http://www.chadema.net/blogu/zitto/
Je, baadhi za maneno haya ya wakati ule yanasimama na kuwa na maana katika hali ya sasa? TUJADILI;
Thursday, November 02, 2006
Uchaguzi wa Afrika Mashariki - Demokrasia yabakwa
Leo Bunge la Tanzania lilitakiwa kuchagua wawakilishi wake katika Baraza la kutunga sheria la Afrika Mashariki (East African Legilstative Assembly). Uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge la Tanzania, Mkataba wa Afrika Mashariki na kanuni ndogo za uteuzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki. Leo tumeshuhudia, kwa mara nyingine tena, CCM wakitumia wingi wao ndani ya Bunge kuminya demokrasia na kukanyaga bila woga maslahi ya nchi yetu.
Kanuni za Bunge na Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinataka uwakilishi uzingatie uwiano wa vyama ndani ya Bunge.
Kambi ya upinzani ilitengewa nafasi moja tu licha kuongeza viti vyake kutoka 17 mwaka 2001 mpaka 45 mwaka 2006. Na hata hako ka nafasi kamoja ka upinzani CCM wameamua kuwachagulia kwa kumpa kura Mzee Msha ili kumpa zawadi John Cheyo ambae siku hizi anaimba nyimbo za CCM. Nikikumbuka kuwa Cheyo ndie mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC), machozi yananitoka kwani sasa serikali itaponda mali ya umma itakavyo maana hakuna chombo ya kuizuia. Cheyo ameshapewa carrot!
Katika Bunge la Afrika Mashriki kuna nafasi tatu kutoka Zanzibar. Kanuni inasema uwiano wa vyama. Zanzibar CUF na CCM zipo neck to neck. Lakini nafasi zote za Zanzibar zimechukuliwa na CCM. Maslahi ya Zanzibar katika Afrika Mashariki yapo mashakani.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni anaomba mwongozo wa Spika ndani ya Bunge, Spika anafoka na kutishia. Haki imaminywa.
Niliamua kutoka nje ya Bunge na kususia uchaguzi. nikiungana mkono na wabunge 4 wa CHADEMA na wabunge wote wa CUF. Wabunge mashujaa wa CHADEMA waliotoka ni Bi. Halima Mdee, Bibi Maulidah Anna Komu na Chacha Zakayo Wangwe.
Kwa nini nimewalk out? Ni kwa sababu ya Principle - Misimamo isiyoyumba.
Mimi niliamua kuwa mtu wa principles mara tu niliamua kuanza siasa.
Nilitoka nje ya Bunge kwa sababu sikutaka kuingia katika histroia ya kukanyaga demokrasia. Ninaamini uchaguzi huu ni batili kwa sababu kanuni za Uchgauzi hazikufuatwa toka mwanzo wa mchakato.
Siamini katika CCM kutuchgaulia wapinzani Mbunge wake.
Siwezi kuramba miguu ya CCM, chama ambacho asilimia 90 ya wabunge wake wameingia Bungeni kwa takrima (soma rushwa). Walk out, ni kuonesha kuwa siridhiki na mchakato wa uchaguzi. Sikubaliani na kuburuzwa.
Ninawajutia Watanzania. kuamua kuchagua Bunge lililojaa chama kimoja. Hawapati thamani ya kura zao.
Najiuliza. Katika hali kama hii ya demokrasia ndani ya Bunge. Kuna haja ya kuwa Mbunge? Sipati Jibu. Nachanganyikiwa.
Je, hakuna njia nyingine ya kuimarisha demokrasia katika nchi? Demokrasia ya vyama vingi. Natafuta kitabu kinachoitwa 'ending one party dominance: Doroth Solinger. yeyote atakayepata kitabu hiki popote pale, anifanyie utaratibu nikipate. Labda nitapata mikakati ya kuimarisha demokrasia ya vyama vingi nchini.
Ni kupitia Bunge lenye angalau theluthi ya Wabunge kutoka upinzani, ndio Watanzania watapata thamani ya kura na kodi wanazolipa. Vinginevyo, nikitumia msemo wa Freeman Mbowe Bunge litabaki kuwa mchezo wa kuigiza katika Luninga (rejea makala za Freeman Mbowe za mwaka 2003).
