Kuendesha biashara yako mwenyewe ni kazi ngumu sana

Endelea kupambana usikate tamaa.
Kuwa mbunifu, pia sio mbaya ukaongeza huduma nyingine ambayo haitoathiri shughuli za unyoaji.
 
Kwanza sehemu ya kufanyia biashara pia UBORA wa huduma, tatu usilazimishe faida kubwa


Ucheshi kwa wateja na mbinu za kuwaweka kuwa wakudumu
 
Fanya SWOT analysis ikusaidie kujua unakwama wapi. Kama huwezi tafuta mtu anayefahamu akuongoze. Bila hii utakuwa unakomaa kama ntu anayekomaa chumba chenye giza akimsaka paka mweusi ambaye hayupo!
 
Mkuu fanya hivi

Jitafakari kwa kina sana(mf. Wewe ni nani unamadhaifu yapi unanguvu gani).

Njoo jiangalie ni wapi unafanya vizuri ufanyapo jambo mpka watu wanasema yes. Iangalie familia yako/yenu (baba mama dada kaka wadogo zako wajomba baba wakubwa kwa wadogo mama wakubwa kwa wadogo shangazi) wamefanikiwa kwenye upande upi? KUAJIRIWA AU KUJIAJIRI? Utapata jibu. Amini sio kila mtu ni wa biashara sio kila mtu wa kujiajiri na kinyumeche.

NYONGEZA;
Usisukumwe na peer pressure usione umri unasogea bila mafanikio usione marika wamefanikiwa nawe haufanikiwi haya huwaongoza vijana wengi kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Nikuambie tu kuna mahusiano madooooogo sana kati ya UMRI & MAFANIKIO.

Kila la kheri mkuu
 
Nmekusoma mkuu, uko sawa kabisa.!
 
Usikate tamaaa...watu wengi wanapitia kama hali yako......Fanya tathimini kama wakuu wanavyokushauri huko juu...Muombe mungu sana pia...
 
Vitu ninavyozingatia kama mteja kwanza ni usafi wa salon yenyewe, sterilizer, ubora wa mashine, after shelv liquor, uwezo wa kinyozi. Nikipata hivyo vyote basi huwa
Nanyoa salon moja, kinyozi yule yule na kama anamyoa mtu mwingine nitamsubiri amalize na kama hayupo nipo radhi niahirishe. Nikikaa kwenye kiti sina haja ya kumuelekeza nanyoaje ni story mwanzo mwisho yani anaanza mtoto huyu, yule wa pale unamuonaje bro aah yule fresh.. poa bro nakusawazishia au yule ni grid au kama kuna pisi naielewa nampa kazi kwakweli hawajawahi kuniangusha.
Kutokana na mazoea haya akihama salon huwa wananiambia bro nimehamia mahali fulani na mimi nawafuata huko kuwaunga mkono. Soma kwa makini nilichokiandika
 
Location, convicing power
 
Utafiti ...Mtaji.... Location....Bidhaa....Bei... customer care....hapo wewe ni kupiga pesa tu.
 
Nakazia hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…