Kuendelea kutumia Kiswahili Shule ya msingi ni kujipiga mtama wa kitaaluma

Kuendelea kutumia Kiswahili Shule ya msingi ni kujipiga mtama wa kitaaluma

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Sioni sababu ya kujifunza kwa Kiswahili Shule ya msingi.

1: Walimu wao wanajifunza kozi kwa Kiingereza.

2: Kiswahili tayari tunakiongea nyumbani hata Mtoto akitoka Shule atakiongea hawezi kukisahau.

Hasara tunazopata

1: Watoto wa shuleza msingi wanakuwa wazito na hawaendani na kasi ya dunia.

2: Maarifa mengi ya ziada yako kwa kimombo watoto tunakuwa tumewafungua kwenye kasha la Kiswahili.

Maoni

Kiswahili libaki kama somo tuwafungulie watoto wetu kujuifunza mambo kwa Kiingereza.

Kama ni shida miundombinu angalau tuanze kwa Shule zote za kwenye majiji na miji mikubwa.

Ni hayo tu
 
kuna wimbo wa Senzo anasema Who's gonna care for you and I

hii ni kweli dunia ya saivi maarifa yapo kwa kiingereza mtu anamaliza degree hata masters ila English bado inamsumbua sasa huyo mtu atawezaje kugrasp knowledge mpya hata you tube au platforms nyingine
 
Ni kwel kabsa unayoyasema lakin mabadiliko hayatatokea kwasababu wenye nyazifa za kufanya mabadiliko watoto wao hawapo kwenye hzo shule
Kabisa..
Watoto wa wakubwa wanasoma Academy halafu wanapewa scholarship za kwenda kusoma elimu ya juu huko nje - Canada, Us, Eu, nk..
Meanwhile, Wakubwa wanawaambia wanyonge kuwa Kiswahili Kwa sasa ni 'Bidhaa' adimu, wakomae nacho!
Miaka ijayo kutakuwa na tabaka la 'watwana' na 'mabwana' kutokana na huu msingi wa kibaguzi wa elimu!
 
Hakuna anayekiogopa. Hakifai kutumika kufundishia kwenye nchi yetu.
Unatakiwa uwe na nguvu ya uchumi pia ili kuendelea kukomaa na kiswahili hiki.

Unamfundisha mtoto kwa kiswahili ... hata chuo watu wanamaliza hawako vizuri sababu ya kuchanganya lugha ... utashindana na nani kwenye soko la ajira kidunia .... Hatuoni wakenya na waganda wanavyochukua fulsa.. hata kujiamini kunashuka .... Kama tunakipenda kiswahili basi kuna jambo la kufanya kuhusu uchumi wetu ili tuweze kujitegemea kwa sehemu kubwa.
 
Hakuna anayekiogopa. Hakifai kutumika kufundishia kwenye nchi yetu.
Taarifa nyingi za maana zipo kwa kiingereza. Watoto wa Shule za serikali huwa ni watafiti na wanaakili kuliko international. Wakiongezewa dimension ya English kuanzia chekechea, nchi nzima itachangamka kiakili
 
Huwezi kusoma kiingereza hujui hata kuandika "shangazi "

Kiufupi shule za msingi ndio watoto wananza kujifunza kusoma na kuandika kiswahili achilia mbali kiingereza ambacho maneno yake ni magumu kwa mtoto mdogo
 
kwenye umri huo ndio mda sahihi wa kujifunza hayo unayosema magumu .... kiswahili kiwe somo kama somo .... kwa kuwa kiswahili kinaongelewa nyumbani watakijua tuu ...

Option ya pili ... kama tunakipenda sana kiswahili chetu ... tubadili mitaala yetu level zote ziwe kiswahili ili iwe rahisi kwa wote kujifunza. Hapo hapo unatakiwa ukapambanie Ajira/fulsa za kimataifa na kiswahili chako ....
 
Yani Kama kiingereza ni cha kubabaisha,hata kujiamini kunapungua kabisa...kilichobaki ni kila mmoja apambane na watoto wake katika hali Kama hii.
 
Huwezi kusoma kiingereza hujui hata kuandika "shangazi "

Kiufupi shule za msingi ndio watoto wananza kujifunza kusoma na kuandika kiswahili achilia mbali kiingereza ambacho maneno yake ni magumu kwa mtoto mdogo
Ukijua kuandika shangazi na aunt kwa pamoja kuna tofauti gani.?

English medium za serikali Olympio, Diamond na nasikia wanafungua nyingine mawilayani wao hawakuona hilo la 'Shangazi'?
 
