Stiv
Member
- Jul 17, 2021
- 6
- 3
PAMOJA TUNASHINDA
Kumekuwa na mapambano na vita dhidi ya umasikini, nchi imekua ikibadilisha sera na kauli mbiu kila utawala mpya ukiingia, Licha ya jitihada zote hizo takwimu zinaonyesha ya kuwa kuna maendeleo ya serikali ki takwimu na watu wake wakisalia katika mkwamo ule ule wa umasikini (Wealth, 2019), Kwa haraka haraka ukiangalia katika majiji mbalimbali nchini Tanzania utagundua kua asilimia kubwa majumba na vitega uchumi vikubwa humilikiwa na serikali au taasisi. Licha ya kuwa Kila aliye na nguvu hujishughulisha kupata kipato na si kwamba wakazi walio katika familia zilizo katika mkwamo wa kiuchumi hawajishughulishi, la hasha, hujishughulisha tena kwa nguvu nyingi
Tangu kale na kale kwa kuwepo duniani familia imekua ni taasisi yenye mchango mkubwa kwa mabadiliko ya mwanaadamu na jamii. Katika Afrika Familia imekua kiungo muhimu sana katika ku endeleza maadili, tamaduni, miiko, pia msaada mkubwa katika matatizo, misiba, magonjwa, na sherehe mbalimbali kama vile harusi na nyinginezo, ilikuhakikisha mafanikio katika kuhakikisha muendelezo ya mila, tamaduni na mshikamano huo kila mtu katika familia (baba mama mtoto ) kijamii amepewa wajibu (Social responsibility) kuutekeleza katika familia yake. Licha ya uwepo wa mshikamano katika mambo mbalimbali, familia nyingi zilizo katika mkwamo wa kiuchumi zimekosa muungano au mshikamano katika swala la uchumi, pia majukumu ya watu wa familia katika uchumi yana mapungufu.
Mfano mzazi huangaika kuhakikisha chakula, elimu, afya, mavazi, makazi bora kwa wanawe. Na mtoto husoma na kuwajibika kwa wazazi. Mtoto akifika umri wa kujitegemea au akimaliza elimu na kujiajiri au kuajiriwa, hurudi katika mzunguko ule ule wa kuhudumia familia ipate mahitaji muhimu.
Ili kupambana na umaskini katika kaya hizi, zinaitaji kuwepo kwa ushirikiano katika swala la kiuchumi kama ilivyo katika Nyanja zingine za kijamii. Ushirikiano huo ningependa kuufananisha na mfumo wa jua
Picha na Mtandao
Sifa ya mfumo wa jua ni; Jua ambalo ni nyota ni kitovu , sayari huzunguka jua, kila sayari hujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake na kila kitu kilichopo katika mfumo wa jua huwa na sifa zake za kipekee, humaanisha ya kuwa kuna kanuni (nguvu inayozishikilia sayari hizo), hizi sayari haziingiliani katika mizunguko yake.
Na hizi ndio sifa ambazo biashara kifamilia itatakiwa kuwa , sifa izo ni kama ifuatavyo moja jua maana yake ni kuwepo kwa biashara moja ambayo itasimamiwa na kukua kutoka kizazi kimoja hadi kiingine , sayari humaanisha familia mbalimbali katika ukoo au ni washiriki katika familia hujizungusha katika biashara kuu ya kimkakati katika ukoo, familia hizi au watu katika familia wako huru kujihusisha na namna nyingine ya kipato bali pia huzunguka (huwajibika) katika biashara kuu ya kifamilia au kiukoo, Ili kuepusha migongano na kuendesha biashara kwa kuegamia upande au kiholela ni muhimu sana kuwepo kwa kanuni zitakazo simamia misingi ya uendeshaji biashara , sheria hizi zinapaswa kuwa madhubuti kuepusha mianya ya kuleta migongano na chuki ndani ya familia na pia zinatakiwa kushikwa mkono na mhimili wa serikali( mahakama).
Mfumo wa biashara za kifamilia si mpya duniani, Bali Tanzania na nchi nyingi za kusini mwa jangwa la sahara uwepo wake ni katika asilimia ndogo sana . moja ya chapisho imeonyesha ya kua,Biashara zinazoendeshwa na familia katika nchi za uarabuni za mashariki ya kati, ni asilimia tisini (90%) ya makampuni, pia yameajiri asilimia themanini (80%) ya nguvu kazi, na huchangia asilimia sitini (60%) ya pato la taifa (GDP) (Samara, 2020).
Katika utafiti wa Frolen 1998 ilikadiriwa ya kuwa asilimia 65 hadi 80 ya makampuni duniani yanamilikiwa na familia. Na pia utafiti wa mwaka 2005 wa Miller & Le Breton-Miller, 2005 ulionyesha ya kuwa biashara za kifamila zilikua kiungo muhimu kwa nchi nyingi duniani (Chahal and Sharma, 2020). Nchini marekani utafiti wa mwaka 2003 ulionyesha ya kua biashara za kifamilia ni za kuchukuliwa katika umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo ambapo zilichangia asilimia sitini ya nguvu kazi yote na kuchangia asilimia sitini nane 64% ya pato la taifa na kuzalisha kazi mpya kwa asilimia sabini na nne 74% (Astrachan and Shanker, 2003)
Kama tulivyoona takwimu kutoka nchi zilizo endelea juu ya biashara za kifamilia tunaweza jifunza kutoka kwao na kuja na mipango madhubuti katika kuinua uchumi wa watu, familia na jamii kwa ujumla. Katika mjumuisho wa machapisho ya tafiti mbalimbali India (Chahal and Sharma, 2020) , ilionyesha changamoto zifuatazo na suluhisho.
