Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Watanzania ni wagumu kweli kweli kuelewa. Chinga amelalama weeee lakini hamkumuelewa.Wana JF si kawaida yangu kuandika sanasana na imenilazimu leo... Tangu zamani niliamini kuwa CHADEMA kinaweza kuwa chama cha 'Demokrasia' na daima kitaruhusu 'Demokrasia' kuchukua mkondo wake lakini tunapoelekea inaelekea sivyo.
Naam, nazungumzia kikao kilichofanyika leo na 'wazee' wa CHADEMA kuanza 'kumshinikiza' Zitto Kabwe kuondoa jina katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti.
Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.
Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...
Kama ni kuondoa basi wote wawili (Zitto na Freeman) waondoe majina na ifikiriwe namna mpya.
Katika hili, mmechemsha!
Yaani mambo yapo hivi, CHADEMA kinakuwa chama cha kidemokrasia pale tu ambapo uongozi wa juu unabaki Moshi. Katika hili hakuna majadiliano.
Ikiwa kama ni Ndesamburo ndie aliyegombea, baraza la wazee usingelisikia na wote wangeenda katika uchaguzi na kihalali kabisa aliyeshinda ndiye angekuwa mwenyekiti.
Sasa kitachofuata ni kiini macho, yaani wote watajitoa halafu Ndesamburo ndiye atagombea. Kaa uonelakini usije ukaniita mimi mganga au mchawi.