Kuendesha gari na sandles kwa traffic ni kosa?

Kuendesha gari na sandles kwa traffic ni kosa?

Wakuu salama za sikukuu.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.

Nimetoka zangu gereji naingia tu. Main road hapa maeneo ya mianzini. Nikasimamishwa na traffic. Kaanza na mambo yambo yake, naomba leseni yako, nikampatia. Akanibambikia makosa yake kaanza eti naongea na simu nikalichomoa,
kubwa kuliko akaniambia naendesha nikiwa nimevaa sandles (nimevaa viatu vyisivyo na kamba ya nyuma).
kanikomalia hapo, afu hapo faini ya 30 sina.
Nikabembeleza balaa.

Jamani naomba kuuliza eti ni kosa kuendesha gari ukiwa umevaa sandles.

Wenye ujuzi wa makosa ya barabarani. Hili nalo lipo kwenye list.
Sina hakika kama ni kosa, maana katika zile Basic Traffic Offences, ambazo zipo 20, hakuna kipengele kinachotaja aina ya viatu anavyopaswa dereva avivae.
 
Ni kosa mkuu, ila ni rahisi sana kulikwepa, mm huwa naendesha sana na sandals, cha kumwambia ni kwamba unaendesha peku, ila unazivaa ukiwa unashuka
 
Back
Top Bottom