Kuendelea kuwekewa "mbinyo" na Jumuiya ya kimataifa, ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kuiokoa nchi yetu katika anguko la kidemokrasia

Kuendelea kuwekewa "mbinyo" na Jumuiya ya kimataifa, ndiyo njia pekee iliyobaki inayoweza kuiokoa nchi yetu katika anguko la kidemokrasia

Kwa faida ya wana JF ungetutajia alichosema Tundu Lissu siku hiyo na kilichotokea siku ya uchaguzi
Mh Lissu alisema tume ya uchaguzi imeandaa kura feki 12 million za Magufuli na kweli Magufuli alipata kura hizo hizo, huo haukuwa uchaguzi
 
Kuna nyimbo nyingine kama huu zinatokana na kutoelewa mambo tu. Kwa mfano ikitokea nchi ikawekewa vikwazo vya uchumi unadhani utafaidika nini; au kwa lugha rahisi sana unadhani ni nani atakayeumia zaidi. Unadhani vikwazo vitamkomoa Magufuli na CCM lakini inabidi ufikiri mara mbili zaidi kabla ya kuombea hilo.

Zimbabwe ilikuwa na vikwazo vya uchumi kwa muda wa karibu miaka 17 chini ya Mugabe; je yeye pamoja watu wake waliwahi kushindwa kwenda kutembea au kutibiwa Singapore au watoto wao kwenda kusoma Hongkong ? Baada ya Mugabe kuondoka madarakani, je unaamini kuwa uharibifu uliotokana na na vikwazo hivyo umekwisha na kweli watu wa Zimbabwe wanafaidika na maisha tena?

Iraq ilikuwa na vikwazo chini ya Saddam, lakini wakati wote wa vikwazo Saddam na watu wake walikuwa wakiishi vizuri tu isipokuwa raia wa kawaida, na leo ni takriban miaka ishirini tangu Saddam ang'olewe, je unadhani kweli madhara ya vikwazo vile yamekwisha na watu wanaishi maisha mazuri tena?

Kuamini kuwa "utakombolewa" na mataifa ya kigeni kwa kumkomoa magufuli na CCM ni ndoto isiyosaidia lolote. Upinzani ulikosea kuamini kuwa kutangaza chuki dhidi ya magufuli ndiyo sera, wakasahau kujenga mashina . wao walichukulia kuwa siasa ni maandamano na mikutano ya hadhara tu. Halafu eti leo wanalilia mataifa ya nje yaje yawasaidie. Utawala wa demokrasi unatokana na sanduku la kura; kila mtu anayelelamika hapa kudai uchaguzi siyo halali kwa sabu alishindwa kwenye boksi la kura siyo mwanademkrasia huyo.

Kwa kifupi, hayo yanayosemwa na mataifa ya nje yanaisha vivyo hivyo; ndiyo maana bado uliwaona mabalazi wote wa nchi hizo za magharibi waliokuwa wametoa matamko wakihudhuria tukio la kuapishwa kwa magufuli tena.
 
Katika nchi ambayo uundwaji wa Tume ya uchaguzi ni Wa hovyo kabisa, kwa kuwa anaachiwa mgombea wa CCM nfiye ateue makamishna wote naye ameteua makada wakubwa wa CCM. Refer Dkt Mahera

Katika nchi ambayo tunaambiwa matokeo ya Urais yakishatangazwa na Tume ya uchaguzi, hakuna chombo chochote cha sheria kitakachohoji matokeo hayo!

Hapo hapo viongozi wa uojnzani wanapoitisha naandamano ya amani, Polisi wanayazuia maanfamano hayo na kuwafungulia mashitaka ya kubambika ya ugaidi kwa viongozi hao!

Katika nchi ambayo kamanda Wa Polisi Wa Hai anatamkia hadharani mgombea Wa Chadema, Freman Mbowe, kuwa uchaguzi huu hawezi kumshinda mgombea wa CCM!

Hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kwa vitendo hivyo vya huyo kamanda wa Polisi wa wilaya kwa kuvunja viapo vya kazi take, ambavyo vinamtaka asishabikie chama cjochote cha siasa!

Hivi katika nchi ya aina hiyo, huoni kama vikwazo kutoka kwenye nchi wahisani ndiyo njia pekee iliyobaki ya kurejesha mfumo Wa kidemokrasia nchini humo?
 
Mimi binafsi sifurahii hali hii ya kuwekewa vikwazo, kwa kuwa ninajua itatuathiri watu wa kawaida kama mimi na wewe kuliko watawala wetu, lakini kwa kiburi hiki cha Jiwe, unadhani kuna njia nyingine inayoweza kutumika kuirejesha nchi yetu kwenye mfumo Wa kidemokrasia unaotambulika kimataifa?
 
