Kuendelea kuwekewa "mbinyo" na Jumuiya ya kimataifa, ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kuiokoa nchi yetu katika anguko la kidemokrasia

Kuendelea kuwekewa "mbinyo" na Jumuiya ya kimataifa, ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kuiokoa nchi yetu katika anguko la kidemokrasia

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Nchi yetu iko katika mfumo wa vyama vingi kama inavyobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1)

Kwa Bahati mbaya sana, ingawa Katiba ya nchi inatamka hivyo, watawala wetu wanaonekana kabisa ni watu wasioutaka kabisa mfumo wa vyama vingi na wanatulazimisha watanzania wote turejee kwenye mfumo Wa Chama kimoja cha CCM.

Ushahidi wa wazi ni namna uchaguzi mkuu uliopita ulivyoendeshwa, hadi kutolewa matokeo ya mwisho, ambayo yamempa ushindi Wa asilimia zaidi ya 84, mgombea wake John Pombe Magufuli na kujizolea viti 262 vya ubunge kati ya viti 264!

Sasa kazi ipo katika uundwaji wa Kamati za Bunge, ambapo inatakiwa:-

1. Kamati za hesabu za serikali (PAC)
2. Kamati ya mashirika ya Umma (POAC)
3. Kamati ya serikali za mitaa (LAAC) ni "lazima" ziongozwe na wabunge wa upinzani.

Swali kubwa wanalojiuliza watawala je watawapataje wabunge hao wa upinzani wakati wnyewe ndiyo "waliouvuruga" uchaguzi huo hadi kutopatikana kabisa wabunge hao wa upinzani?

Nimesikia fununu kuwa wafadhili mbalimbali, ambao ndiyo huwa wanatufadhili kwa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi trilioni 2 kila mwaka "wanakomalia" kuwa ni lazima sharti hilo litimizwe ndipo walete hayo mapesa yao.

Tumesikia kauli zilizotolewa na washirika mbalimbali wakiwemo Umoja wa mataifa, Ubalozi wa Marekani, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Japan na Jumuiya ya nchi za Ulaya za kutotaka kuutambua uchaguzi huu uliopita kuwa haukuwa na viwango vya kuitwa ni uchaguzi uliokuwa Huru na Haki.

Je, nchi yetu ambayo imegeuka kuwa ombaomba, japo "inajimwambafai" kuwa inaweza kuwa "donor country" itaweza kumudu kuendesha shughuli zake bila kuwategemea hao wafadhili?

Swali muhimu ambalo tunapaswa tujiulize wananchi wote Wa nchi hii, je nchi yetu itakuwa imefuata njia iliyopitia Zimbabwe kwa kuyafanya maisha ya kila Mtanzania kuwa magumu mno kutokana na kiburi cha watawala wetu wa kutaka mfumo wa chama kimoja ambapo ni kinyume cha Katiba ya nchi?
 
Hata mbinyo ukiwekwa wanaoumia ni wananchi wa kawaida wala usitegemee viongozi wataathirika labda waweke mbinyo kwa viongozi binafsi na familia zao
Ninesikia fununu watawala wetu watawekewa "mbinyo" mkubwa wao binafsi ya kutosafiri kwenda kwenye hizo nchi, kufunga account zao kwenye mabenki ya nchi hizo na kutoleta pesa za misaada kwa nchi yetu.

Je unaviona hivyo vikwazo ni vidogo?
 
Vikwazo vya namna hiyo naviunga mkono kwa sababu vinawagusa moja kwa moja waliohusika
 
Bora wake mbinyo ili mwisho wa siku tupate mabadiliko. Japo tutaumia, ila bora tuumie kwa muda kuliko kuishi katika hali hii.
Hivi kipi bora !

Uumie juani unajitafutia ridhiki kwa jasho lako na baadaye ulie kivulini matunda ya jasho lako kwa kujitegemea bila masimango wala masharti yasiyotamkika kinywani au uumie ukiwa kivulini na kisha uanze kufurumishiwa mabomu utoke hapo kivulini na baadaye ulie juani matunda ya uzembe wako wa kushindwa kujitegemea huku ukisimangwa na kupewa masharti yasiyotamkika kinywani na kuyatekeleza kwa mijeredi kutoka kwa hao unaowaabudu!!

