Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Point hapa inaleta tija gani kwa kufanya hivyo au ni hisia tu hasira na chuki?
Kwani historia inasomwa kwa manufaa gani? Ukijua umuhimu wa historia nadhani utakuwa umeshapata jibu la swali lako.
 
Watu wanakosomea kitabu chake alichokiandika kwa hiari na utashi wake huru kabisa! Kinachowakera watetezi wa Magufuli ni kutokana na kitabu hicho kujaa Madudu na maovu mengi ya kutisha ambayo msingependa yawekwe hadharani na kama hivyo ndiyo basi nanyi masukumagang mlikosea sana kumruhusu kuliandika kitabu hicho cha maovu yaliyomshangaza mpaka Lucifer mwenyewe!
Hatumsemi kwa mabaya bali tunakariri mabaya yake kwa sauti hadharani ili yasije yakajirudia tena!
Magufuli tutaendelea kumpiga kwelikweli ili liwe fundisho kwa viongozi wajao kuheshimu sheria na haki za rais wanawaongoza!

Sent from my Nokia G21 using JamiiForums mobile app
 
Wapo wabaya Waliohai,
Wapo Wema Waliohai.
Hao ndio waku-deal nao kuliko ku-deal na Wafu
Yeye mwenyewe si alikuwa anasema tutamkumbuka? Sasa tukimkumbuka dikteta uchwara Kuna shida gani?
Usitupangie Cha kumkumbuka sisi tunatoa sifa zake dikteta lilikuwa jitu katili sana kuwahi kutokea. Na ashukuriwe MUNGU kwa kulifyekelea mbali.
 

Duh !!!
 
Anatajwa na Wajerumani? Au kina Nani?
Kutaja taja Wafu kila mara ni dalili ya kuchanganyikiwa.
Unataja Watu ambao hawana chochote chakufanya

Katika vita siku zote usimchagulie mtu silaha, kama unavyofanya acha watu watiririke yaliyo mioyoni mwao. Mbona yeeh hayati aliwahi kusema watu wasimpangie nini cha kufanya yaani ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga. Acha watu watiririke hapa ndo jukwaa lao la kuongea kwa uhuru
 
Mkuu ukiwa hai utasifiwa ukifa utasifiwa zaidi na sikukadhaa baada ya mazishi yako hasa msiba ukiisha

Hapo tutaanza kuya skia Yale uliyo yafanya Siri

Mganga wako ata jurikana,mchepuko,mtoto wa nje ya ndoa,nazile tabia za kumhesabia shemeji vipande vya nyama ndani Zita vuma

Nikawaida na ndivyo ilivyo
Lita kuja litokee tukio lingine litakalo trend mpaka jpm itakuwa zilipendwa

Niwakati na haizuiliki mkuu
 
Wanafikiri kwa kufanya hivyo kutafuta ujinga na upuuzi unaofanywa Sasa.
 

Hata wao ni watanzania. Kila mtu ana haki ya kumkumbuka kwa namna alivyoguswa, tusipangiane.
 
Kwa akili yako na uwezo wako wa kufikiri; ukifanya comparison analysis kwanini ikiwa Kuna awamu zilizopita na zilifanya maovu kwanini hayati alaumiwe Sana kuliko watangulizi wake!

Ukweli Ni kwamba alifika the highest degree of impunity Katika Mila na desturi za maisha ya watanzania. He was everything.

Umeandika vyema kwamba so vyema watu kumwit shetani yule. Hata Mimi siungi mkono kumuita binadamu shetani. Lakini unakumbuka kauli yake mwenyewe kwa kinywa chake mwenyewe kwamba anatamani matajiri waishi Kama mashetani? Na kweli matajiri wakaanza kukiona Cha maoto ikiwemo utitiri wa kesi zilizoitwa za uhujumu uchumi? Hakuwahi hata siku moja kujitenga na matendo maovu yakiyokua yakitendeka isipokua alitoa zawadi ya vyeo na madaraka kwa waliyofanya matendo hayo maovu.

Unakumbuka as watendaji waliokufa chini yake walipomfananisha na Mungu na Wala hakuwahi kukataa isipokua alisema anatamani kuwa siku Moja akifa aende mbinguni kuongoza malaika hata sio wateule wa Mungu? Huoni Kama hiyo Ni kufuru?

Kuna mkuu mmoja wa mkoa alisema bila aibu mbele za umma kwamba Mungu amshukuru Magufuli kwa kuiondoa corona! Magufuli hakuwahi kutoka hadharani kukataa Hilo Wala kuonesha kutokufananishwa na Mungu! Maandiko yanatuambia Mungu alimwadhibu Lucifer kwa sababu alitaka kusujudiwa Kama Mungu(Mungu Ana wivu na Hilo amelionesha katika maandiko)

Tumeshakataa kabisa kumhusisha Magufuli na kushambuliwa kwa TAL. Lakini kiuhalisia Rais ndio Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama. TAL aliposhambuliwa wanachama wake waliojitokeza kumuombea walikutana na mkono wa polisi mpaka makanisani. Hakuwahi kujitenga na matendo hayo. Ama hata tu kwa kuongea hadharani. (Alifurahia)

Akiweka Jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kimara kibaha aliviambia vyombo vya habari "you are free but not to that extent" akalenga specifically Mwananchi Newspaper muda mfupi tu Azory Gwanda akapotea na maelezo ya mke wake Ni watu wa serikali! Utawala wake ulikaa kimya kimya na hakuwahi kujitenga na matendo hayo. Mpaka waziri bwana Kabudi aliponukuliwa alisema kuwa "amekufa"

