie nachoka sana kila mara watanzania mnapo kuja hoja nyepesi .Huko CCM kuna ujinga kibao ikiwa ni pamoja udini kumea hadi nje lakini no talking about it .CCM ina miaka mingapi ukilinganisha na Chadema ? Jamani we all know kwamba wakati vyama vina anzishwa watu wengi kama ilivyo walikuwa ni watu w akudharau kwaba wapinzani ni wapuuzi hawawezi kufika popote .Leo wamefika mahala pamoja na shida zao na uchanga nk bad utasikia Michaga mara wadini .Hivi kama watu hawaendi kwenye Chama na kugombea nafasi mnataka kesho kitokee nini ?
Nadhani this is to low hakika .Uongozi wa Chadema juu kuna Mbowe hadi sasa haya tuje chini huku tuona kuna wachaga wangapi akina Zitto ni wakristo ama wachaga akina Slaa ? Hebu tuangalie shida iliyoko mezani muda huu na si zaidi ya kuleta habari za akina Tambwe .CCM ina ukabila udini na hata ukanda kama wabisha angalia viongozi wote wakubwa wa CCM wakwepo akina Tambwe wanatokea wapi linganisha na Chadema.

Chadema they made a mistake kwenye viti maalumu nadhani hawatakaa warudie lakini pia lazima watu wajitolee kushiriki siasa wapate hizo nafasi na si kulalama tu.

Lunyungu,

..hizi shutuma za ukabila na udini Chadema wenyewe mmeshindwa kuzishughulikia.

..tena ni tatizo kubwa kiasi kwamba hata kuna baadhi ya viongozi waandamizi[mfano chacha wangwe] walikuwa na hisia hizo.

..hili somo kwamba Chadema haina udini wala ukabila ni somo ambalo Watanzania wameshindwa kulielewa. Chadema mnapaswa kuwasaidia ktk hili, kama ambavyo mwalimu anapolazimika kuweka pass-mark ndogo ili wanafunzi wengi wafaulu.

..kwasababu hizo hapo juu ndiyo maana naona Chadema wangempa nafasi Zitto Kabwe ili kuondokana na ile dhana kwamba chama chao ni mali ya Wachaga na Wakristo.

NB:

..unasema watu wajitokeze, Zitto huyo amejitokeza na Chadema mlipaswa ku-jump on the opportunity to have a non-Chaga party Chairman.
 
Kifupi sioni sababu kabisa ya nafasi nyeti ya chama kama Mwenyekiti Igombewe na wanachama kwa kutumia Demokrasia, bila kuzingatia ethics na hatua za makuzi ya fikra zinazokiongoza chama.. Yaani kwa mtazamo wangu huwezi kuwa Sheikh au Padre kwa kutumia Demokrasia isiyokuwa na kipimo cha elimu, umri na wokovu wa mhusika ktk imani hiyo. Na wala sii haki kutumia mtazamo wetu finyu kukosoa Uongozi wa Kanisa au msikiti kwa madai ya Demokrasia ikiwa utaratibu wa dini hiyo unahitaji elimu, umri au kupitia ngazi fulani kabla hujafikia kuchukua kiti cha Upadre au Kuongoza Msikiti..

Mkuu heshima mbele, lakini nikukumbushe tu kuwa huwezi kuokoka hapa duniani.
 
Mkuu heshima mbele, lakini nikukumbushe tu kuwa huwezi kuokoka hapa duniani.
Hata sikuelewi mkuu wangu, kama wewe huamini Sheikh au Padre wako ana Practice what he Preach, huo wokovu unautegemea vipi huko mbinguni au sijui wapi!..
Hata hivyo mkuu wangu bila shaka imani yako ni tofauti na yangu kwani naamini kabisa hakuna wokovu mbinguni kama hakuna wokovu hapa duniani..Yaani pepo unaitengeneza hapa duniani na sii Mbinguni, kule ni ktk matunda ya kile ulichokifanya hapa duniani.
 
Jamani hivi Mzee Mwanakijiji upo? sijaona mchango wako ktk hili sakata la zitto
 
Nitarudia kusema hivi:-
Mwenyekiti wa chama ni nafasi nyeti sana ya chama..Sio nafasi inayostahili kila mtu kugombea bali ni nafasi ambayo Kila Mwanachama atapenda kuongozwa na mtu fulani...
Mathlan Katika mkutano mkuu wa chama majina hupendekezwa na wana caucas kisha jina moja likachaguliwa kuchukua nafasi ya mwenyekiti badala ya kila mtu kuchukua form na kujiandikisha kugombea nafasi hiyo.
Nyerere, Mwinyi, Mkapa na JK ni Wenyeviti waliopitia mfumo unaokubalika zaidi ya huu wa Chadema na hii Demokrasia yenu..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom