Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Mkuu, kuna watu ambao wanapaswa kulazimishiwa kufanya mambo ya msingi. Usipowalazimisha huwa hawafanyi. Mfano kuna mahali usipoweka matuta wenye magari wanagonga watembea kwa miguuu, so tuache atakaye asimame asiye taka atembee?

Tatizo ni kwamba kuna vitu hata kama ni vizuri, ukivifanya peke yako havitatatua tatizo la msingi, ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mkono, masuala ya namna hiyo yanahitaji maamuzi ya kisera na kila mtu awajibike kufuata sera.
 
Mkuu, unafikiri kuamua kutonunua maji kukwepa kutoa Sh. 20 kusaidia mlemavu au mtoto yatima, hilo ni suala la umasikini na utajiri, au ni suala la roho mbaya?

Na kama wewe una hali mbaya kiasi kutoa 20shilingi ni ishu hivyo na una akili timamu, afya na.k vipi mlemavu au mtoto yatima alietelekezwa?
 
macho_mdiliko ili uwe kwenye nafasi nzuri kuelewa hoja yangu. Assume wewe ndio yatima/ mlemavu ambao kwa ulemavu ulio nao huwezi kufanya kazi na kuzalisha chochote na ndugu wamekutosa. Unaishi mtaani kwa kuombaomba na kulala Chini ya madaraja

Halafu wahanga wa leo wao ni wazima ila wanalalamika kipato chao kidogo, halafu hoja hii ije mezani, mtizamo wako ungekuwa ni nini?

Hapo ndio unaweza kuliona suala hili kwa jicho sahihi.
 
Punguza hizo fedha mnazowalipa wabunge ili kuwanususru hao wenye mahitaji maalum!! Tatizo letu liko kwenye resource allocation.
 
Punguza hizo fedha mnazowalipa wabunge ili kuwanususru hao wenye mahitaji maalum!! Tatizo letu liko kwenye resource allocation.
Mkuu hili linaweza kuwa moja ya suluhisho, lakini kitu nisichokubali mimi ni utaratibu wa kila mtu kuhisi mwenzake ndio mwenye wajibu halafu yeye ana haki tu,hilo ni tatizo kubwa. Yaani inapokuja suala la kuhurumiwa kila mtu anadhani yeye ndio anapaswa kuhurumiwa. Linapokuja suala la kupokea kila mtu hudhani yeye ndio hupaswa kipokea. Linapokuja suala la kutoa,kila mtu hudhani mwenzake ndio hupaswa kutoa ni.k hii ni mbaya sana.

Kutatua tatizo la namna hii kwenye mada hii lazima kila mtu achangie/akatwe ki dizaini fulani.
 
Walazamishe wabunge watoe!
Wabunge 309 wakikatwa Kodi kwenye package Yao hata kama ni 15% Tu itatosheleza kabisa kusaidia hao watu wako! Na kile kiinua mgongo cha hao wabunge cha 200+M wakikatwa Kodi 15%, watakuwa wamechanja zaidi!

Siyo ulazimishe watu tuliopigika tutoe! Kwa kutuletea tozo! Za kwenye soda na juice zinatosha!
 
Waanze kuchangia hao wabunge!
Ndiyo mje kwa wananchi!

Anzeni na mawazo ya wabunge kuchangia pato la taifa! Kupitia Kodi za mishahara yao.
 
Tunaiona dunia vile tulivyo.

Haiwezekani mtu aandike kitu, wewe mwenyewe ukiri kuwa ni cha ki 'utopia' halafu hapohapo umushutumu kwa 'ubinafsi wake'!!

Inaanza na wewe, ukishajiamini kuwa una roho nzuri au at least unaweza kuwa na roho nzuri ndio unaweza kuziona na roho nzuri zilizozagaa mitaani.

Ukiona huwezi kuamini mtu, jua kwamba na we umeshindwa kujiamini na ni matokeo ya ukoloni, matokeo ya kutoukataa ukoloni uliokuja na mbinu ya kutengeneza mistrust baina ya watu ili watawalike wasiungane
 
Watu wangu tena? hahahahah! Mkuu yaani unaona uchungu sana kuchangia sh. 20 kwa kununua maji ya chupa kwa ajili ya kuchangia mlemavu au mtoto yatima? Kweli? Yaani hata ungekatwa 100, badala ya kununua maji 400 ununue 500 unadhani itakuathiri kihivyo? Halafu kama huna hela kabisa unabeba maji yako.

Naona unekoma na wabunge tu. Kuna mwingine kakomaa na walevi. Walevi nao wakiibuka watakomaa na wanywa soda. Hahahahah yaani mradi kukwepa wajibu tu. Mwisho wa siku unaweza kushangaa walevi ndio wanakubali kuchangia hahahahahah
 

Wananchi wanachangia kupitia KODI lukuki wanazolipa!! Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wanalipa kodi nyingi sana; tatizo sio watu kuchangia bali ni jinsi hiyo michango kupitia kodi inavyotumika!!!
 
Kwenye malipo ya umeme kuna tozo zisizo za lazima au zinazoweza kupunguzwa bila athari.
Hivyo basi tunaweza kupata thumni [senti 50] au shilingi 1:00 kwa kila uniti ya umeme.
Hapa namaanisha tusiongeze gharama bali pesa hizi zipatikane muno huko kwenye tozo/makato yaliyomo.
 
Hiyo ni kazi ya NGO's, wanaweza kuweka mabox kwenye kaunta za supermarket ambapo watu wanaweza kuweka chenji zinazobaki wakishalipia manunuzi, huko majuu inatumika sana hata kuchangia pesa za tafiti mbalimbali, mfano saratani za kina mama..........wale wahudumu pale kaunta za malipo wanakuwa wanawa alert wateja kama watachangia kwenye box ambalo linakuwa pembeni....
 
Mambo yetu tumeyamaliza?

Nikajua unawazungumzia wenye mahitaji maalumu wa Tanzania.
 
Wananchi wanachangia kupitia KODI lukuki wanazolipa!! Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wanalipa kodi nyingi sana; tatizo sio watu kuchangia bali ni jinsi hiyo michango kupitia kodi inavyotumika!!!
Mkuu suala la kukosena uadilifu na baadhi ya watu kutumia vibaya kodi za watu nakubaliana nawe kuwa ni tatizo lakini tunatakiwa kuendelea kupambana nalo huku tukifanya mambo ya msingi. Yaani hatuwezi kuacha mambo ya msingi kwa sababu ya wezi.

Ni sawa na kusema kwa kuwa kuna panya road basi tusimiliki mali ili wakose cha kuiba. Unadhani utakuwa uamuzi sahihi?
 
Good point ila bongo hawatachangia.halafu hela itakayochangwa kwa mfumo huo bongo haitakuwa na accountability kabisa, wataila walioweka maboksi.
 
Hapo sawa,kwa sababu tuna wizara ya makundi maalumu inahitaji pesa kuondoa watu ombaomba mitaani,walemavu,wagonjwa makubwa,wazee nk ..
Sahihi kabisa mkuu. Yaani ile ya kusema tu kuanzia kesho hatutaki mtu mtaani haiwezi kufanya kazi ispokuwa kama kuna namna ya kuwanusuru wahusika. Kuna watu wamekata tamaa mkuu, hawana matumaini yoyote, hata ukisema uwapeleke jela wala hata hawajitetei.
 
Hizo tozo watozwe hao wanaoruka sarakasi badala ya hoja na wanapata posho bila hiyana, tozo kibao lakini kinachofanyika hakionekani
 
Fedha itaishia kwa watu fulani tu
Hakuna chochote kitakChowafikia
Bongo as usual upigaj jadi yetu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…