Kuendesha biashara yako mwenyewe ni kazi ngumu sana

Kuendesha biashara yako mwenyewe ni kazi ngumu sana

wasalaamu wadau,, nimekuwa kila nikianzisha biashara sitoboi kabisa,..kwa mfano nilikuwa namiliki saloon yangu ya kiume lakini cha ajabu sipati wateja,..yaani unaweza kukaa kutwa nzima ukaambulia vichwa viwili tu,,,siku nikipata wengi ni watatu mwisho,.. vivyo hivyo hata biashara zingine nilizowahi kuanzisha kama vile kuuza nguo na mahindi,...je mimi nakosea wapi wadau? au wengine huwa munafanyeje? karibuni kwa ushauri maana hapa nahisi kushindwa,. sijui bora kuajiliwa tu,..daah
Location vipi?
Make location inabeba vitu ving sana kwa wakati mmoja.
1.İdadi ya Saloon eneo husika
2. Maisha ya watu wa eneo husika
3. Population ya eneo husika
4. Accessibility ya hio Saloon.
Hayo pia yanakuja kudetermine price

Na mengine mengi kama Management
 
Mkuu komaa usikate tamaa. Mimi ninapofanyia biashara frame ya pembeni yangu alifungua mtu biashara kama yangu, kodi ilivyoisha akafunga biashara. Same fremu kafungua mwingine nae anasema akimaliza kodi harudi.

Kama sio kukomaa ningeshafunga biashara kitambo kabisa. Imagine wenzio wanakuja wanakata tamaa ila sio kwamba kuna siku sikosi. Nakosa lakini naamini kwenye kupata na kukosa kwamba sio kila siku nitapata tu.

Komaa mkuu. Biashara inayoanza ngumu sana. Nina mwaka now ila bado naona kama nimeanza jana biashara ila sikati tamaa kuona haikua kama nilivyodhani itakua ndani ya muda niliodhani mimi biashara itakua.

Nina rafiki yangu anabiashara ya mihogo. Anasema yeye ilimchukua miaka mitatu kusimama vizuri.

Mimi nikiwaza ndo kwanza mwaka nasema bado nina muda wa kusimama vizuri

Safi sanaa ongeza juhudii
Unakuta pia mtu anachukua frame anakuwa anafungua mara moja moja hawi active wateja wanakupotezea
 
Safi sanaa ongeza juhudii
Unakuta pia mtu anachukua frame anakuwa anafungua mara moja moja hawi active wateja wanakupotezea
Yes. Inapoteza wateja pia hii sababu hawana uhakika na huduma yako
 
wasalaamu wadau,, nimekuwa kila nikianzisha biashara sitoboi kabisa,..kwa mfano nilikuwa namiliki saloon yangu ya kiume lakini cha ajabu sipati wateja,..yaani unaweza kukaa kutwa nzima ukaambulia vichwa viwili tu,,,siku nikipata wengi ni watatu mwisho,.. vivyo hivyo hata biashara zingine nilizowahi kuanzisha kama vile kuuza nguo na mahindi,...je mimi nakosea wapi wadau? au wengine huwa munafanyeje? karibuni kwa ushauri maana hapa nahisi kushindwa,. sijui bora kuajiliwa tu,..daah

Mkuu, ofisi yako inamuda gani ??
 
1.Eneo unalofanyia
2.Wateja wako watakua wa namna gani
3.Mazingira yako ya biashara(usafi,ubora wa vifaa nk)
4.Huduma iliyopo inatolewaje(kinyozi anajua kunyoa vyema inavyotakiwa mtu akaridhika..mimi naishi eneo A lakini lazima nikanyoe eneo E kutokana na huyo kinyozi kua noma)
5.Bei ikoje inaendana na mahitaji ya sasa
6.uvumilivu
7.Jitahidi uwe una sali mara kwa mara