Hii si nchi tajiri haihitaji hela yoyote.
Mkuu Mapolisi si waliwapiga kuwaua na kuwajeruhi wengine kisa uchaguzi? Kwa mara ya kwanza watashuhudia serikali walioipigania ikishindwa kuwalipa Watumishi wake mishahara kwa wakati.
 
Mimi binafsi sifirahii hali hii ya kueekewa vikwazo, kwa kuwa ninajua kitatuathiri watu wa kawaida kama mimi na wewe kuliko watawala wetu, lakini kwa kiburi hiki cha Jiwe, unadhani kuna njia nyingine inayoweza kutumika kuirejesha nchi yetu kwenye mfumo Wa kidemokrasia unaotambulika kimataifa?
Vikwazo siyo njia hata siku moja, waambie viongozi wa upinzani wajipange vizuri kwa ajili ya 2025 kuliko kuota kuwa kuwa kuna shortcut ya kutoka mataifa ya nje.

Usidhani kuwa kweli mataifa ya nje yanamchukuia Magufuli kama unvyoamini; Lissu ni mhamiaji wa Ubelgiji, wala makelele yake pamoja na Masterdama wake yabadili chochote kuhusu uhusiano wa Tanzania na nchi za nje. Kuna watu kadhaa waliokuwa wanahusiana na biashara za madini ambazo zilivurugwa na magufuli wamekuwa washinikiza maseneta kadhaa Marekani walioko kwenye kamati ya mambo ya nje kuiwekea pressure serikali ya Tanzania, lakini mambo yote hubakia hapo tu, yaani matamko tu.
 
Ni bora huyo Jiwe apewe adhabu kali, yani kwenye uchaguzi mkuu unaleta kura feki na kura za wananchi hazihesabiwi!!
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Halafu eti ndiye kinara wa kupambana na wanaofoji vyeti! Lakini pia wanasema ukimuona mtu msibani analia sana kuonyesha kuguswa na msiba ule basi ujue ndiye mchawi.
 
Umeongea vyema, Nimekuja kugundua kwambaTanzania hakuna watu/mtu shupavu. Shupavu tuliowategemea wameonyesha taswira tofauti kabisa.
Nadhani shupavu wapo, kwa staili anayoitumia Magufuli ya KUUA, lazima kubadili mbinu ikibidi kwenda nje kwa wanaokuunga mkono! Lissu and Lema are the right person in the right directon! Ngoja wakimbie kuuawa, then tokea huko matokeao yapo njiani
 
Kuna nyimbo nyingine kama huu zinatokana na kutoelewa mambo tu. Kwa mfano ikitokea nchi ikawekewa vikwazo vya uchumi unadhani utafaidika nini; au kwa lugha rahisi sana unadhani ni nani atakayeumia zaidi. Unadhani vikwazo vitamkomoa Magufuli na CCM lakini inabidi ufikiri mara mbili zaidi kabla ya kuombea hilo.

Zimbabwe ilikuwa na vikwazo vya uchumi kwa muda wa karibu miaka 17 chini ya Mugabe, je yeye pamoja watu wake waliwahi kushindwa kwenda kutembea au kutibiwa Singapore au watoto wao kwenda kusoma Hongkong ? Baada ya Mugabe kuondoka madarakani, je unaamini kuwa uharibufu uliotokana na na vikwazo hivyo umekwisha na kweli watu wa Zimbabwe wanafaidika na maisha tena?

Iraq ilikuwa na vikwazo chini ya Saddam, lakini wakati wote wa vikwazo Saddama na watu wake walikuwa wakiishi vizuri tu isipokuwa raia wa kawaida, na leo takriban miaka ishirini tangu Saddam angolewe, je unadhani kweli madhara ya vikwazo vile yamekwisha na watu wanaishi maisha mazuri tena?

Kuamini kuwa "utakombolewa" na mataifa ya kigeni kwa kumkomoa magufuli na CCM ni ndoto isyosaidia lolote. Upinzani ulikosea kuamini kuwa kutangaza chuki dhi ya magufuli ndiyo sera, wakasahahu kujenga mashina . wao walichukulia kuwa siasa ni maandamao na mikutano ya hadhara tu. Halafu eti leo wanalilia mataifa ya nje.

