Kuendelea "kusinyaa" kwa CHADEMA nani alaumiwe?

Jiwe na maccm ndio walaumiwe! Wakora wakubwa sana! Jiwe alileta Siasa za visasi na ukichaa!
 
Labda ni yule wa milele, sina uhakika though
 
Umeleta uzi mwenyewe na umeutawala mwenyewe. Hongera sana mkuu.
 
 
Ofisi za Kanda magari yote aliyonunua Mbowe yamekufa. Yalikuwa ya mitumba, na mengi yalikaribia kuwa write off
 
kiliazima
Kama imesinyaa CCM wakubali kura zipigwe wazi zihesabiwe wazi CCM wakipata hata 20% ya total votes nahama nchi naenda Afghanistan,CCM kilishakufa,lingine JPM aliharibu morali ya watu kupiga kura,kama CCM wanajua hawajasinyaa wanaogopa Nini tume huru ya uchaguzi na katiba mpya yenye Taasisi imara?CCM wakubali kura ziwe huru waone nani kasinyaaaa
 
Kinasinyaa sababu ya mikakati ya CCM, kuanzia polc-CCM, mamlaka za kiserikali - watu wanasota gerezani, wengine wanapotezwa, na serikali haifanyi chochote - Hatushangai ndo tabia za kiafrika hasa haya ma-vyama yalorithi baada ya wakoloni - yanalewa madaraka, wanachama wake wanakuwa pro - chama na wafia chama kuliko Taifa.
Vyombo vya dola vyote viko huko, ni winga lao - hakuna instruments ambazo ziko huru kupromote demokrasia. Na cha ajabu nyie ma-pro CCM amuoni umuhimu wa vyama vingi vyenye nguvu - mnaendeshwa na mitamaa na ulafi wa mali tu - NDO MAANA VYAMA vingi vya upinzani vinapitia changamoto-
Sema sasa matokeo yake tutakoma wote - watoto wenu, wajukuu zenu, vilembwe vyenu navyo vitapita kwenye moto uleule tu - wa effects ya kuwa na mfumo wa udikteta wa kichama - mnaua checks and balance - mnaua ushindani...
Mkimaliza upinzani mtaanza kumalizana nyinyi kwa nyinyi sababu binadamu sio kondoo - na mmeishaanza - si unaona akina Mpina - sasa subiri mmalize kabisa mtagundua kuwa mnaenda kinyume na ulimwengu -
 
Wanasubiri makapi ya ccm wataamka tena

Agent mwenyewe anasubiri msimu wa mavuno
 
Ccm hawatakinupinzani kabisa wanatumia Kila mbinu kuwadhoofisha cdm sababu no hizi
1. Kutekwa
2.Kuua
3.Kuhonga
4. Kujaribu uchaguzi
5. Kuiba kura
6. Kuwanyima maendeleo maeneo yaliyochavua wapinzani
6. Kubana media zote
8. Vitisho
9.kudhoofisha kiuchumi

Lakini yote kwa yote chadema inaweza kufa au kupoteza lakini upinzani tangu
1995 wakati wa lyatonga hautakaa ufe utabafilika na upepo uliopo

Kwa mauaji na utekaji huu watu wameogopa kujitokeza hadharani kama wapinzani

Lakini pia chadema inahitaji viongozi wapya mwenyekiti mpya na katibu mpya Hawa waliopo hawana mvito tena

Mwenyekiti kafunga mikata na samia mpaka 2030 Kavita hela ndefu hana Cha kupoteza
 
Ccm hawaki upinzani
Wanatumia Kilabinu upinzani ufe
Juzi wamemuu Mzee kibao sasa kwa Hali hii cdm itastawi vipi
 
Ccm hawaki upinzani
Wanatumia Kilabinu upinzani ufe
Juzi wamemuu Mzee kibao sasa kwa Hali hii cdm itastawi vipi
si kweli,
upinzani katika ujumla wake unajimaliza wenyewe kutoka taasisi za kisera za kisiasa hadi kua taasisi za kiraia za kibinafsi kulalamika tu 🐒
 


Yaani tatizo la Watanzania vijana wa siku hizi ni upewo mdogo. Tunawajua vijana kwa maandiko yenu. Tatizo sio Chadema ni CCM kupumbaza Watanzania. Tanzania ni nchi ambayo vijana wamelala na kuweka uchawa na hata hawajui waendako. Juzi vijana wa muziki walikuwa wanalalamikia ukiritimba wa vibali lakini wakikutana na viongozi badala ya kueleza matatizo wanajikita kwenye uchawa.

Tatizo la Tanzania ni Watanzania wenyewe. Hamuwezi kukaa na kushinda mitandaoni halafu kuwasubiria eti Mbowe, Lissu, Zitto na wengine kuwaletee maendeleo. Wakina Mama na vigogo wa CCM wameshajua vijana wanajali kiki na uchawa tu sasa wanajaza ndugu zao kwenye uongozi. Raisi Samia watoto wake na mpaka wakwe wake wapo madarakani njie mnatumwa kutukana Chadema mitandaoni. Hao viongozi wa Chadema ni watu wa kawaida na maisha yao. Kama watanzania wanapenda hizi rushwa, ukiritimba, uchawa, undugu wa sasa mnabakia kuwa masikini tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…