Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Zitto kishakula za mafisadi,anajiandaa kwenda CCM...hana lolote anatafuta kula tuu!

Kweli kabisa ... sasa inasubiriwa tu ni wizara gani atapewa maana toka aimalize issue ya Buzwagi kiaina kwa kuingia kamati ya Kikwete, wakulu wa chama la kijani walikuwa wanamuandalia zawadi ya nguvu.
 
- Hii ni JF kumkoma nyani hatujawahi kuogopa mtu hapa wala ishu, tumewanyamazia toka majuzi tukidhani mtayamaliza huko Chadema kwa manufaa ya masilahi yetu wananchi,

- Sasa mmeharibu halafu mnajaribu tena kuja hapa JF ku-spin nonsense! Mkulu PM tumejaribu sana kuwaheshimu na hili lakini mlichofanya ni aibu kubwa sana, sasa muacheni Zitto ajimalizie zaidi, lakini jaribuni kukinusuru chama Chadema kwa kufunga midomo yenu sasa.

Ni ushauri wa bure tu, Zitto hana anything to lose ila ana everything to gain, hapa na hizi behavior zake naona inapaliliwa njia ya kwenda CCM hebu nyamazeni msijiabishe zaidi maana he is taking down the whole chama mnapozidi kumuandama. Nimewaambieni siku nyingi sana kwamba Chadema mna matatizo ya washauri kama CCM, how can you fight Zitto at this stage alipofikia? Halafu uka'expect ku-win?

Respect.

FMEs!

Ila Zitto kwa sasa hivi ccm itamfaa zaidi kuliko chadema maana mambo aliyosema leo na ambayo anaendelea kuyasema hayana tofauti na Hiza.
 
- Haya niliyasema siku nyingi sana nenda kwenye thread za ile ishu, mkanishupalia sana hapa na uchunguzi wangu, sasa mnaona mwenyewe Zitto amekubali,

- Mkulu Ushiwarombo uko wapi maana wewe ndiye uliyekua mbishi sana kwamba ninatunga zile habari za kupatikana kwa text messages kuhusu computers kati ya yule kijana aliyeko jela na mbunge mmoja maarufu sana, sasa si uona haya ya leo yanajisema yenyewe! Aibuu!

Respect.

FMEs!

Hapana mkuu sio mimi ,mimi nilikuwa upande wa Wangwe mpaka kesho.
 
mkuu umenena ...nimeona loophole mbaya sana ambayo inaweza kutumiwa na maadui wa zitto na maadui wa chadema ...ieleweke kuwa kila chama kina siri zake......na moja ya sifa ya kiongozi ni kuhifadhi...sasa siwaelewi watu wanaomshabikia zitto kuropoka wakati wanajuwa amejipotezea sifa ya kuaminika kuhifadhi mambo mazito..ukizingatia kati ya vijana wa umri wake ni front runner to presidency....sasa unafikiri watu wa usalama faili lake leo wataongezea comment gani....hasa ukizingatia uzito wa siri viongozi wanazobeba..

hapo nyuma nimewakumbusha kuwa pamoja na mrema kutofautiana na chama cha ccm ...hadi leo hajatoa siri hata moja zaidi ya viti ambavyo kila mtu alijuwa kama chavda..etc..hasa ukizingatia nafasi yake kama mkuu wa usalama ccm,mbunge ,waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu..

nahisi kuwa tutakuwa na tatizo la kiusalama huko mbeleni...kama idara ya usalama haitachukua jukumu la kutoa mafunzo ya maadili na uongozi kwa vijana wote wanaopata nafasi kubwa au ubunge hata wa upinzani...nimesikitika sana ...maneno ya kuropoka angetoa mtu kama hiza au aina yake nisingesikitiaka ...lakini zitto ni kijana tunayemtegemea ..kwenye hii safari...!!!..lazima awe na maadili ya uongozi ...kubalini kataeni sifa ya muhimu tunayoangalia kwa kiongozi ni kutunza siri!!!

wanaomshabikia mbona hawajiulizi kusikia siri zaidi ya tetesi kuhusu ...sokoine,kolimba.,na wengine wengi...??????.. au ccm hawana midomo???

Hizo siri ndizo zimetufikisha hapa acha watu wamimine,unajuwa mkifanya kitu harafu mwingine akaenda kukitema kana kilivyo ,siku nyingine mtaogopa kufanya kwa ze said siri.

kwa hili nipo na zitoo 100% kama nilivyokuwa na zakayo wangwe marehemu
 
Field marshall ES,
Mkuu hakuna mtu anayezungumzia kuenguliwa kwa Zitto ktk kugombea uenyekiti. Kwanza ni swala la chama Chadema halikuhusu kitu wewe mbona Malecela alienguliwa.. Kuna majina kibao yaliernguliwa kabla jina la Mama Asha Rose Migiro halijapigiwa kura huko UN, tena Kenya wanalia hadi kesho kwani walitegemea mtu kutoka kwao kushika nafasi hiyo.. Kila sehemu ya taasisi duniani huwa na mchekecho wa majina unaoweza kuengua jina la mtu yeyote kutokana na mapungufdu wanayoyahitaji wao..Imetokea CCM, imetokea CUF imetokea UN na vyama kibao vya kisiasa hadi nchi zinazodai kuwa na demokrasia ya kweli. Mkuu, angalia nyumba yako huwezi kutuchagulia mke hata kidogo. Sifa za zinazotakiwa kugombea kiti cha mwenyekiti CCM haziwezi kuwa sawa na vyama vyote na demokrasia haiwezi kukiuka SIFA zinazomwezesha mgombea ku qualify..who knows pengine Zitto hakuwa na sifa hizo...

Pamoja na yote haya sisi tulikwisha elewa kitu gani kinafanyika, njama zote against Zitto zilijulikana lakini tatizo letu ni Zitto mwana JF sio wajinga wengine. tatizo ni pale kiongozi wetu huyu anapojibu mapigo ya paparazi kwa hamaki bila kufahamu kwamba naazidi kutuweka Uchi.. Hakujibu kwa kutumia hekima, alikichafua chama na wote waliokuwepo sawa na mke/mme anayekwenda hadithia marafiki zake negative vibes kuhusu mwenza au kinachofanyika ndani ya nyumba yake.. Ikiwa mashtaka ni halali nenda Polisi au vyombo vya sheria sio kuanika na kulia lia kwa majirani ukifikiria watakuonea huruma sana kumbe ndio kwanza unaharibu ndoa yako..Hizi ndizo lawama zetu kwa Mh. Zitto...Mkuu unajua fika kuwepo kwa watun kama hawa na wameharibu ndoa zao iwe mwanamke/ mwanamme..

