Kuendelea kumtaja Hayati Magufuli kwa mabaya ni upuuzi wa ajabu

Nadhani hujui unachokitaka! Rudia kusoma ulichoandika!
Magufuli alikua kiongozi wa kisiasa na sio kiongozi wa Parokia!

Kwenye siasa Kuna watu walimchagua na Kuna watu hawakumchagua, Kuna watu aliwaibia kura zao kwa lazima hawatampenda kamwe!

Kuna watu wakifurahishwa na alivyoumiza watu kwa matamshi yake binafsi yasiyoendana na Mila na desturi zetu za kitanzania hawatamsifia Wala kumpenda!

Unapoona watu wengi wanapiga mayowe na kulalamika juu ya ufidhuli wake! Ujue mabaya yalizidi mema! Vumilia tu mzee
 
Mimi sikumwelewa magu kabisa. Yaani huyu mzee aliendekeza udikteta hadi kwenye michezo. Kwa vile yeye alikuwa makolo, acha atuundie zengwe wananchi. Kamata manji weka ndani. Sukuma manji ndani, filisi kabisa ili asifadhili yanga yangu, acha yanga iyumbe, hakuna pesa. Daah, miaka yote ya magu ubingwa ukawa mthimbadhi. Aiseee! Toka mbeleko imekatika watani hawana hali. Lakini sijui walikosana nini na "Mo" heeee! wasiojulikana hao kwa "mo" jamani baba yuleee. Msimtajetaje mwendazake.
 
Wataje kwa majina acha kuelea hewani bwana Mzee JF Ni GT forum!
Waziri Nape amekuwa anatoa majibu ya dharau kwa wananchi wanapohoji masuala ya msingi kwenye wizara yake, Nape anajua hamna la kumfanya nyie mpo busy kueleza mabaya ya Magufuli. Lakini pia kuna Waziri Makamba na Mwigulu wote wamekuwa wakionyesha viburi wazi wazi. Binafsi nachokiona funzo litakalopatikana ni kwa ccm kuzingatia asije tena mtu kama Magufuli ambaye atawagusa hadi watoto wa mjini wenyewe chama chao.
 
Nilichokielewa ni kwamba kumbe zinatumika hisia zaidi kwenye hii mijadala, kwamba kwa sababu mie sikumpenda aliiba kura basi nitaeleza mabaya yake tu kwa sababu simpendi na mwengine kwa sababu sikupendezwa na kauli zake basi nitaeleza mabaya yake tu sitamzungumzia tofauti na mabaya yake.
 
Hizo sio hisia huo Ni uhalisia unapenda na established facts na sio hearsay's! Hisia Ni feelings hapa hakuna feelings Ni ukweli! Na huwezi kumpangia mwanadamu namna ya kukutazama!

Na kueleza mabaya ya mtu sio kwa sababu humpendi unampemda ndio Mana hutaki ayafanye hayo mabaya na unawapenda watu wengine kwa maana hiyo hutaki waumizwe na mabaya hayo au waige hayo mabaya!

Kama wewe Ni mkristo utasoma biblia Yohana mbatizaji alikatwa kichwa sababu alikemea uovu wa Herode!

Tusiache kuwalaumu watu kwa mabaya yao ili yasijiruddie tena.
Kama una nafasi ya musafisha msafishe tu Ila usilazimishe watu wote wamuone malaika Kama alivyokufuru yeye mwenyewe!
 
Ila kumtaja Idd Amin kwa mabaya au Hitler?
Ushasikia wanasiasa wa Ujerumani wakishinda majukwaani kulaani utawala wa Hitler? Hata hapo Uganda nitajie mwanasiasa anayeimba habari za Idd Amin!

Mwanzisha mada anamaanisha Magufuli ameshatangulia hakuna tunaloweza kubadili lakini waliohai ndio wanaowajibika sasa! Kila mabadiliko tunayotaka Magufuli hawezi kutusaidia bali Mama Samia.

Ila inaonekana kumtukana Magufuli ni kama ajenda ya kimkakati! Bahati mbaya wananchi wa kawaida wanaamini hivyo pia.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Reactions: nao
Brother nikwambie ukweli tu hakuna anayemtukana Magufuli!

Historia Ina vitu vifuatavyo:
1. Who
2. Why
3. When
4. Where

Hapo kwenye when ndio wapaswa ujifunze kuwa Ni swla la muda au wakati, itafika wakati kizazi Cha kumtaja mwendazake kitakua hakipo kabisa kumlaumu au hata kumsifia kwa sababu there is little eye witness accounts au actual experience of the situation.

Ni miaka miwili tu imepita tangu atangulie kuzimu! Sio rahisi hivyo kuondoka midomoni mwa watu waliompenda na waliomchukia!

Huwezi kusikia habari za hitle kwani ni zaidi ya miaka 80 imepita tangu auondoke kwenye uso wa dunia!
Habari zake tutazisoma tu kwenye kumbukumbu na documentaries zinazotengenezwa vivyo hivyo kwa Jiwe.

Na kwa bwana Nduli amini toka Waka 78 Ni zaidi ya miaka 40 Sasa kwa hiyo Kuna kizazi kkikichoexperiece utawala wake alikua Ni wimbo kila sehemu lakini with time everything fade away.

Wakati huu Ni kuvumilia tu watu waseme watu wafanye reforms maisha yaendelee! Ni ngumu kuwaziba midomo watu walioonja utamu na ugumu wake!
 
Kuna waovu wangapi duniani wanashabikiwa au muovu lazima awe kiongozi wa nchi?
Wewe usiwapangie watu cha kuandika humu kama wewe humsemi kimpango wako. Kaa pembeni kuleee [emoji117][emoji117][emoji117][emoji117][emoji117][emoji117]
 
Hajawahi kutokea Kiongizi mwizi na muuaji kama magufuli
 
Huyo Magu inabidi mabaya yake yaendelee kutajwa na ikibidi yaingizwe kwenye mitaala wanafunzi hata wa vizazi vijavyo wayasome mabaya yake kama wanavyosomwa akina Hitler, Mussolini au aliyekuwa jirani hapa Idd Amin Dada.
Kuna faida kubwa kukumbushana mara kwa mara ili kuwa na umakini makosa ya kuwa na aina fulani ya viongozi yasiwe yanarudiwa.
 

Tutake tusitake Magufuli ataendelea kutajwa kwa mazuri na mabaya. Lakini watu watakumbuka mabaya kuliko mazuri muda unavyokwenda huo ndiyo ukweli. Hili ni fundisho watu wakifa na kukakuwepo fikra kwamba umeshiriki hautakwepa lawama milele. Sasa wajukuu wa Magu wanaanza kumjua kama muuaji na sio shujaa. Hakuna hata mtu mmoja ameshawahi kusema Mzee Mwinyi ni muuaji mzee wa watu ana miaka zaidi ya 90 kwasababu aliishi kwa utu. Tupende tusipende kwenye ukatili uncle wangu Magu ni ngumu kumtetea.
 
Binafsi sikumbuki kumponda wala kumsifia huyo mtu.

Ila jambo ambalo mleta mada hajalielewa nikwamba unapomsifia mtu kubali watakao mpinga.
Pia unapompinga mtu tambua kama wapi wanaomkubali na watamsifia

Sifa na kejeli,kukubalika na kukataliwa,kukwezwa na kutwezwa ndio mizani za matendo ya binadamu katika maisha
Wewe mleta mada pasipokujua umesababisha watu wamponde huyo ambae umesema ni mfu asijadiliwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…