Yaani ninyi ihiii!!!
 
Uchaguzi ukiwa Huru na Haki, CCM ijiandae kukabidhi Ikulu.
Nimemnukuu Katibu Wa Uenezi na itikadi wa CCM, Humphrey Polepole
 
Hivi kipi bora !

Uumie juani unajitafutia ridhiki kwa jasho lako na baadaye ulie kivulini matunda ya jasho lako kwa kujitegemea bila masimango wala masharti yasiyotamkika kinywani au uumie ukiwa kivulini na kisha uanze kufurumishiwa mabomu utoke hapo kivulini na baadaye ulie juani matunda ya uzembe wako wa kushindwa kujitegemea huku ukisimangwa na kupewa masharti yasiyotamkika kinywani na kuyatekeleza kwa mijeredi kutoka kwa hao unaowaabudu!!

Yaani ninyi ihiii!!!
Ni bora huyo Jiwe apewe adhabu kali, yani kwenye uchaguzi mkuu unaleta kura feki na kura za wananchi hazihesabiwi!!
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Ni bora huyo Jiwe apewe adhabu kali, yani kwenye uchaguzi mkuu unaleta kura feki na kura za wananchi hazihesabiwi!!
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Kura feki zingepitia wapi wakati tayari Lissu kashatuhakikishia hakuna kura feki wala figisu inaharibu utaratibu wa uchaguzi wa mwaka huu!? Na akaongeza kuwa dunia inafuatilia kila kitu kinachoendelea hapa nchini.

Ni wiki na ushee sasa uchaguzi umepita. Dunia imenyamaza wala haizungumzii habari za kura feki wa kura za mabegi! Ila ninyi tu mmejificha kwa uongo mliofundishwa na Antipasu ilikuficha aibu ya matokeo yenu ya uchaguzi. Mpone sasa muanze kufanya kazi acheni kujichechemesha!
 
Katika msitu mmoja nyani waliweka kikao, Ili kujadili ni namna ganii watamdhibiti binadamu aliyekua akiwafukuza pindi walapo mahindi aliyo yapanda!, Basi bwana wakafikia muafaka wa kumuua yule binadamu, na siku hiyo jioni walikula mahindi yote yakaisha, ilipofika mchana wa siku iliyofuata wakaenda shambani, Ila hawakukuta kitu mwisho walikufa na njaa.

NOTE: MAPAMBAZUKO YANAPOKARIBIA KIZA HUWA TOTORO.

Penda nchi yako
 
Kura feki zingepitia wapi wakati tayari Lissu kashatuhakkkishia hakuna kura feki wala figisu inaharibu utaratibu wa uchaguzi wa mwaka huu!? Na akaongeza kuwa dunia inafuatilia kila kitu kinachoendelea hspa nchini.

Ni wiki na ushee sasa uchaguzi umepita. Dunia imenyamaza wala haizungumzii habari za kura feki wa kura za mabegi! Ila ninyi tu mmejificha kwa uongo mliofundishwa Antipasu ilikuficha aibu ya matokeonyenu ya uchaguzi. Mpone sasa muanze kufanya kazi acheni kujichechemesha!
Huyo Mh Lissu alipokuwa Kawe alisema Magufuli/Tume wameandaa kura feki za Jiwe kiasi gani na Magufuli kapata kiasi gani kama unakumbuka?

To be honest, Magufuli hajawahi shinda uchaguzi wowote toka akiwa mbunge.
 
Huyo Mh Lissu alipokuwa Kawe alisema Magufuli/Tume wameandaa kura feki za Jiwe kiasi gani na Magufuli kapata kiasi gani kama unakumbuka?
To be honest, Magufuli hajawahi shinda uchaguzi wowote toka akiwa mbunge
Kwa faida ya wana JF ungetutajia alichosema Tundu Lissu siku hiyo na kilichotokea siku ya uchaguzi.
 
Uko sahihi, lkn lazima kuwe na MTU shupavu wa kuyasemea.
Umeongea vyema, Nimekuja kugundua kwambaTanzania hakuna watu/mtu shupavu. Shupavu tuliowategemea wameonyesha taswira tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom