Mwafrika hawezi kukomboka. Kama angekuwa anaweza angekuwa keshakomboka zamani za kale. Au wewe mfuasi wa Ujamaa unadhani ni lini Mwafrika atakomboka?
Saa ya Ukombozi ni Sasa - Usiniulize Nani Mwanzilishi wa 'Falsafa' Hii ya Kukomboka!
Unaanza kutoka nje ya mada sasa. Sijui ni maboksi au nini....
'Nyani' - rejea matumizi ya ' ' katika neno ujijibu swali lako la kukomboka nako kuwa 'falsafa'!
Mkanda - rejea historia ya Waafrika/Weusi toka enzi za Axum na Kemet utueleze lini tulianza 'kuwa tulivyo'!
Zaku - rejea kazi yako ya maboksi kwenye hayo mazingira ya hizo 'dali' za kuyabebea utueleweshe 'nadharia' yako ya 'motisha'!
Tukubalini kwanza ndivyo tulivyo, hiyo itakuwa moja ya hatua kubwa mno na ya msingi ktk ujenzi wa uchumi endelevu.
Huwezi kuwa 'ndivyo ulivyo' ukategemea kujiletea maendeleo maana maendeleo ni kubadili jinsi ulivyo sasa utajibadilije na ilhali hivyo ndivyo ulivyo? 'Muanzilishi' wa falsafa hiyo humu JF anaitumia hiyo lojiki kuonesha kuwa hakuna haja ya kuhangaika kuleta uchumi endelevu n.k. maana kuwa uchumi duni ndio jinsi tulivyo. Kwa lugha nyingine, maadam hivi ndivyo tulivyo basi angalau tuwaite wengine ambao sivyo walivyo ili watusaidie kutuletea maendeleo ikibidi kwa viboko kama alivyofanya Jerumani!
Tena waumini wa 'falsafa' hii ya kinasaba wananukuu mpaka Biblia inayosema Je Muithiopia anaweza kujibadili ngozi yake au chui kubadili madoa yake. Hivyo wanataka tupate masihi wa kuweza kuja kutuokoa na huo 'ufungwa' wa hulka, tabia na utamaduni wetu ambao 'ndivyo ulivyo'!
It is an essentialist's fatalistic argument - it only lead one to a cul-de-sac, that is, a dead end!
But the 'founder' of 'Classical Ujamaa' reminds us that "the choice is not between change or no change; the choice for Africa is between changing or being changed - changing our lives under our own direction, or being changed by the impact of forces outside our control"!
Mkuu
Ndivyo tulivyo, naomba nitoe mifano lakini uichukulie mifano huru na wala usikwazike kwa hiyo mifano.
Mtu alivyo mara zote hawezi kukubali kama yeye ni ndivyo alivyo na kutokubali kwake kuwa ndivyo alivyo kutamchukuwa miaka mingi sana ama karne na karne ama kusitokee kabisa maana anaamini yupo ktk mstari sahihi.
Binadamu anayetambuwa udhaifu na kuukubali udhaifu wake mara nyingi huwa mtu mwenye mafanikio ktk nyenendo zake.
Mwanafunzi mjinga huwa hajitambui kuwa ndivyo alivyo na kinachomsituwa ni MTIHANI baada ya kufeli mara kadhaa,na mwanafunzi anayetambuwa kuwa ndivyo alivyo huwafuata wkongwe na walimu wake ili wampatie njia mbadala na aweze kufaulu.Lakini yule ambaye ndivyo alivyo anapoamuwa kuyakataa matokeo na kutoa visingizio kibao mara kaonewa mara madarasa machache ,mara mwalimu anamwonea huyu huwa hajatambuwa kuwa ndivyo alivyo na mwisho wake ni mbaya zaidi.
Waafrika tumefeili mitihani miaka mingi sasa toka uhuru hadi leo tatizo ni ndivyo tulivyo tulikubali tatizo na tujaribu kulitatua kuendelea kujiaminisha sivyo tulivyo kunatupeleka shimoni,SASA nimeanza kuamini kwa kiasi fulani wasingelikuja wakoloni tungekuwa nyuma sana wenda bado tungekuwa tunakula mizizi.
Bravo bravismo my broda
Huwezi kuwa 'ndivyo ulivyo' ukategemea kujiletea maendeleo maana maendeleo ni kubadili jinsi ulivyo sasa utajibadilije na ilhali hivyo ndivyo ulivyo? 'Muanzilishi' wa falsafa hiyo humu JF anaitumia hiyo lojiki kuonesha kuwa hakuna haja ya kuhangaika kuleta uchumi endelevu n.k. maana kuwa uchumi duni ndio jinsi tulivyo.
Broda NN, swali lifuatalo katika variation mbalimbali tumeshaulizana mara kibao:
Unaijibu vipi hii hoja iliyoulizwa na Companero hapo juu?
'Nyani' - rejea matumizi ya ' ' katika neno ujijibu swali lako la kukomboka nako kuwa 'falsafa'!
Mkanda - rejea historia ya Waafrika/Weusi toka enzi za Axum na Kemet utueleze lini tulianza 'kuwa tulivyo'!
Zaku - rejea kazi yako ya maboksi kwenye hayo mazingira ya hizo 'dali' za kuyabebea utueleweshe 'nadharia' yako ya 'motisha'!
Ubunifu kama NN anavyosema.
Hizo sababu nyingine mimi naziona ni longolongo tu. Ubunifu ndio kiini cha maendeleo. Huu ubunifu una extend hadi kwenye sera, mipango, na zana za kuleta maendeleo. Watu kama hamko wabunifu, maendeleo mtayaona au kuyasikia kwa walio wabunifu tu. Haiwezekani kukwepa ubunifu katika maendeleo.
Yanaendana na ukweli kuwa binadamu wote wametokana na kizazi kimoja.
Hii ni nadharia tu ambayo haina uthibitisho wa kutosha kama ilivyo nadharia ya evolution.
Quote:
Hivyo basi level ya ubunifu kwa vizazi vya mwanzo vya binadamu ilikuwa sawa.
Si kweli kwa sababu hata watoto wawili wenye wazazi sawa wanaweza kuwa na uwezo tofauti katika mambo tofauti.
Quote:
Na kama ilikuwa sawa basi wangeweza kusambaa na kuongezeka dunia proportionally kwa sababu walikuwa wana ubunifu wa kukabiliana na mazingira yao.
Kwa sababu haikuwa sawa ndio maana hayo hayakutokea
Quote:
Lakini kwa sababu hawakusambaa na kuongezeka proportionally, basi inawezekana maendeleo yao yalikuwa yanaathirika na mazingira yao au maendeleo yao yalitegemea nani kabalikiwa au kalaaniwa na Mungu.
Hapo kwenye nyekundu ndio kiini hasa cha umasikini wetu mtake msitake, mkubali msikubali
Kwikwikwi, unajua pride wakati mwingine inanifanya niwe mgumu ku-reconcile with facts.
Kuna posti nilikuwa namjibu Mkandara, nimehamua kutoi-post tu kwa sababu ina-contradict na nadharia yangu ya mazingira na incentives.
..Leo hii mtu akiitwa mjinga au maskini wanasema ni tusi wakati lengo kubwa la Kitaifa ni kufuta Umaskini na Ujinga..Huoni kaa hapa tunajifunga wenyewe.. utachukia vipi kuitwa maskini na mjinga wakati unatambuwa kwamba ni mapungufu makubwa kitaifa tunayotakiwa kuyafanyia kazi!....