Kama swala lilikuwa kuenguliwa kwa jina lake ingebakia kuwa somo hilo na lawama zake zingewafuata wahusika ktk kikako cha chama kwani hakijaisha bado. Tofauti na Lwakatare ambaye aliahidiwa mengi wakati wa kikao Zitto kabahatika kuyaona yote dhidi yake wakati wa kikao, hakuwa na sababu ya kulalamikia pembeni ktk magazeti.

Tumeona ya Spika Sitta ktk kikao cha CCM lakini kwa busara zake mzee hakuweka vitisho, matusi na kuvaa gloves tayari kurusha ngumi..kwa sababu maslahi ya chama chake yako mbele ya tuhuma alozushiwa. na bahati Ukweli umetoka na Mafiosadi haswa wanajulikana walichojaribu kufanya. Ndani ya Chadema pia wapo mafisadi na Zitto hana sababu wala haja ya kujilinda kwa maneno wala kukurupuka kudai yeye sii Fisadi..Kauli na Vitendo vyake pekee ndivyo vinaweza kumsafisha na wala hakugombea Uengozi ili kufurahisha watu. Kuna problem ndani ya chama ni jukumu lake kurekebisha tabia hizo zikome na kama atashindikana ktk vikao vyote vya vyama basi hana sababu wala haja ya kuendelea kukaa chama hicho. Na bila shaka Wapiganaji wengi tungemfuata.. nashindwa kuanmini kwamba hata Dr. Slaa mpiganai mwingine amewekwa ktk kundi baya halafu mtetezi mkubwa wa Mh. Zitto ktk kikao cha chama ametokea kuwa ni mama yake!.. Hii kweli inaingia akilini mkuu wangu?.. Kuna Ujinga unaendela na sii Zitto mwenyewe ila wapambe wake ndio wanaharibu kabisa!

Nafikiri Malecela hakuondolewa jina lake ila mafisadi walipiga kampeni za kifisadi akatolewa kwa kura ktk round ya mwanzo.Habari ndiyo hiyo.
 
MkamaP,
Una hakika na unayoyasema?
Unafikiri Malecela angeruhusiwa kugombea angeondolewa round ya kwanza! thubutu....bila shaka umesahau kuwa Wazee wa chama walimwita na kumwambie ajikate akataka kukata rufaa ikapigwa chini vile vile..Malecela angeiingia ktk Kura nina hakika angefika final ya watatu..Kifupi kuna majina kibao yalienguliwa na wazee wa chama. Hili ni jambo la kawaida kabisa ktk chaguzi nyingi za chama au taasisi.
 
MkamaP,
Una hakika na unayoyasema?
Unafikiri Malecela angeruhusiwa kugombea angeondolewa round ya kwanza! thubutu....bila shaka umesahau kuwa Wazee wa chama walimwita na kumwambie ajikate akataka kukata rufaa ikapigwa chini vile vile..Malecela angeiingia ktk Kura nina hakika angefika final ya watatu..Kifupi kuna majina kibao yalienguliwa na wazee wa chama. Hili ni jambo la kawaida kabisa ktk chaguzi nyingi za chama au taasisi.

unasema mwaka gani?

kama ni 2005 alipigwa chini kwa kura za kifisadi(siasa za maji taka),raundi ya kwanza alikuwepo malecela,mwandyosya,karume ,ahmed,kikwete na balozi wa urusi.

wakaingia round ya pili watatu ahmed,kikwete na mwandosya.
habari ndo hiyo.

Ni sahihishe kama nimekosea
 
Ndugu zangu,

Huyu aliyeandika post hii ni mmoja wa vijana wa makao makuu ya CHADEMA ambaye amekuwa akinipinga siku zote kwa chuki tu ya kuwa mimi nimepaata umaarufu wa kisiasa kuliko yeye na kundi lake.
"mimi nimepata umaarufu wa kisiasa"
bwana maarufu angalia matumizi yako ya keyboard, au ndio umaarufu umekuzidi mpaka umenogewa


Pili, ni dhahiri kulikuwa kuna makundi katika uchaguzi wa BAVICHA. Mimi niliweka wazi msimamo wangu wa kumwunga mkono kafulila. Wakurugenzi wa Makao makuu ya chama kuanzia Katibu Mkuu mpaka wakurugenzi kama John Mnyika, John Mrema na hata maafisa kama Halima Mdee walikuwa wanampinga David Kafulila. Hawa wanaogopa uwezo wa Kafulila wa kukataa kutumika na kuwa independent katika maamuzi yake.
kwani haya uwezi kuyaongea faragha mkamalizana mpaka uyaweke hapa jamvini, huoni kwamba hii ni kuongeza mfarakano baina ya wewe na viongozi wenzako
sasa hivi kila mtu anajua kuwa mnyika, mrema wanamuogopa kafulila kwa ajili ya maamuzi yake. kweli hii ndio staili nzuri ya kujenga chama kwenye public.


Ninaomba sana vijana wa Makao Makuu - hasa Mrema, Mnyika na wengineo waache spinning za kipumbavu ambazo hazijengi umoja na mshikamano wa chama. Waache kuchafua jina langu. Wakumbuke kuwa kuna maisha mbele yetu na kuna kazi ya kujenga chama chetu.
Je na wewe kuja kuwaomba hapa jamvini waache kuspini sio kuspini pia? huoni kwamba unaspin kwana wana JF kuwa mnyika na mrema hawakutakii mema

Vijana hawa wakumbuke kuwa majungu hulipwa hapa hapa duniani. Wasubiri nao watakuwa wabunge na watapata ajenda zao za kuwafanya kuwa maarufu.
bwana maarufu again

Wakumbuke pia mimi na Mbowe tunafahamiana kabla yao na tutakaporekebisha tofauti zetu na kugundua wapambe nuksi watakuwa kwenye aibu kubwa. Dunia hadaa!
***kwa hiyo wewe umeingia kwenye kinyanganyiro kwa ajili ya wapambe kukuchonganisha wewe na mbowe
***kumbe ni tofauti zako binafsi wewe na mbowe ndio zimekufanya ukagombee uenyekiti


Kafulila kashinda uenyekiti wa vijana. Mpeni ushindi wake. Msibake demokrosia.
final nail in the coffin

bwana zito sijui ni nini lakini angalia sana matumizi ya lugha zako yaani hili tamko lako lina vitu vingi sana ambavyo ungetakiwa usiviandike...
kama ulivyosema wapambe, angalia sana hao wapambe na kama ndio wamekushauri uandike hivi ujue wapambe wako hawakufai utafute wengine ASAP


kila la kheri.....
 