Kwa kifupi, hayo yanayosemwa na mataifa ya nje yanaisha vivyo hivyo; ndiyo maana bado uliwaona mabalazi wote wa nchi hizo za magharibi waliokuwa wametoa matamko wakihudhuria tukio la kuapishwa kwa magufuli tena.
Sasa unashauri nini kifanyike kwa hichi Magufuli anachoifanya hii nchi usiishie tu kusema hivyo unavyosema

Kwa sababu lengo hapo ni hilo hao wananchi walimie meno sawasawa yani waishi maisha magumu kwelikweli
Ili baadae watambue umuhimu wa juhudi wanazofanya wenye uchungu na hii nchi siyo kwa faida binafsi na ingekuwa kwa faida binafsi mtu kama Lisu angehamia tu ccm na aanze kula mishahara mirefu kwanini anapata shida kiasi hicho ni kwa sababu tu ya uzalendo hakuna kingine

Raia wakisulubika vizuri wakosoaji wataongezeka na wengi watakuwa tayari kwa lolote baada ya kuchoka kwa ugumu wa maisha kutokana na serikali kuwabana sana wananchi ili iweze kupata mapato yake kuendesha nchi baada ya misaada ya nje kukatwa raia watarudi nyuma kimaendeleo badala ya kwenda mbele na matokeo yake watapinga ujinga huu kwa umoja sana na nguvu ya umma itashinda na lengo litakuwa limetimia
 
Huo mbinyo ndio utaleta maendeleo ? Atakayeumia ni mtanzania wa kawaida kabisa, sio wanasiasa.
 
Inauma sana Tanzania nchi ya heshima kubwa duniani kuheshimu haki za binadamu na demokrasia kufika hatua ya kudharaulika namna hii kweli??? Hapana hapana

Mwalimu angekuwepo asingekubali ...mambo ya kihuni kama haya!!
 
Nchi yetu iko katika mfumo wa vyama vingi kama inavyobainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1)

Kwa Bahati mbaya sana, ingawa Katiba ya nchi inatamka hivyo, watawala wetu wanaonekana kabisa ni watu wasioutaka kabisa mfumo wa vyama vingi na wanatulazimisha watanzania wote turejee kwenye mfumo Wa Chama kimoja cha CCM.

Ushahidi wa wazi ni namna uchaguzi mkuu uliopita ulivyoendeshwa, hadi kutolewa matokeo ya mwisho, ambayo yamempa ushindi Wa asilimia zaidi ya 84, mgombea wake John Pombe Magufuli na kujizolea viti 262 vya ubunge kati ya viti 264!

Sasa kazi ipo katika uundwaji wa Kamati za Bunge, ambapo inatakiwa:-

1. Kamati za hesabu za serikali (PAC)
2. Kamati ya mashirika ya Umma (POAC)
3. Kamati ya serikali za mitaa (LAAC) ni "lazima" ziongozwe na wabunge wa upinzani.

Swali kubwa wanalojiuliza watawala je watawapataje wabunge hao wa upinzani wakati wnyewe ndiyo "waliouvuruga" uchaguzi huo hadi kutopatikana kabisa wabunge hao wa upinzani?

Nimesikia fununu kuwa wafadhili mbalimbali, ambao ndiyo huwa wanatufadhili kwa kiasi kinachokadiriwa cha shilingi trilioni 2 kila mwaka "wanakomalia" kuwa ni lazima sharti hilo litimizwe ndipo walete hayo mapesa yao.

Tumesikia kauli zilizotolewa na washirika mbalimbali wakiwemo Umoja wa mataifa, Ubalozi wa Matekani, Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Japan na Jumuiya ya nchi za Ulaya za kutotaka kuutambua uchaguzi huu uliopita kuwa haukuwa na viwango vya kuitwa ni uchaguzi uliokuwa Huru na Haki.

Je, nchi yetu ambayo imegeuka kuwa ombaomba, japo "inajimwambafai" kuwa inaweza kuwa "donor country" itaweza kumudu kuendesha shughuli zake bila kuwategemea hao wafadhili?

Swali muhimu ambalo tunapaswa tujiulize wananchi wote Wa nchi hii, je nchi yetu itakuwa imefuata njia iliyopitia Zimbabwe kwa kuyafanya maisha ya kila Mtanzania kuwa magumu mno kutokana na kiburi cha watawala wetu wa kutaka mfumo wa chama kimoja ambapo ni kinyume cha Katiba ya nchi?
Mtu kama wewe ulienda shule kweli? CUF wana wabunge 3,Act wazalendo 4, Chadema mtu 1 hawatoshi kuwa wenyeviti wa hizo kamati?
 
Inaandaliwa list ya wabunge wa ccm ambao watavalishwa jina la wapinzan, NEC inahusika hapa.
 
Nanusa tu kwamba huenda IGP wetu akaangushiwa jumba bovu.....

.
 
Back
Top Bottom