Hayo ninayoyafahamu mimi
 
wasalaamu wadau,, nimekuwa kila nikianzisha biashara sitoboi kabisa,..kwa mfano nilikuwa namiliki saloon yangu ya kiume lakini cha ajabu sipati wateja,..yaani unaweza kukaa kutwa nzima ukaambulia vichwa viwili tu,,,siku nikipata wengi ni watatu mwisho,.. vivyo hivyo hata biashara zingine nilizowahi kuanzisha kama vile kuuza nguo na mahindi,...je mimi nakosea wapi wadau? au wengine huwa munafanyeje? karibuni kwa ushauri maana hapa nahisi kushindwa,. sijui bora kuajiliwa tu,..daah
ww una nyota ya mteja..!🤣
 
Mkuu sina cha kuongeza Saloon ninayonyoa mimi ina mazingira mazuri ila vilivyobaki vyote ni kama hivyo yule jamaa anatumia hadi nusu saa kuninyoa tu aisee
BIASHARA ya salon.....
Mambo ya msingi ya kuzingatia
Kama upo uswahilini....usiirembe Sana salon yako...wabongo wakiona umeremba Sanaa wanakimbia kwa kujua bei ni kubwa.

Shusha bei,kama wenzio wananyoa buku jero,wewe nyoa buku,

Wahi kufungua...... Chelewa kufunga.

Customer care nu muhimu....

Kinyozi akimyoa MTU asimuondoe haraka haraka,labda kuwe na vichwa nje....mteja akimaa mda mtefu akinyolewa ndio anaamini kuwa jamaa amenyoa vizuri...Ila faster faster anahisi amelipuliwa

Kinyozi awe na uongo Fulani wenye faida, mfano kuna Saloni moja hivii,kila MTU akimyoa utamkuta anasema" hivi nywele zako kwa jinsi zilivyo angekuwa kinyozi wasiwasi...lazima akunyoe vibaya....maana kinasehemu zimekaa vibaya ...inamaana anamuaminisha kuwa yeye ndio Bora ,hivyo asiende kwingine.....kumbe anamjazaa tuu.

Piaa kinyozi awe mpiga Stori Sanaa na watejaa,mteja akija anapiga stor Sana za siasa na zinginee,basi jamaa anajikuta kesho analud hapo hapoo.

Piaa kinyozi MTU akija kunyoa basi amnyoe na ndevu kwa pesa yake ile ile.

Huu ndio ushauri wangu.....japo napata kvant hapa,Sasa siajua NI ushaur wangu au NI akiri za kvant.
 
Yes. Inapoteza wateja pia hii sababu hawana uhakika na huduma yako
We angalia wamiliki wa makampuni hawataki hata siku moja kufunga yaan wanataman hata jumapili wafungue biashara watu wafanye kazi
 
Mchawi ni location akisindikizwa na rafki yake ajulikanaye kama ubora wa huduma unazotoa , narudia tena mchawi ni location.....ukikosea location wafaaaaaaaaaaa no mercy and no compromise....!!! Yaan hyo factor inastand alone haihtaji mbwembwe za kusali ama kuroga ......

habari ya location labda zinatofautiana mkuu,..kwa kweli mimi nipo sehemu iliyochangamka kweli na si kwamba nipo peke yangu la hasha, kuna wenzangu lakini naona tunatofautiana wenzangu wenyewe ni afadhali wanapata vichwa sijui wana marafiki wengi,..
 
Tafuta frem zilizopo kwenye kona inayopita watu wengi, usilipie frem iliyoko uchocho...bora umwage yebo yebo huko barabarani maana hakuna gharama za uendeshaji
 
1.Jitahid kuwa creative.

2.Usianzishe biashara jirani na mtu anayefanya biashara hiyo hivyo toka zamani.

3. Usianzishe biashara ukitegemea jirani zako, ndugu zako, na marafiki ndyo watakuwa wateja. Hasa za duka.

4. Usianzishe biashara ukitegemea kuanza kupata faida ndani ya mwaka 1.

5. Ukianzisha biashara tafta ushaur kwa waliofanikiwa, sio walioshindwa.

6. Biashara yoyote inahitaji uvumilivu na Muda.
 
Factor nyingine kwenye saloon ni ujuzi (mastering) na kujali mteja , yaan mteja awe kama mtoto wako , mashine isiwe zile za kuumiza na kupiga makelele ,mkuu ukiweza hvyo vitu wateja utawakimbia .....
 
Back
Top Bottom