LGE2024 Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na sarakasi zinazoendelea

LGE2024 Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na sarakasi zinazoendelea

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

MwajabuOmary

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
384
Reaction score
418
Nimekua nikifuatilia taarifa mbalimbali za uchaguzi wa Serikali za mitaa tangu uandikishwaji wa wapiga kura hadi kufikia sasa wakati wa wagombea kuteuliwa.

1. Wakati wa uandikishaji yalikuwepo malalamiko kutoka vyama vya upinzani kwamba kuna wanafunzi wa shule za secondary na msingi wameandikishwa kupiga kura katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa. Kama nakumbuka vizuri baadhi ya wachungaji walilikemea hilo kwamba Taifa tunalolijenga ni taifa la hatari sana. Aidha katika sakata hilo pia yalikutwa majina ya watu waliofariki. Jambo hili kama ni kweli basi sio la kiungwana. Kwa mantiki hiyo basi zoezi la uandikishaji halikua la haki kwa sababu lilikua limejaa janjajanja nyingi.

2. Tumekuja wakati wa kujaza fomu, kuzirejesha na kufanyika kwa uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo. yaliyojitokeza ni vichekesho; wapo baadhi ya watendaji bila hata kuwa na sababu walikataa kupokea fomu za wagombea. Wagombea wameenguliwa kwa sababu za ajabu kabisa.

Tafakari yangu katika maeneo mawili niliyoyataja hapo juu; Je Tanzania kuna shule za aina mbili tofauti za watu wa CCM na zile za wapinzani hali inayopelekea watu wa ccm wawe na akili zaidi kuliko wanaosoma shule za wapinzani? Jibu ni hapana watanzania wote wanasoma shule za aina moja. Na hili liko wazi na ndio maana wapinzani wengi wanaorubuniwa kujiunga na ccm wanapewa nafasi katika serikali.

Je kuna wana ccm ambao wameenguliwa au ni kwa wapinzani tu?

Zipo kauli za kuwapoteza wapinzani zinazopelekea wapinzani kukiona cha mtema kuni kama zifuatazo
1. Maridhiano
2. Ndani ya miaka mitatu mama kafanya maajabu,
3. CCM haihitaji kubebwa
Kauli hizo kwangu sioni kama zina mashiko kwa sababu haziendani na uhalisia.
tangu sarakasi hizi zimeanza sijasikia kauli yoyote kutoka Tume Huru ya Uchaguzi kama inavyoitwa. Aidha TAMISEMI wizara ambayo ndio msimamizi Mkuu wa uchaguzi huu na ambayo ipo chini ya ofisi ya Rais hawajatoa kauli yoyote juu ya malalamiko ya wapinzani.

Na kama hali itabakia kuwa hivyo basi sioni kama kulikua na sababu ya kumuondoa Nape na yule DC. Tetesi zilizopo ni kwamba baadhi ya watendaji waliotenda haki tayali wameondolewa katika nafasi zao na walioonyesha ukatili wa kukiuka taratibu upo uwezekano wa kupandishwa vyeo na huo ndio utamaduni wetu.

NINI KIFANYIKE
Wahusika (TAMISEMI) wajitokeze hadharani kukemea maovu hayo na kuamuru wagombea wote walioenguliwa warudishwe katika nafasi zao za kugombea. Kama ukimya utaendelea kutamalaki wapinzani msubiri maumivu kwani sarakasi za mwisho wakati wa uchaguzi ndio mtajua hamjui.
 
Back
Top Bottom