Vibabu vya Chadema vitakiua chama, yaani wao ndio wamekuwa waamuzi wakuu wa mambo mbalimbali ya Chama, labda ni katiba yao lakini sidhani njia wanayoitumia ni demokrasia ya kweli kwa sababu hata Komunisti China nao wana katiba inayofuatwa huku ikiwanyima haki za msingi wananchi. Sidhani kama ilikuwa ni haki kumshauri Zitto ajiengue kutoka kwenye kugombania uenyekiti wa Chama, kwa hiyo pia kama kutakuwa na mtu mwingine akiamua kutaka kuwa mgombea wa urais kupitia Chadema nae atazuiwa ili Freeman Mbowe apitishwe bila ya kupingwa. Hii ni demokrasia ya Kifisadi isiyofaa kabisa na haina tofauti na ile ya Chama Cha Mafisadi (CCM). Kwa sababu binafsi naamini mtu anaefaa kugombea urais kutoka Chadema kutokana na kuwa na sifa zote za Rais anaeweza kuiletea madadiliko makubwa Tanzania ni Dr. Wilbroad Slaa na sio Freeman Mbowe.

Chadema mmeshaanza kulikoroga hata kabla hamjapewa nchi, hii inatia shaka sana kama mtaweza kuleta mabadiliko ya kweli ambayo CCM imeshindwa kuyaleta kwa miaka yote ambayo wako madarakani.

Nyinyi mnaomlaumu Zitto kwa uamuzi wake wa kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa Chadema inaonyesha ni jinsi gani mmelelewa na CCM kupitia siasa zake mbovu za Kijamaa. Demokrasia ya kweli inaruhusu mwanachama yeyote kugombea uongozi katika chama, Kama vibabu wa Chadema wanaogopa Freeman kushiriki kwenye chaguzi na Zitto hivi kweli atamuweza Kikwete wa Mafisadi CCM??
 
This is part of spinning. Uwongo, uzushi nk. Tatizo wanaopanga haya wanasahau kuwa tuliyapanga wote dhidi ya marehemu Chacha Wangwe. Unatengeneza uwongo, unausambaza, na hatimaye wewe mwenyewe unauamini kuwa ni kweli.

Kama kuna kitu kilimuuma marehemu wangwe na alikufa nacho ni kile cha kumsema kuwa alikuwa anatumiwa na mafisadi. Namshukuru Mungu kuwa nilimwomba radhi Chacha kabla na baada ya kifo chake siku ya postmorterm kwa kumzushia uwongo.

Asha ni mmoja wa wenzangu tulioshiriki kumtenda Chacha. Wanatumia mtindo ule ule na wanapita njia zile zile. Rashidi wa Kuli alisema, YANA MWISHO HAYA!

Asha, (ninakujua wewe ni nani) kuwa mkweli wa nafsi yako! Utalipwa hapa hapa duniani kwa uzushi wako na wenzako.

To put record clear - Kasisiko sio ndugu yangu wa damu. Ni mwenyekiti wangu tu wa Mkoa Kigoma. Pili, Baregu hajahudhuria kikao hata kimoja cha wazee toka ajue ukweli wa mambo.
Tatu, chama jana kimechagua rasmi Baraza la Wazee na mgombea aliyekuwa ananiunga mkono waziwazi ameshinda. Inakuwaje bado vikao vya wazee vya chama vinaendeshwa na Mtei na Ndesamburo?

Pili, vyombo vyote vya habari vilikuwapo katika hotuba ya Mtei. Imekuwaje NIPASHE peke yake ndio ione alisema kuna ufisadi kwenye chaguzi za chama? Mhariri mtendaji wa Nipashe ni jesse kwayu kutoka Machame. Mmiliki wa Nipashe ni Reginald Mengi kutoka Machame.

Spinns sio sustainable. Acheni tujenge chama chetu.


Pole sana Zitto. Nakuomba pumzika na usichangie mpaka ukitulia. Haya yote unayoyaandika huenda ungetulia usingeyaandika.

Kuna mambo yana udhi lakini ni muhimu kukaa na kutulia kabla ya kuyajibu.

Pole tena maana siasa za Tanzania sasa nafikiri zimekuwa balaa tupu.
 
Vibabu vya Chadema vitakiua chama, yaani wao ndio wamekuwa waamuzi wakuu wa mambo mbalimbali ya Chama, labda ni katiba yao lakini sidhani njia wanayoitumia ni demokrasia ya kweli kwa sababu hata Komunisti China nao wana katiba inayofuatwa huku ikiwanyima haki za msingi wananchi. Sidhani kama ilikuwa ni haki kumshauri Zitto ajiengue kutoka kwenye kugombania uenyekiti wa Chama, kwa hiyo pia kama kutakuwa na mtu mwingine akiamua kutaka kuwa mgombea wa urais kupitia Chadema nae atazuiwa ili Freeman Mbowe apitishwe bila ya kupingwa. Hii ni demokrasia ya Kifisadi isiyofaa kabisa na haina tofauti na ile ya Chama Cha Mafisadi (CCM). Kwa sababu binafsi naamini mtu anaefaa kugombea urais kutoka Chadema kutokana na kuwa na sifa zote za Rais anaeweza kuiletea madadiliko makubwa Tanzania ni Dr. Wilbroad Slaa na sio Freeman Mbowe.

Chadema mmeshaanza kulikoroga hata kabla hamjapewa nchi, hii inatia shaka sana **** mtaweza kuleta mabadiliko ya kweli ambayo CCM imeshindwa kuyaleta kwa miaka yote ambayo wako madarakani.

