Stan Mashamba
JF-Expert Member
- Apr 22, 2020
- 3,183
- 2,479
Mh Lissu alisema tume ya uchaguzi imeandaa kura feki 12 million za Magufuli na kweli Magufuli alipata kura hizo hizo, huo haukuwa uchaguziKwa faida ya wana JF ungetutajia alichosema Tundu Lissu siku hiyo na kilichotokea siku ya uchaguzi
Mkuu Mapolisi si waliwapiga kuwaua na kuwajeruhi wengine kisa uchaguzi? Kwa mara ya kwanza watashuhudia serikali walioipigania ikishindwa kuwalipa Watumishi wake mishahara kwa wakati.Hii si nchi tajiri haihitaji hela yoyote.
Itakuwa jambo jema snMkuu Mapolisi si waliwapiga kuwaua na kuwajeruhi wengine kisa uchaguzi?? Kwa mara ya kwanza watashuhudia serikali walioipigania ikishindwa kuwalipa Watumishi wake mishahara kwa wakati.
Vikwazo siyo njia hata siku moja, waambie viongozi wa upinzani wajipange vizuri kwa ajili ya 2025 kuliko kuota kuwa kuwa kuna shortcut ya kutoka mataifa ya nje.Mimi binafsi sifirahii hali hii ya kueekewa vikwazo, kwa kuwa ninajua kitatuathiri watu wa kawaida kama mimi na wewe kuliko watawala wetu, lakini kwa kiburi hiki cha Jiwe, unadhani kuna njia nyingine inayoweza kutumika kuirejesha nchi yetu kwenye mfumo Wa kidemokrasia unaotambulika kimataifa?
Halafu eti ndiye kinara wa kupambana na wanaofoji vyeti! Lakini pia wanasema ukimuona mtu msibani analia sana kuonyesha kuguswa na msiba ule basi ujue ndiye mchawi.Ni bora huyo Jiwe apewe adhabu kali, yani kwenye uchaguzi mkuu unaleta kura feki na kura za wananchi hazihesabiwi!!
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Nadhani shupavu wapo, kwa staili anayoitumia Magufuli ya KUUA, lazima kubadili mbinu ikibidi kwenda nje kwa wanaokuunga mkono! Lissu and Lema are the right person in the right directon! Ngoja wakimbie kuuawa, then tokea huko matokeao yapo njianiUmeongea vyema, Nimekuja kugundua kwambaTanzania hakuna watu/mtu shupavu. Shupavu tuliowategemea wameonyesha taswira tofauti kabisa.
Sasa unashauri nini kifanyike kwa hichi Magufuli anachoifanya hii nchi usiishie tu kusema hivyo unavyosemaKuna nyimbo nyingine kama huu zinatokana na kutoelewa mambo tu. Kwa mfano ikitokea nchi ikawekewa vikwazo vya uchumi unadhani utafaidika nini; au kwa lugha rahisi sana unadhani ni nani atakayeumia zaidi. Unadhani vikwazo vitamkomoa Magufuli na CCM lakini inabidi ufikiri mara mbili zaidi kabla ya kuombea hilo.
Zimbabwe ilikuwa na vikwazo vya uchumi kwa muda wa karibu miaka 17 chini ya Mugabe, je yeye pamoja watu wake waliwahi kushindwa kwenda kutembea au kutibiwa Singapore au watoto wao kwenda kusoma Hongkong ? Baada ya Mugabe kuondoka madarakani, je unaamini kuwa uharibufu uliotokana na na vikwazo hivyo umekwisha na kweli watu wa Zimbabwe wanafaidika na maisha tena?
Iraq ilikuwa na vikwazo chini ya Saddam, lakini wakati wote wa vikwazo Saddama na watu wake walikuwa wakiishi vizuri tu isipokuwa raia wa kawaida, na leo takriban miaka ishirini tangu Saddam angolewe, je unadhani kweli madhara ya vikwazo vile yamekwisha na watu wanaishi maisha mazuri tena?