Alitumia Jeshi kudhulumu Korosho za wamakonde; kila walipodai haki yao kwa mujibu wa Sheria alijitokeza hadharani mwenyewe na kumwambia PM iwapo wataandamana ataanza na shangazi zake kuwapiga virungu (udhalilishaji na ubabe)

Sote tunajua kwamba Tanzania Ni nchi ya vyama vingi inayoheshimu utawala wa Sheria na demokrasia. Alitamka wazi wazi kwamba siwezi kukupa mshahara nyumba na gari halafu umtangaze mpinzani ameshinda uchaguzi! Kauli yake ilikua nzito na mwangwi wake ulionekana kwenye chaguzi mbili mfululizo (mitaa na uchaguzi mkuu) Kuna watu wanaachiliwa huru hivi Sasa na Mahakama za Rufani kwa kubambikiwa kesi za mauaji. Hakuwahi kujitenga na Mambo haya hata siku moja isipokuwa aliwazawadia vyeo kina Mahera na wenzake! Alienda mbele kuwafananisha binadamu wenzie na magunzi! Kwamba ukichanganya betri na magunzi haviwaki na kutamka wazi kwamba msipochagua CCM sileti maendeleo!

Bomoa bomoa ya kimara hakuna atajayeishahu shida Ni kwamba alipokua mwanza alitamka hadharani kuwa wale was mwanza walimpigia kura kwahiyo wasibomolewe huo Ni ubaguzi wa wazi wazi usiotilia Shaka.

Mambo Ni mengi Sana ukiyaandika hayaishi Wala kitabu hakitatosha!
Alikua na mazuri yake lakini maovu yali-outshine mazuri yake! Kwakua aliwaongoza watu waacheni waseme ili viongozi wajao wajifunze kuwa mabaya au mema ya mtu huambatana nae. Kifo hakikupi Kinga ya kujadiliwa kabisa.
Adious
 
Nimekuambia hakuna adui wa wote

Hata jambazi anaweza kuwa kaksi na katili wa kutisha lakini hawezi kukosa rafiki au watu wanao msapoti
Mkumbushe kuwa kule South America Kuna drug dealers mtaani kwao wanaonekana Mashujaa
 
Povu la nini? Kama una mazuri ya yule Ziraili mtoa roho za watu yaweke, ila usizuie watu kuandika uovu wa Magufuli.

Sasa unajiita Taikon wa Fasihi lakini hutaki FASIHI itumikke kukosoa matendo ya watawala.
 
Mimi simtetei Magufuli, Ila nashangaa wanaomtaja taja ilhali wapo wabaya wengi Waliohai.

Kwenye vita Watu hupigana na wanajeshi Waliohai na sio kupigana na maiti zilizodondoka chini
Basi katika kusifia wasifie walio hai Mana wafu hawawezi kupokea sifa wameshakufa.

Wanaosababisha watu wamtaje Sana hayati Ni wafuasi wake wanaoliinganisha wakati wa uongozi wa watu walio hai na uongozi wa marehemu!
 
Naona wanapunguza hasira tu wala hakubadilishi chochote, naona wanajistess maana wakiona mtu kaandika mazuri ya Magufuli wanajaa gesi kuandika aya ndefu ndefu, wanahitaji mwanasaikolojia ujue hawajui hawako OK.
Hilo la kuhitaji mwanasaikolojia ni suala la kweli kabisa si utani, hawa jamaa hawapo sawa.
 
Unapoteza muda kulitetea Hilo jangili
 
Mkuu hii barua yote unarudia kueleza mabaya ya Magufuli, huu uzi unahoji kwamba huku kulala na kuamka kutwa kuzungumzia mabaya ya Magufuli inatuletea faida? Toka Magufuli afariki hadi leo karibu miaka miwili bado tu tunaeleza mabaya ya Magufuli kama bado yupo hai, shabaha ya kufanya hivi ni nini au ndio kupunguza tu hasira?
 
Reactions: nao
Shabaha ya kufanya hivi Ni:
1. Viongozi waliopo na watakaokuwepo wajue kwamba uongozi Ni dhamana na watu walioko chini yao wapaswa kuongozwa kwa haki na usawa bila ubaguzi wa namna yoyote ile.

2. MAMA TANZANIA Ni Mali ya watanzania wote hivyo kila mtu ana haki katika Jamhuri kwa mujibu wa Sheria tulizojiwekea wenyewe na Tanzania sio Mali ya mtu mmoja ajiamulie atakavyo Kama Yuko kwenye familia yake au geto kwake.

3. Kifo sio KINGA ya kutokusemwa mabaya ukiyotenda ukiwa hai hivyo matendo ya mtu yataambatana nae vizazi na vizazi yakiwa mema sawa yakiwa mabaya sawa. Sisi wakristo matendo ya watawala na watu waovu yanerkodiwa barabara katika kitabu kitakatifu ili binadamu tujifunze kupitia hayo! Ingekua kifo kinatoa Kinga ya kutosemwa Basi habari Za Nebukadneza na Faraoh au Herode zisingeandikwa kamwe!

4. Na nikwambie hakuna mtu ana chuki binafsi na Magufuli, kwa sababu alikua mtawala wa Jamhuri na sio kiongozi wa familia ya mtu awaye yeyote, watu Wana chuki na tabia zake mbaya, hulka yake mbaya na mfumo mbaya aliouasisi ambao Ni kinyume na Mila na desturi zetu sisi watanzania!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…