
Yanaendana na ukweli kuwa binadamu wote wametokana na kizazi kimoja.
Hii ni nadharia tu ambayo haina uthibitisho wa kutosha kama ilivyo nadharia ya evolution.
Hivyo basi level ya ubunifu kwa vizazi vya mwanzo vya binadamu ilikuwa sawa.
Si kweli kwa sababu hata watoto wawili wenye wazazi sawa wanaweza kuwa na uwezo tofauti katika mambo tofauti.
Na kama ilikuwa sawa basi wangeweza kusambaa na kuongezeka dunia proportionally kwa sababu walikuwa wana ubunifu wa kukabiliana na mazingira yao.
Kwa sababu haikuwa sawa ndio maana hayo hayakutokea
Lakini kwa sababu hawakusambaa na kuongezeka proportionally, basi inawezekana maendeleo yao yalikuwa yanaathirika na mazingira yao au maendeleo yao yalitegemea nani kabalikiwa au kalaaniwa na Mungu.
Hapo kwenye nyekundu ndio kiini hasa cha umasikini wetu mtake msitake, mkubali msikubali