Kuamini kuwa "utakombolewa" na mataifa ya kigeni kwa kumkomoa magufuli na CCM ni ndoto isyosaidia lolote. Upinzani ulikosea kuamini kuwa kutangaza chuki dhi ya magufuli ndiyo sera, wakasahahu kujenga mashina . wao walichukulia kuwa siasa ni maandamao na mikutano ya hadhara tu. Halafu eti leo wanalilia mataifa ya nje.
Kwa kifupi, hayo yanayosemwa na mataifa ya nje yanaisha vivyo hivyo; ndiyo maana bado uliwaona mabalazi wote wa nchi hizo za magharibi waliokuwa wametoa matamko wakihudhuria tukio la kuapishwa kwa magufuli tena.
Mtu kama wewe ulienda shule kweli? CUF wana wabunge 3,Act wazalendo 4, Chadema mtu 1 hawatoshi kuwa wenyeviti wa hizo kamati?Nchi yetu iko katika mfumo wa vyama vingi kama inavyobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1)
Kwa Bahati mbaya sana, ingawa Katiba ya nchi inatamka hivyo, watawala wetu wanaonekana kabisa ni watu wasioutaka kabisa mfumo wa vyama vingi na wanatulazimisha watanzania wote turejee kwenye mfumo Wa Chama kimoja cha CCM.
Ushahidi wa wazi ni namna uchaguzi mkuu uliopita ulivyoendeshwa, hadi kutolewa matokeo ya mwisho, ambayo yamempa ushindi Wa asilimia zaidi ya 84, mgombea wake John Pombe Magufuli na kujizolea viti 262 vya ubunge kati ya viti 264!
Sasa kazi ipo katika uundwaji wa Kamati za Bunge, ambapo inatakiwa:-
1. Kamati za hesabu za serikali (PAC)
2. Kamati ya mashirika ya Umma (POAC)
3. Kamati ya serikali za mitaa (LAAC) ni "lazima" ziongozwe na wabunge wa upinzani.
Swali kubwa wanalojiuliza watawala je watawapataje wabunge hao wa upinzani wakati wnyewe ndiyo "waliouvuruga" uchaguzi huo hadi kutopatikana kabisa wabunge hao wa upinzani?
Nimesikia fununu kuwa wafadhili mbalimbali, ambao ndiyo huwa wanatufadhili kwa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi trilioni 2 kila mwaka "wanakomalia" kuwa ni lazima sharti hilo litimizwe ndipo walete hayo mapesa yao.
Tumesikia kauli zilizotolewa na washirika mbalimbali wakiwemo Umoja wa mataifa, Ubalozi wa Matekani, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Japan na Jumuiya ya nchi za Ulaya za kutotaka kuutambua uchaguzi huu uliopita kuwa haukuwa na viwango vya kuitwa ni uchaguzi uliokuwa Huru na Haki.
Je, nchi yetu ambayo imegeuka kuwa ombaomba, japo "inajimwambafai" kuwa inaweza kuwa "donor country" itaweza kumudu kuendesha shughuli zake bila kuwategemea hao wafadhili?
Swali muhimu ambalo tunapaswa tujiulize wananchi wote Wa nchi hii, je nchi yetu itakuwa imefuata njia iliyopitia Zimbabwe kwa kuyafanya maisha ya kila Mtanzania kuwa magumu mno kutokana na kiburi cha watawala wetu wa kutaka mfumo wa chama kimoja ambapo ni kinyume cha Katiba ya nchi?
Kumbuka ule mkopo was benk ya dunia ambao ulilazimika kusubiri baada ya Zzk kusema huko ughaibuniUko sahihi, lkn lazima kuwe na MTU shupavu wa kuyasemea.
nakubaliana na weweKumbuka ule mkopo was benk ya dunia ambao ulilazimika kusubiri baada ya Zzk kusema huko ughaibuni
Tusiwadharau Hawa ndg wanaweza kutunyuma usingizi wakikaza
Kuna mtu anatuaminisha nchi inaweza kusonga bila wahisani na benki ya dunia.Tupate kwanza kibano,ili akili itukae sawa. Hii miaka 5, waone athari za wizi wa kura.