Nyinyi mnaomlaumu Zitto kwa uamuzi wake wa kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa Chadema inaonyesha ni jinsi gani mmelelewa na CCM kupitia siasa zake mbovu za Kijamaa. Demokrasia ya kweli inaruhusu mwanachama yeyote kugombea uongozi katika chama, Kama vibabu wa Chadema wanaogopa Freeman kushiriki kwenye chaguzi na Zitto hivi kweli atamuweza Kikwete wa Mafisadi CCM??
mkuu gombea basi urais Marekani. wee sii raia?
 
mkuu gombea basi urais Marekani. wee sii raia?
Mazee Mkandara Mimi ni Mbongo wala si raia wa Marekani, lakini nina uhakika kama ningekuwa mwanachama wa Chadema na nikataka kugombania uenyekiti wa Chama ningewekewa mizengwe kama aliyofanyiwa Zitto ili Freeman Mbowe apite bila kupingwa.
 
- Yale yale aliyoyasema Obama kule Ghana, Africans tuache tabia ya kuwekeza kwenye majina ya viongozi, tujifunze kuwekeza kwenye sound policies hii thread na yaliyojiri ni mfano mkubwa sana wa maneno ya Obama.

- Among all, Chadema sikutegemea kukutwa na haya inasikitisha sana, sawa huenda mmekubaliana na kuyamaliza, lakini swali la the big picture linapaswa kua ni under who´s expense? Somebody must pay for makubaliano yenu ya kumfanya Zitto arudishe fomu, now who is that? kama sio sisi wananchi wa Tanzania?

- I mean, hii ndio mnaita demokrasia makini? Mimi nilifkiri demokrasia makini huanzia kwenye box la kura, kumbe inaweza kupatikana na busara za wazee wa Chama? Yaani na nyinyi Chadema mnakubaliana na tabia za CCM za busara za Spika? Nimeona a lot of spinning humu mnapoteza muda bure, sana sana sasa mnawapa CCM uhuru wa kuzidi kutuchezea wananchi wa taifa hili, kama na ninyi mnafanya kwa nini wao wasifanye?

- Yaaani mnaogopa Mbowe kusimama na Zitto tu? Lakini hamuogopi Mbowe kusimama na rais wa sasa wa CCM? This is incredible, Zitto alipofukuzwa bungeni wengi tumelia kuwa ameonewa, sasa mnakuja na hizi nonsense ambazo ni clear kwamba kumbe hakuonewa kufukuzwa bunge kama ninawasoma vizuri humu na hizi spin zenu! Hamna hata aibu! Hivi mafisadi walimtuma Zitto kuchukua fomu ya Chadema, sasa waliomtuma kuwapigia kelele mafisadi kule bungeni mpaka kufukuzwa ni nani hasa? Hivi hili taifa tumemkosea nini Mungu? Sasa nani wa kumuamini tena hapa kati yenu Chadema na CCM?

- Simtetei Zitto wala Mbowe, ninaitetea demokrasia ambayo hapa imepigwa chini kwa manufaa ya watu binafsi huko Chadema na sio ya chama, no way demokrasia makini sio kumzuia mgombea mwenye akili ya kitoto na ambaye hajamkomaa kiakili, demokrasia ni absolutely opposite ya hii theory kwa sababu inataka apewe nafasi apigwe na kura za wananchi, lakini sio kumzuia kugombea, kuna ubovu mnajaribu kuuficha, sijui ni nini hasa mnachojaribu kukificha chama cha Demokrasia makini? What is it?

- Yaani kweli mnajaribu ku-pull a monkey on us wananchi na huku tunaona kwa macho yetu kwamba mnachosema sio ukweli ila ni zile zile siasa za CCM? Mnakuja hapa kumchafua Zitto na filimbi nyingi za kuwalaumu CCM, badala ya kusimama na kubeba msalaba wenu? Yes I said it huko Chadema kuna uozo kama wa CCM, ila mnajaribu kuuficha na busara za wazee lakini hamsemi nani atakayelipia kwa sababu anytime ukiuminya ukweli lazima kuwe na price to be payed, ni simple life maths.

- Mnaleta spin za ajabu hapa kumchafua Zitto, sasa kwanini msiruhusu akajimalize kwenye uchaguzi kama kweli ni mchafu kama mnavyodai? Aibuu sana hii watu tulikua tunawaamini na kuwategemea kumbe ni wale wale CCM tu, hivi mimi nimesema mara ngapi hapa kwamba the best idea ni ku'do away na viongozi wote na kufuta vyama vyote na kuanza na upya, nilisema hayo kwa sababu ya kutomuamini anybody, I mean kosa la Zitto ni nini hasa kuchukua fomu ya Mwenyekiti?

- Chadema kwa hili mmetuangusha wengi sana na mnanuka kama mafisadi ndani ya CCM tu, haya mafisadi kumbe yapo kote kote sasa dawa ni kuyajua yalioko Chadema maana ya CCM yanajulikana tayari, maana hii ni aibu ya the Century hata mki'spin vipi you are rotten kama mafisadi ya CCM tu, dawa ni kutunga katiba mpya ya kufuta vyama vyote vya siasa Tanzania na marufuku viongozi wote wa sasa kugombea uongozi tena tukianza na vyama vipya, I mean this is the worst ever!

Yaani Chadema chama cha demokrasia makini kinamzuia mwanachama wake kugombea uongozi kwa sababu ya kumuogopa kama CCM na Mrema, na kuanza kumuita majina kibao, ya kumchafua halafu eti atarudi bungeni tena kwa tiketi ya chama hicho na kuwa na heshima ile ile kutoka kwa sisi wananchi, halafu na Chadema nayo itaendelea kuwa na heshima ile ile kama zamani, yaani kweli na ninyi chadema kama CCM mnatufanya sisi wananchi wa Tanzania ni kama watoto wadogo tusio na akili!

Shame on all of you mnaohusika na hii nonsense ya busara kama za Spika! Kule CCM zile busara za Spika ziligahrimu Shillingi Millioni 100 hela zetu wananchi walipa kodi, sasa Chadema tuambieni huko kwenu hizi busara zitatumika hela ngapi na za nani?

Respect.

Field Marshall Es!
Ni wazee wanne ambao wameamua kuibana Demokrasia ya Chadema kwa maslahi yao BIBNAFSI.
 
Mazee Mkandara Mimi ni Mbongo wala si raia wa Marekani, lakini nina uhakika kama ningekuwa mwanachama wa Chadema na nikataka kugombania uenyekiti wa Chama ningewekewa mizengwe kama aliyofanyiwa Zitto ili Freeman Mbowe apite bila kupingwa.
maana yangu pia ni kwamba hata Marekani ungewekewa mizengwe hata kama ungekuwa Mmarekani..
Mimi sina noma kabisa na mkuu Zitto isipokuwa unapotaka kugombea Uenyekiti ni muhimu kujitokeza mapema .ujitangaza ukapata wajumbe wanaoku support nammuhimu zaidi kuona kama una qualify na pia uwezekano wa ushindi Upo sio kulazimisha kitu.