Hivi mnajua huko vijijini watoto hawajui kabisa kiswahili 😂😂😂,asilimia 70% shule za vijijini watoto wao wanongea lugha za kabila lao na walimu wanatumia nguvu kubwa Sana shuleni kuwasisitiza kuongea kiswahili ....!mpaka watoto wananza darasa la kwanza ndio wanakuja kujua kuwa Kuna lugha inaitwa kiswahili .....

Hii nchi Bado ni masikini sanaa Tena wa kutupwa ,msijipe mambo ambayo hamuwezi ,...kisa nyie mmekulia mjini mnajiona Tanzania yote ipo hivo 😂😂😂😂tembea uone ...Kuna maeneo unaweza kukataa hadharani kuwa hapa sio Tanzania ,ni Burundi au congo ....
 
Kutumia kiingereza sekondari na chuo kikuu ndiyo kujidumaza, na ujinga mkubwa. Kiingereza tungejifunza kama lugha tu.
Wana jf mimi ninavyojua lugha ni utamaduni hiyo kushadidia lugha za wengine hasa kiingereza ni kwamba kuoenda utamaduni wa kiingereza na kuudharau utamaduni wa mswahili kama ambavyo wakoloni walivyotuaminisha kuwa utamaduni wetu ni wakishenzi
 
Hivi mnajua huko vijijini watoto hawajui kabisa kiswahili [emoji23][emoji23][emoji23],asilimia 70% shule za vijijini watoto wao wanongea lugha za kabila lao na walimu wanatumia nguvu kubwa Sana shuleni kuwasisitiza kuongea kiswahili ....!mpaka watoto wananza darasa la kwanza ndio wanakuja kujua kuwa Kuna lugha inaitwa kiswahili .....

Hii nchi Bado ni masikini sanaa Tena wa kutupwa ,msijipe mambo ambayo hamuwezi ,...kisa nyie mmekulia mjini mnajiona Tanzania yote ipo hivo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]tembea uone ...Kuna maeneo unaweza kukataa hadharani kuwa hapa sio Tanzania ,ni Burundi au congo ....
Ndio maana inaitwa shule/masomo ... kutojua kiswahili haiwazuii wao kufundishwa kwa mtaala wa kingereza ... na kiswahili likabaki kama somo .
 
Yani Kama kiingereza ni cha kubabaisha,hata kujiamini kunapungua kabisa...kilichobaki ni kila mmoja apambane na watoto wake katika hali Kama hii.
Kwelii mkuuKama kiingereza ni cha kubabaisha,hata kujiamini kunapungua kabisa...kilichobaki ni kila mmoja apambane na watoto wake katika hali Kama hii.
Kweli
Hivi mnajua huko vijijini watoto hawajui kabisa kiswahili 😂😂😂,asilimia 70% shule za vijijini watoto wao wanongea lugha za kabila lao na walimu wanatumia nguvu kubwa Sana shuleni kuwasisitiza kuongea kiswahili ....!mpaka watoto wananza darasa la kwanza ndio wanakuja kujua kuwa Kuna lugha inaitwa kiswahili .....

Hii nchi Bado ni masikini sanaa Tena wa kutupwa ,msijipe mambo ambayo hamuwezi ,...kisa nyie mmekulia mjini mnajiona Tanzania yote ipo hivo 😂😂😂😂tembea uone ...Kuna maeneo unaweza kukataa hadharani kuwa hapa sio Tanzania ,ni Burundi au congo ....
Hivi mnajua huko vijijini watoto hawajui kabisa kiswahili 😂😂usiklimia 70% shule za vijijini watoto wao wanongea lugha za kabila lao na walimu wanatumia nguvu kubwa Sana shuleni kuwasisitiza kuongea kiswahili ....!mpaka watoto wananza darasa la kwanza ndio wanakuja kujua kuwa Kuna lugha inaitwa kiswahili .....

Hii nchi Bado ni masikini sanaa Tena wa kutupwa ,msijipe mambo ambayo hamuwezi ,...kisa nyie mmekulia mjini mnajiona Tanzania yote ipo hivo 😂😂😂😂tembea uone ...Kuna maeneo unaweza kukataa hadharani kuwa hapa sio Tanzania ,ni Burundi au congo ....
Hata Kampala nilifika Mara ya kwanza nikajichanganya mtaani usiku, hawajui kiingereza wala kiswahili wanatwanga kilugha jiji zima. Nilivyouliza nikaambiwa kiingereza na kiswahili wanajifunzia Shule ni.

Hata huko kijijini inawezekana.
 
Back
Top Bottom