Natoa wito kwa vijana wa Tanzania mliopo popote duniani, tuungane kuimarisha demokrasia nchini petu. This is a noble call. Wale wanaoweza kushika majimbo na waseme mapema ili tuyaandae majimbo yao, wale wasioweza wachangie mawazo na rasilimali ili kuweka miundombinu ya demokrasia katika nchi yetu. Muundombinu mkubwa ni vyama imara vya siasa vyenye mtandao mpana na sera za uhakika na zinazotekelezeka. Inawezekana, timiza wajibu wako katika ujenzi wa demokrasia.
Uchaguzi wa Afrika Mashariki - Demokrasia yabakwa
Leo Bunge la Tanzania lilitakiwa kuchagua wawakilishi wake katika Baraza la kutunga sheria la Afrika Mashariki (East African Legilstative Assembly).
Uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge la Tanzania, Mkataba wa Afrika Mashariki na kanuni ndogo za uteuzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki. Leo tumeshuhudia, kwa mara nyingine tena, CCM wakitumia wingi wao ndani ya Bunge kuminya demokrasia.
Kanuni zinataka uwakilishi uzingatie uwiano wa vyama ndani ya Bunge. Kambi ya upinzani ilitengewa nafasi moja tu licha kuongeza viti vyake kutoka 17 mwaka 2001 mpaka 45 mwaka 2006. Na hata hako ka nafasi kamoja ka upinzani CCM wameamua kuwachagulia kwa kumpa kura Mzee Msha ili kumpa zawadi John Cheyo ambae siku hizi anaimba nyimbo za CCM.
Nikikumbuka kuwa Cheyo ndie mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC), machozi yananitoka kwani sasa serikali itaponda mali ya umma itakavyo maana hakuna chombo ya kuizuia. Cheyo ameshapewa carrot!
Katika Bunge la Afrika Mashriki kuna nafasi tatu kutoka Zanzibar. Kanuni inasema uwiano wa vyama. Zanzibar CUF na CCM zipo neck to neck. Lakini nafasi zote za Zanzibar zimechukuliwa na CCM. Maslahi ya Zanzibar katika Afrika Mashariki yapo mashakani.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni anaomba mwongozo wa Spika, Spika anafoka na kutishia. Haki imaminywa.
Niliamua kutoka nje ya Bunge na kususia uchaguzi. nikiungana mkono na wabunge 4 wa CHADEMA na wabunge wote wa CUF. Kwa nini nimewalk out? Principle. Mimi ni mtu wa principle. Sikutaka kuingia katika histroia ya kukanyaga demokrasia. Ninaamini uchaguzi huu ni batili kwa sababu kanuni za Uchgauzi hazikufuatwa toka mwanzo wa mchakato. Siamini katika CCM kutuchgaulia wapinzani Mbunge wake. Siwezi kuramba miguu ya CCM, chama ambacho asilimia 90 ya wabunge wake wameingia Bungeni kwa takrima (soma rushwa). Walk out, ni kuonesha kuwa siridhiki na mchakato wa uchaguzi. Sikubaliani na kuburuzwa.
Jambo la ajabu ni kwamba, hata wagombea hawakuruhusiwa kuwa na mawakala katika kuhesabu kura. Uchaguzi haukuwa na uwazi wowote. Tutaamini vipi kuwa wagombea walipata kura zilizotangazwa? Demokrasia inakanyagwa.
Ninawajutia Watanzania. kuamua kuchagua Bunge lililojaa chama kimoja. Hawapati thamani ya kura zao.
Najiuliza. Katika hali kama hii ya demokrasia ndani ya Bunge. Kuna haja ya kuwa Mbunge? Sipati Jibu. Nachanganyikiwa. Je, hakuna njia nyingine ya kuimarisha demokrasia katika nchi? Demokrasia ya vyama vingi. Natafuta kitabu kinachoitwa 'ending one party dominance: Doroth Solinger. yeyote atakayepata kitabu hiki popote pale, anifanyie utaratibu nikipate. Labda nitapata mikakati ya kuimarisha demokrasia ya vyama vingi nchini. Ni kupitia Bunge lenye angalau theluthi ya Wabunge kutoka upinzani, ndio Watanzania watapata thamani ya kura na kodi wanazolipa. Vinginevyo, nikitumia msemo wa Freeman Mbowe Bunge litabaki kuwa mchezo wa kuigiza