Zitto kalazimisha kwa sababu kuna baadhi ya watu walijifanya wao wajanja na wanakitawala chama. Zengwe lote ndani ya chadema limeundwa hivyo unachoona kinang'aa sii bahati mbaya ila Zitto mwenyewe alitegema haya kutokea.

Mkuu hata iwe Urusi, China, UK, Austarlia, Marekani, Canada au Santa Domingo. unapotaka kugombea kiti chochote cha Uongozi ni vizuri kuwataarifu wanachama kwani Chama ni sawa kabisa na Mafiaso. Kumwodoa Don inabidi uwe na watu nyuma yako na sijui kama Zitto alikuwa na nia ya kumwondoa Mbowe ila kuonyesha uzembe ulokuwepo ndani ya chama.
 
mkuu umenena ...nimeona loophole mbaya sana ambayo inaweza kutumiwa na maadui wa zitto na maadui wa chadema ...ieleweke kuwa kila chama kina siri zake......na moja ya sifa ya kiongozi ni kuhifadhi...sasa siwaelewi watu wanaomshabikia zitto kuropoka wakati wanajuwa amejipotezea sifa ya kuaminika kuhifadhi mambo mazito..ukizingatia kati ya vijana wa umri wake ni front runner to presidency....sasa unafikiri watu wa usalama faili lake leo wataongezea comment gani....hasa ukizingatia uzito wa siri viongozi wanazobeba..

hapo nyuma nimewakumbusha kuwa pamoja na mrema kutofautiana na chama cha ccm ...hadi leo hajatoa siri hata moja zaidi ya viti ambavyo kila mtu alijuwa kama chavda..etc..hasa ukizingatia nafasi yake kama mkuu wa usalama ccm,mbunge ,waziri wa mambo ya ndani na naibu waziri mkuu..

nahisi kuwa tutakuwa na tatizo la kiusalama huko mbeleni...kama idara ya usalama haitachukua jukumu la kutoa mafunzo ya maadili na uongozi kwa vijana wote wanaopata nafasi kubwa au ubunge hata wa upinzani...nimesikitika sana ...maneno ya kuropoka angetoa mtu kama hiza au aina yake nisingesikitiaka ...lakini zitto ni kijana tunayemtegemea ..kwenye hii safari...!!!..lazima awe na maadili ya uongozi ...kubalini kataeni sifa ya muhimu tunayoangalia kwa kiongozi ni kutunza siri!!!

wanaomshabikia mbona hawajiulizi kusikia siri zaidi ya tetesi kuhusu ...sokoine,kolimba.,na wengine wengi...??????.. au ccm hawana midomo???

MKUU CHADEMA MMEMCHUKUA LWAKATARE TOKA CUF NA ALIKUWA KIONGOZI KULE.AKAWEKA SIRI ZA CUF HAPA HAPA JF KWANI YEYE NI MEMBER HAPA TOKA 2008
.ALIZIWEKA SIRI ZA CUF KABLA HAMJAMCHUKUA KWENDA CHADEMA.JEE KIGEZO CHA KUVUJISHA SIRI MLIKITIZAMA?BAADA YA KUWEKA WARAKA MCHAFU DHIDI YA CUF.AKAWA ANAITUMIA JF KUTUNDIKA MAPICHA YAKE AKIWA BUKOBA WAKATI MNAMKABIDHI KADI NA HATA ALIPOPOKELEWA KWA MAANDAMANO MAKUBWA HUKO BUKOBA.

KAMA CHADEMA NI WATU WANAOJALI SIRI ZA WATU,MKUU UNGEMWAMBIA LWEKATARE AWE NA KIFUA CHA KUTUNZA SIRI,LEO NDIO UMEJUA KUWA KUNA SIRI?

mheshimiwa naomba unielimishe juu ya siri kwa viongozi.
 
Pole sana Zitto. Nakuomba pumzika na usichangie mpaka ukitulia. Haya yote unayoyaandika huenda ungetulia usingeyaandika.

Kuna mambo yana udhi lakini ni muhimu kukaa na kutulia kabla ya kuyajibu.

Pole tena maana siasa za Tanzania sasa nafikiri zimekuwa balaa tupu.

Mkuu wewe ulipoenda Kyela na jina lako lilipokuwa likitajwa sisi tulikutetea na haikutosha uikaingia Mwenyewe kujibu hoja mbali mbali.

Zitto alidhalilishwa na watu wa Mbowe kwa kuleta habari ya uongo,majungu,dharau na uzushi juu ya ushiriki wa Zitto na Mama yake kwenye uchaguzi wa vijana.maneno yale bila ya Zitto kuja kuyakanusha yangezidi kuvuruga jina lake. unataka akae kimya hadi lini. tarehe 26 mwezi huu KIBANDA kaandika makala chafu kwenye gazeti la MBOWE TANZANIA DAIMA. jumapili hii tarehe 30 akaja NGURUMO kutia msumari kupitia gazeti hilo hilo. Zitto akawa kimya tu.

leo hii wamekuja kwa kumuingiza mama yake mzazi.Zitto sio Mtume au malaika ana kiwango cha kuvumilia. wewe mbona unamchafua Mwakyembe kwanini usinyamaze? mie nilifungiwa kwa kukutetea wewe wiki nzima ulipokuja hata kunipa pole umeshindwa.

Kweli binadamu hatujioni.

Zitto jibu kadri inavyowezekana. wao wamewatumia KIBANDA,KWAYYU NA NGURUMO kukuchafua kwa wajumbe wa mkutano mkuu, sasa wameumbuka pamoja na yote hayo Kafulilla kapiga bao.
 
