Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Nchi yetu iko katika mfumo wa vyama vingi kama inavyobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1)
Kwa Bahati mbaya sana, ingawa Katiba ya nchi inatamka hivyo, watawala wetu wanaonekana kabisa ni watu wasioutaka kabisa mfumo wa vyama vingi na wanatulazimisha watanzania wote turejee kwenye mfumo Wa Chama kimoja cha CCM.
Ushahidi wa wazi ni namna uchaguzi mkuu uliopita ulivyoendeshwa, hadi kutolewa matokeo ya mwisho, ambayo yamempa ushindi Wa asilimia zaidi ya 84, mgombea wake John Pombe Magufuli na kujizolea viti 262 vya ubunge kati ya viti 264!
Sasa kazi ipo katika uundwaji wa Kamati za Bunge, ambapo inatakiwa:-
1. Kamati za hesabu za serikali (PAC)
2. Kamati ya mashirika ya Umma (POAC)
3. Kamati ya serikali za mitaa (LAAC) ni "lazima" ziongozwe na wabunge wa upinzani.
Swali kubwa wanalojiuliza watawala je watawapataje wabunge hao wa upinzani wakati wnyewe ndiyo "waliouvuruga" uchaguzi huo hadi kutopatikana kabisa wabunge hao wa upinzani?
Nimesikia fununu kuwa wafadhili mbalimbali, ambao ndiyo huwa wanatufadhili kwa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi trilioni 2 kila mwaka "wanakomalia" kuwa ni lazima sharti hilo litimizwe ndipo walete hayo mapesa yao.
Tumesikia kauli zilizotolewa na washirika mbalimbali wakiwemo Umoja wa mataifa, Ubalozi wa Marekani, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Japan na Jumuiya ya nchi za Ulaya za kutotaka kuutambua uchaguzi huu uliopita kuwa haukuwa na viwango vya kuitwa ni uchaguzi uliokuwa Huru na Haki.
Je, nchi yetu ambayo imegeuka kuwa ombaomba, japo "inajimwambafai" kuwa inaweza kuwa "donor country" itaweza kumudu kuendesha shughuli zake bila kuwategemea hao wafadhili?
Swali muhimu ambalo tunapaswa tujiulize wananchi wote Wa nchi hii, je nchi yetu itakuwa imefuata njia iliyopitia Zimbabwe kwa kuyafanya maisha ya kila Mtanzania kuwa magumu mno kutokana na kiburi cha watawala wetu wa kutaka mfumo wa chama kimoja ambapo ni kinyume cha Katiba ya nchi?