Tanzania haina competitive advantage ya kuendelea kwa lugha ya kiswahili. Wachina wengi wanaokuja huku hawajaenda Shule lakini licha ya kujua kichina wanaABC za English.
Kuna MTU huwa namtafsiria message za kiswahili kwenda kingereza ili aongee na bosi wake mchina Whatsapp. Bosi yuko China hajaenda Shule sana ila ni mfanyabiashara mkubwa anajua English kidogo kama daraja.
Hao wote uliowataja sio wajuha kuhivyo, tayari wanawatu wao walitawanyika duniani Siku nyingi hivyo kila taarifa na mambo ya Muhimu tayari yapo kwao kwa lugha zao sio sisi.
Na kila wakitaka kuchukua hatua za kimataifa lazima wajifue kiingereza hata kama hawajaenda
Apa unachanganya mambo mawili mkulungwa
Sina shida na mtu kujifunza lugha yoyote iwe kingereza, kichina kijapani, kisambaa, kichaga n.k, kwani lugha ni jambo muhimu sana katika mawasiliano na maendeleo kwa ujumla
Shida yangu ni namna ambavyo tutatumia lugha ya ughaibuni kujistaarabisha, kujipatia maarifa au generally kujipatia elimu
Ikumbukwe kwamba lugha sio maneno tu yatokayo mdomoni bali lugha ni chombo muhimu sana ambacho kimebeba utamaduni, maarifa na juzi mbalimbali za watu wa jamii fulani
Na ikumbukwe pia lengo la elimu sio kutoa kijana "smati" anayechomekea na mwiko anayezunguka na bahasha kuomba ajira za kola nyeupe....refer interview wanahitajika watu watatu wanaoenda kuomba ni 500?
Lengo la elimu ni kumfanya kijana ama mtu yeyote kuweza kuyatumia mazingira yanayomzunguka pamoja na rasilimali zilizopo kuweza kujiletea maendeleo.....
Mathalani uwepo wa makumi elfu ya mahekta vijijini huku watu wakilia njaa ndio ujinga wenyewe ama kutokuelimika
So bado napinga jambo la kuifanya elimu yetu itolewe kwa lugha za kigeni ila nasapoti lugga za kigeni ziwe nyongeza ya lazima kwenye masomo yetu
Note: sina imani na mfumo wa elimu nchini
Kwamba ukijua kinjekitile ngwale kafa lini ndio tayari ushaelimika?
Tujaribuni kuchek china, india malaysia, brazil, wanatoa elimu ya namna gani
Ukishaelimika kichwani utachangamana na jamii yyte ile hta wamasai na hata usijue lugha zao utafanya nao miamala mbalimbali hata kwa kutumia wakalimani
Mfano wachina wanafuata fursa uku bongo wakiwa weupe hawajui kiswahili ama kingereza ila wanasavaivu