- Inachekesha sana kwa mtumzima kama wewe kuleta habari za Malecela, wakati Zitto anaongelea habari za jinsi alivyoshirikiana na wenziwe huko Chadema kumuuua Wangwe,

- unajaribu kutetea Zitto kuenguliwa nje ya vikao vya chama badala ya kugombea il, ashindwe kwenye uchaguzi, unasema ni jambo la kawaida huku ukiwa unajua kabisa kwamba ni tabia mbaya sana ya CCM iliyotufikisha hapa tulipo yaani taifa la Banana Republic, unajaribu kwa nguvu zote kutetea huku ukitumia mifano ya upuuzi wa CCM, and you think you are making a sense,

- Hivi ni lini umesikia rais wa US ameondolewa nje ya uchaguzi wa kidemokrasia, mmelichemsha sasa mlinywe wenyewe CCM has nothing to do with it hili kama la wangwe ni lenu wenyewe na ni aibu sana, demokrasia inadai Zitto aruhusiwe kugombea kama kushindwa akashindwe kwenye kura za wananchi sio busara za wazee wanaogawana ruzuku za chama,

- Kama kweli Chadema mnajali demokrais makini basi mpeni nafasi Zitto agombee, hili halina mjadala wala compromise, na hamtaweza ku-recover from this ugly political mistake, sasa tumeelewa kwamba hicho ni cahma cha wachache sana ambao kugombea kwa Zitto kumetishia mlo wao yale yale ya kina Karamagi, sasa mnajionyesha rangi zenu rasmi kwamba hamna cha demokrasia wala umakini, ni wababaishaji tu kama yale mafisadi ya ndani ya CCM,

Kama kweli mnajali demokrasia basi waaambieni viongozi wenu wamruhusu Zitto kugombea kama hamuwezi acheni na hizi spin za kitoto za kulinganisha Zitto na Malecela, kwa sababu ni aibu sana kwa watuwazima, JF hatujawahi kuogopa mtu wala jina au chama, licha ya baba wa mtu yoyote hapa huwa tunapiga mawe tu mmelichemsha sasa mlinywe kama ni spin Zitto atawachafua sana na hamumuwezi, si unaona so far anayoyafanya mamluki wa demokrasia, mnafikiri mnaweza kutudanganya hapa watuwazima, mmelikoroga sasa mlinywe la moto!

Kama kweli nyinyi ni demokrasia makini mruhusuni Zitto agombee, kama hamuwezi basi nyamazeni kama mafisadi wa ndani ya CCM, wao huwa hawasemi sana huwa wana vitendo tu, Chadema mmetuabisha sana na kutukatisha tamaa wananchi ulio wengi, kumbe mko sawa na CCM tu!

Respect.

FMEs!
 
- inachekesha sana kwa mtumzima kama wewe kuleta habari za malecela, wakati zitto anaongelea habari za jinsi alivyoshirikiana na wenziwe huko chadema kumuuua wangwe,

- unajaribu kutetea zitto kuenguliwa nje ya vikao vya chama badala ya kugombea il, ashindwe kwenye uchaguzi, unasema ni jambo la kawaida huku ukiwa unajua kabisa kwamba ni tabia mbaya sana ya ccm iliyotufikisha hapa tulipo yaani taifa la banana republic, unajaribu kwa nguvu zote kutetea huku ukitumia mifano ya upuuzi wa ccm, and you think you are making a sense,

- hivi ni lini umesikia rais wa us ameondolewa nje ya uchaguzi wa kidemokrasia, mmelichemsha sasa mlinywe wenyewe ccm has nothing to do with it hili kama la wangwe ni lenu wenyewe na ni aibu sana, demokrasia inadai zitto aruhusiwe kugombea kama kushindwa akashindwe kwenye kura za wananchi sio busara za wazee wanaogawana ruzuku za chama,

- kama kweli chadema mnajali demokrais makini basi mpeni nafasi zitto agombee, hili halina mjadala wala compromise, na hamtaweza ku-recover from this ugly political mistake, sasa tumeelewa kwamba hicho ni cahma cha wachache sana ambao kugombea kwa zitto kumetishia mlo wao yale yale ya kina karamagi, sasa mnajionyesha rangi zenu rasmi kwamba hamna cha demokrasia wala umakini, ni wababaishaji tu kama yale mafisadi ya ndani ya ccm,

kama kweli mnajali demokrasia basi waaambieni viongozi wenu wamruhusu zitto kugombea kama hamuwezi acheni na hizi spin za kitoto za kulinganisha zitto na malecela, kwa sababu ni aibu sana kwa watuwazima, jf hatujawahi kuogopa mtu wala jina au chama, licha ya baba wa mtu yoyote hapa huwa tunapiga mawe tu mmelichemsha sasa mlinywe kama ni spin zitto atawachafua sana na hamumuwezi, si unaona so far anayoyafanya mamluki wa demokrasia, mnafikiri mnaweza kutudanganya hapa watuwazima, mmelikoroga sasa mlinywe la moto!

Kama kweli nyinyi ni demokrasia makini mruhusuni zitto agombee, kama hamuwezi basi nyamazeni kama mafisadi wa ndani ya ccm, wao huwa hawasemi sana huwa wana vitendo tu, chadema mmetuabisha sana na kutukatisha tamaa wananchi ulio wengi, kumbe mko sawa na ccm tu!

Respect.

Fmes!
hao wazee wanne wa chadema wasiotambulika kikatiba walipostaafu kazi hawakulipwa pension zao?

wamezuia zitto kwa vile akiingia hawataweza kuchukua pesa kienyeji.unafikiri mbowe anaweza kumuhoji mzee mtei kama akitaka kuchukua milioni 50 za chama?wanatia aibu hawana tofauti na majambazi ya epa.
 
hapa nafikiri kosa kubwa kuliko la wote ni la zitto.
hawezi kutaka tu kugombea uenyekiti bila ya kutoa taarifa za awali ndani ya chama, na nna uhakika kuwa zitto analijua hilo, ila alifanya kwa kusudi labda kuonyesha kuwa chama hakiendeshwi kwa demokrasia na akashindwa kujua impact ya hicho anachokifanya.

on top of that, kaja hapa kaanika siri za chama zote nje, kuanzia ya wangwe, ya CAG sijui na makundi ya watu ndani ya chama, .....nna wasi wasi zitto ana nia ya kuvunja chama na si vyenginenevyo
 
- Inachekesha sana kwa mtumzima kama wewe kuleta habari za Malecela, wakati Zitto anaongelea habari za jinsi alivyoshirikiana na wenziwe huko Chadema kumuuua Wangwe,

- unajaribu kutetea Zitto kuenguliwa nje ya vikao vya chama badala ya kugombea il, ashindwe kwenye uchaguzi, unasema ni jambo la kawaida huku ukiwa unajua kabisa kwamba ni tabia mbaya sana ya CCM iliyotufikisha hapa tulipo yaani taifa la Banana Republic, unajaribu kwa nguvu zote kutetea huku ukitumia mifano ya upuuzi wa CCM, and you think you are making a sense,

- Hivi ni lini umesikia rais wa US ameondolewa nje ya uchaguzi wa kidemokrasia, mmelichemsha sasa mlinywe wenyewe CCM has nothing to do with it hili kama la wangwe ni lenu wenyewe na ni aibu sana, demokrasia inadai Zitto aruhusiwe kugombea kama kushindwa akashindwe kwenye kura za wananchi sio busara za wazee wanaogawana ruzuku za chama,

- Kama kweli Chadema mnajali demokrais makini basi mpeni nafasi Zitto agombee, hili halina mjadala wala compromise, na hamtaweza ku-recover from this ugly political mistake, sasa tumeelewa kwamba hicho ni cahma cha wachache sana ambao kugombea kwa Zitto kumetishia mlo wao yale yale ya kina Karamagi, sasa mnajionyesha rangi zenu rasmi kwamba hamna cha demokrasia wala umakini, ni wababaishaji tu kama yale mafisadi ya ndani ya CCM,

Kama kweli mnajali demokrasia basi waaambieni viongozi wenu wamruhusu Zitto kugombea kama hamuwezi acheni na hizi spin za kitoto za kulinganisha Zitto na Malecela, kwa sababu ni aibu sana kwa watuwazima, JF hatujawahi kuogopa mtu wala jina au chama, licha ya baba wa mtu yoyote hapa huwa tunapiga mawe tu mmelichemsha sasa mlinywe kama ni spin Zitto atawachafua sana na hamumuwezi, si unaona so far anayoyafanya mamluki wa demokrasia, mnafikiri mnaweza kutudanganya hapa watuwazima, mmelikoroga sasa mlinywe la moto!

Kama kweli nyinyi ni demokrasia makini mruhusuni Zitto agombee, kama hamuwezi basi nyamazeni kama mafisadi wa ndani ya CCM, wao huwa hawasemi sana huwa wana vitendo tu, Chadema mmetuabisha sana na kutukatisha tamaa wananchi ulio wengi, kumbe mko sawa na CCM tu!

Respect.

FMEs!

mkuu FM

kama mambo yenyewe ndio hivi basi muacheni huyu kijana Zitto,aamue la kufanya ikiwezekana kukaaambali na hicho chama hebu soma hizi habari ambazo ziko kwenye Tanzania Daima.


Chadema yachafuka,mgombea atishia kuchoma kisu, uchaguzi vijana waahirishwa
broken-heart.jpg
Na Waandishi Wetu

HALI ya kisiasa ndani ya Chadema imezidi kuchafuka baada ya uchaguzi wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha) kuahirishwa kwa miezi sita, huku mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo (jina tunalo) akitishia kumchoma kisu mwanachama anayeaminika kuwa kambi ya naibu katibu mkuu, Zitto Kabwe.

Wakati hatma ya uchaguzi huo ikiwa bado njia panda, mizengwe imezidi kutikisa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake baada ya mmoja wa wagombea anayeaminika kuwa upande wa Zitto kunusuruka kung'olewa.

Joto zaidi linaloonyesha hali tete ndani ya Chadema, lilipandishwa na hatua iliyotangazwa jana mchana na katibu mkuu, Dk Wilbrod Slaa ya kuahirisha uchaguzi huo hatua ambayo ilipingwa na Zitto na msemaji wa chama hicho David Kafulila ambao wanataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika juzi na kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC), ambacho inasemekana kinafanyika leo.

Wagombea waliokuwa wakiwania nafasi ya uenyekiti wa Bavicha ni John Heche, Dadi Igogo na David Kafulila ambaye licha ya kuwa ofisa habari wa chama hicho, anatarajiwa kuwania ubunge Jimbo la Kigoma Kusini mwaka 2010.

Akitangaza kuahirishwa kwa uchaguzi huo jana, Dk Willibrod Slaa alisema uchaguzi huo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo.

“Mimi kama katibu nimeshauriana na kamati ya wazee ya chama nikiongozwa na Mzee (Edwin) Mtei, Bob Makani na Balozi (Christopher) Ngaiza tumeubatilisha uchaguzi huo, hivyo utafanyika ndani ya miezi sita ijayo,” alisema Slaa.

“Tumeamua hivi kwa sababu kwanza kufanya uchaguzi ni gharama, tunatumia karibia Sh50 milioni ambazo zinaweza kujenga zahanati moja. Jamani hapa tutawaeleza nini Watanzania.

“Wajumbe walidai kuwa uchaguzi ulijaa rushwa, lakini niliwambia waandike malalamiko kwa maandishi na ujumbe mfupi na wamenipatia nitayafanyia kazi na yatatolewa maamuzi na vyombo husika.”

Lakini Zitto alipinga uamuzi huo akisema katibu mkuu hana mamlaka ya kutoa tangazo hilo na kwamba nanlaka hayo ni Kamati Kuu (CC).

"Lakini pia, chombo pekee chenye uwezo wa kufanya uamuzi huo ni Kamati Kuu, sasa inakuaje chombo kingine kichukue uamuzi tena bila matokeo kutangazwa wala mgombea kukata rufaa," alisema Zitto.

Alifafanua kuwa uamuzi huo umetokana na baadhi ya watu kukataa matokeo hayo baada ya kuweka mbele maslahi binafsi badala ya maslahi ya chama kwa kuwa jambo la msingi katika suala hilo ni matokeo hayo kutangazwa kwanza kabla ya kuahirisha uchaguzi.

"Jambo la kwanza ni kutangaza matokeo na baadaye kama kuna mgombea alikuwa akipinga, anaweza kukata rufaa, lakini matokeo hayajatangazwa wala hakuna aliyekata rufaa," alifafanua Zitto.

Kutokana na utashi wa katiba, Zitto alisema tayari amemwomba katibu mkuu kuitisha mkutano wa CC kujadili suala hilo.

"Nimemwomba Dk Slaa aitishe kikao cha Kamati Kuu tujadili hii hali maana kama viongozi hatutakuwa na busara na chama kitavurugika," alionya.

Alipoulizwa nini mustakabali wa Chadema kutokana na matukio hayo ya vurugu yanayotikisa chama, alijibu: "Viongozi tusipotumia busara chama kitavurugika, lakini tukitumia busara na kuweka maslahi ya chama mbele, tutaweza kutatua haya mambo kwa urahisi."