Mara kadhaa familia huhusisha malengo ya kijamii na kihisia (socialemotional goal), bila kuzingatia faida au hasara katika biashara yao. Hii hutokea ili kujilinda dhidi ya mahusiano ya kifamilia na jamii nyingine. Hii huleta utofauti katika namna ya kuwekeza ukifananisha na makampuni yasiyo ya kifamila. Hivyo inashauriwa kutofautisha kati ya malengo ya kijamii na kihisia dhidi ya malengo ya kiuchumi ya biashara.
Biashara za kifamilia zimekua zikitumia njia zilezile za utendaji kazi bila ya kugundua njia na teknolojia imara Zaidi ya utendaji wa biashara, sababu kubwa ikiwa hofu ya uwekezaji, Licha ya ukweli kua ili kuongeza ubora na kipato Zaidi unahitaji teknolojia yenye ufanisi mkubwa. Suluhisho ni familia kujua ya kua inahitajika mabadiliko ya kiutendaji na kiteknolojia ili kuendana na wakati pia kuimararisha na kukuza biashara.
Ukosefu wa watu walio na ujuzi mahususi katika biashara, hii hutokana na familia kulazimisha kuweka watu wa familia/koo, biashara kubwa huitaji watu wenye ujuzi mabalimbali (professionals), ili kuimarisha biashara. Suluhisho familia inatakiwa kuwekeza katika mifumo imara ambayo itasaidia kuto kulazimika kuweka wanafamilia hata wale wasio na ujuzi na kuwaacha watu ambao wengekuwa na msaada Zaidi katika biashara hiyo.
Kuto kujali wasio wa familia kama inavojali wa familia, watu huogopa unyanyasaji katika biashara nyingine kutokana na utofauti wa huduma kwa watendaji wake, suluhisho ni muhimu kurasimisha biashara ya kifamilia na kujali mahitaji na haki ya kila mfanyakazi kulingana na sera na kanuni za biashara husika bila upendeleo.
Kukosekana kwa mpango wa kuendeleza biashara kwenda kizazi kingine, hii ni shida kubwa na chanzo kikubwa cha kudorola kwa biashara na mapigano ndani ya familia. Suluhisho ni kuandaliwa kwa katiba yenye kueleza kila hitaji na kanuni katika maswala yote ya uendeshaji wa biashara, katiba hiyo ni ile iliyopitishwa na vyombo vya kiserikali na kukubaliwa na wanafamilia/koo. pia kuwa na mikakati maalumu ya kuwaandaa warithi.
Kutokea kwa migogoro katika familia, shauri ya kutofautiana kimawazo hivyo kuchelewesha maamuzi, juu ya nani achukue nafasi ya uongozi katika biashara, nani aandaliwe katika kuisimamia biashara mgawanyo wa mapato, kuwahusisha wake au mume wa mwanafamilia, fikra ya kuwa familia fulani ndio imeshikilia biashara na fikra zingine na sababu nyingine nyingi zinazo weza kuleta mtafaruku kati ya wanafamilia. Ili kuzuia hilo ni muhimu kuwepo kwa uwazi, uwajibikaji na mawasiliano ya namna biashara inavyoenda, uwepo wa mikutano ya mara kwa mara ambayo inajadili biashara ya familia/koo na mgawanyo wa kazi, jukumu la mgawanyo wowote baina ya wanafamilia linapaswa kuwa la mkutano sio la familia Fulani au mtu Fulani.
Kuhitimisha , biashara za kifamilia zinanafasi kubwa ya kukua na kutoa familia za uchumi mdogo kimasomaso. Licha ya changamoto za kibiashara na kiuchumi uwepo wa tabia ya kiujasiriamali, uthubutu, umoja na uwekezaji katika familia ni ufunguo wa kufikia malengo ya kutokomeza janga la umaskini wa watu nchini Tanzania .
MWISHO,
REJEA
- Astrachan, J. H. and Shanker, M. C. (2003) ‘Family Businesses ’ Contribution to the U . S . Economy : A Closer Look’, XVI(3).
Chahal, H. and Sharma, A. K. (2020) ‘Family Business in India : Performance , Challenges’, 1, pp. 9–30. doi: 10.1177/2632962X20960824.
- Samara, G. (2020) ‘Journal of Family Business Strategy Family businesses in the Arab Middle East : What do we know and where should we go ?’, Journal of Family Business Strategy, (xxxx), p. 100359. doi: 10.1016/j.jfbs.2020.100359.
Wealth, T. R. (no date) ‘Human Capital : The Real Wealth of Nations’.

Upvote
2