Zitto alihoji: "Kwanini wazee wasitumie busara kama walizotumia kuniomba mimi nijitoe kwa kutaka wagombea wengine wajitoe au wakubali matokeo kwa kumwachia Kafulila?
"Tukiwa na busara; tukiheshimu demokrasia, tutaweza kuvuka salama. Naamini hilo tu ndiyo suluhisho la kukivusha chama salama."

Naye Kafulila alipinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi kabla ya kutangaza matokeo akisema anataka kutangazwa kwanza kwa matokeo ambayo anaamini, yalimpa ushindi.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kafulila alisema haoni sababu ya kutotangazwa kwa matokeo hayo ambayo anaamini alishinda licha ya kutokubalika na sehemu kubwa ya wajumbe wa sekretarieti na wabunge wa viti maalum.

"Ukiangalia hata hayo mambo ya karatasi kuongezeka, utaona labda ulikuwa ni mpango maalumu wa kumwangusha mtu fulani, lakini imeshindikana," aliongeza.
"Kwa kifupi, sikubaliani na uamuzi huo ninachotaka kwanza matokeo yatangazwe na pia baraza halina mamlaka hayo. Hiyo ni kazi ya Kamati Kuu."

Habari zinadai kuwa tangu John Mnyika kuondoka kwenye wadhifa wa uenyekiti wa vijana wa Chadema, kumekuwa na mkakati wa kumdhibiti Kafulila unaofanywa na baadhi ya vigogo wa Chadema kutokana na mgombea huyo kuonekana mwiba kwao.

Kafulila anasemekana kuwa ni mtu anayepinga waziwazi mambo yanayoendeshwa kinyume na taratibu na amekuwa hahofii viongozi wa juu yake kueleza msimamo wake.

Wakati hayo yakiendelea, vurugu zaidi zimezidi kutikisa chama hicho na jana zilifikia katika hatua ya mgombea mmoja wa nafasi ya uenyekiti wa vijana kutaka kumchoma kisu mwanachama ambaye alikuwa akimtetea Zitto Kabwe asitukanwe na mgombea huyo.

Kabla ya kufikia hatua ya kutishiana visu, mgombea huyo alikuwa akibishana na baadhi ya wafuasi wa Kafulila kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema zilizo Kinondoni jijini Dar es salaam.

Wakati Mwananchi inafika kwenye ofisi hizo majira ya saa 7:00, vurugu zilikuwa zimeshapoa tangu saa 5:00, lakini wanachama walikuwa wamekaa kwenye vikundi wakijadili matukio mbalimbali ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mgombea huyo na mwanachama mmoja anayedaiwa kuwa anamuunga mkono Kafulila, walirushiana ngumi kwanza na baadaye ndipo mgombea huyo alipotoa kisu na kumtishia.

Mashuhuda hao walidai kwamba mara baada ya mgombea huyo kutoa kisu, wanachama wengine waliokuwa karibu waliingilia kati na kumtoa eneo hilo.

Mwanachama anayedaiwa kutishiwa kisu aliiambia Mwananchi kuwa alikuwa akimsihi mgombea huyo kuacha kumsema vibaya Zitto kwa kuwa malalamiko yote ya uchaguzi wa juzi yako ngazi za juu za chama hicho.

Mwanachama huyo alifafanua kwamba baada ya kumwambia mgombea huyo maneno hayo, alipandisha ghadhabu zaidi na kuanza kutukana.

“Sasa mimi nilivyoona anamtukana Zitto, nilimwambia aache lakini hakusikia; alikuwa anasema Zitto wako na Kafulila walishirikiana kumwibia kura. Kutokana na kuendelea kuongea ovyo, tulishikana na alivyoona muziki ni mnene alinitolea kisu na kutaka kunichoma,” alidai.

Katika hatua nyingine, Dk Slaa juzi alilazimika kurudi katika ukumbi wa uchaguzi wa Bavicha mnamo saa 6:20 usiku ili kutuliza ghasia zilizoibuliwa na wajumbe mara baada ya kupata habari kuwa kura 20 ziliongezeka katika nafasi ya mwenyekiti.

Wajumbe hao ambao walionekana kuwa upande wa mgombea wa nafasi hiyo, John Heche ambaye ni diwani wa Tarime Mjini, walipinga matokeo kabla hayajatangazwa hali iliyomlazimu msimamizi wa uchaguzi huo, Charles Mwera, ambaye pia ni mbunge wa Tarime, kutoyatangaza.

Dk Slaa, ambaye aliondoka kwenye ukumbi huo juzi saa 7:00 mchana, alirejea kwa mara ya pili saa 6:20 usiku, vurugu zikiendelea baada ya Heche kumpiga ngumi mbili ofisa wa kurugenzi ya uchaguzi ya Chadema, Ali Chitandana na kumlazimu kufanya kazi kubwa kuzituliza.

“Jamani wajumbe nawaomba muwe watulivu kila kitu kilichotokea nimepewa taarifa na Mnyika, kwa hiyo kama kuna mtu ana malalamiko ayaandike na kuyawasilisha makao makuu ya chama kesho (jana) asubuhi ili niyafanyie kazi,” alisema Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, wajumbe hao walimweleza wazi Dk Slaa kuwa hawajalipwa fedha zao za posho hali iliyomlazimu katibu huyo mkuu kumwagiza Mtunza Fedha kuwalipa wajumbe hao kutoka mikoa mbalimbali nchini usiku huohuo.

“Wewe Mtunza Fedha walipe wajumbe posho zao; jamani nimeshamwagiza atawalipa wote ila wale ambao wameshakata tiketi kwa ajili ya kusafiri watarudishiwa fedha zao kesho (jana) kwa sababu hamuwezi kuondoka kwa kuwa uchaguzi huu unaweza kurudiwa, lakini yote yatajulikana mara baada ya viongozi kukutana,” alisema Dk Slaa.

“Kwa kweli, nimesikitika sana hiki kitendo kilichotokea leo ni aibu kwa chama. Hapa wapinzani na magazeti yatapata pa kusemea.

Hiki chama ni cha demokrasia; nahitaji kujua kila kitu kilichotokea ili vifanyiwe maamuzi na yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja au nyingine atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa katiba ya chama.” Habari hii imeandikwa na Ramadhan Semtawa, Fidelis Butahe, Musa Mkama na Fred Azzah
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom