Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Saidia wewe kama wewe kuepuka hiyo laana!
Msaada haulazimishwi. Unafikiri Baraka itatoka wapi Kwa hao so called wahitaji. Kama watoaji wana manung'uniko na malalamiko na mahangaiko mioyoni mwao!??

Umejaliwa toa wewe na jamaa zako. Watanzania niwaache kwanza, tumeshatoa vya kutosha, nimetoa laki 6 wamenikata ,elfu nane na ushee! Tozo my foot!
Mkuu, kuna watu ambao wanapaswa kulazimishiwa kufanya mambo ya msingi. Usipowalazimisha huwa hawafanyi. Mfano kuna mahali usipoweka matuta wenye magari wanagonga watembea kwa miguuu, so tuache atakaye asimame asiye taka atembee?

Tatizo ni kwamba kuna vitu hata kama ni vizuri, ukivifanya peke yako havitatatua tatizo la msingi, ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mkono, masuala ya namna hiyo yanahitaji maamuzi ya kisera na kila mtu awajibike kufuata sera.
 
Siku hizi umefanya nini unaandika utopia namna hii? Ni kutafuta ulaji au uko kwenye ulaji mpaka umevimbiwa? Wewe unadhani sh 20 kwa raia wa kawaida ni kitu kidogo? Ukiwa nazo wewe unadhani kila mtu naye anazo? Badala ya kusema serikali ipunguze matumizi ya anasa kama kusafiria bussiness class, kununua magari ya fahari, safari zisizo na lazima, idadi ya wabunge kubwa, kuwa na utitiri wa viongozi ngazi ya wilaya nk wewe unataka kukamua tena wananchi? Kweli waafrika tuna roho za kishetani zilizojaa ubinafsi!
Mkuu, unafikiri kuamua kutonunua maji kukwepa kutoa Sh. 20 kusaidia mlemavu au mtoto yatima, hilo ni suala la umasikini na utajiri, au ni suala la roho mbaya?

Na kama wewe una hali mbaya kiasi kutoa 20shilingi ni ishu hivyo na una akili timamu, afya na.k vipi mlemavu au mtoto yatima alietelekezwa?
 
macho_mdiliko ili uwe kwenye nafasi nzuri kuelewa hoja yangu. Assume wewe ndio yatima/ mlemavu ambao kwa ulemavu ulio nao huwezi kufanya kazi na kuzalisha chochote na ndugu wamekutosa. Unaishi mtaani kwa kuombaomba na kulala Chini ya madaraja

Halafu wahanga wa leo wao ni wazima ila wanalalamika kipato chao kidogo, halafu hoja hii ije mezani, mtizamo wako ungekuwa ni nini?

Hapo ndio unaweza kuliona suala hili kwa jicho sahihi.
 
Kama ukishindwa kunywa maji ya chupa, utakunywa ya bomba. Ni bora wewe unywe maji ya kudownload wenye mahitaji maalum nao wapate chakula na kulala ndani, kuliko unywe ya chupa wakati wenye mahitaji maalum wanalala kwenye mitaro na kula majalalani.

Wakati tunajadili bajeti ya Ustawi wa Jamii na Makundi maalum, hili ni muhimu sana.
Punguza hizo fedha mnazowalipa wabunge ili kuwanususru hao wenye mahitaji maalum!! Tatizo letu liko kwenye resource allocation.
 
Punguza hizo fedha mnazowalipa wabunge ili kuwanususru hao wenye mahitaji maalum!! Tatizo letu liko kwenye resource allocation.
Mkuu hili linaweza kuwa moja ya suluhisho, lakini kitu nisichokubali mimi ni utaratibu wa kila mtu kuhisi mwenzake ndio mwenye wajibu halafu yeye ana haki tu,hilo ni tatizo kubwa. Yaani inapokuja suala la kuhurumiwa kila mtu anadhani yeye ndio anapaswa kuhurumiwa. Linapokuja suala la kupokea kila mtu hudhani yeye ndio hupaswa kipokea. Linapokuja suala la kutoa,kila mtu hudhani mwenzake ndio hupaswa kutoa ni.k hii ni mbaya sana.

Kutatua tatizo la namna hii kwenye mada hii lazima kila mtu achangie/akatwe ki dizaini fulani.
 
Mkuu, kuna watu ambao wanapaswa kulazimishiwa kufanya mambo ya msingi. Usipowalazimisha huwa hawafanyi. Mfano kuna mahali usipoweka matuta wenye magari wanagonga watembea kwa miguuu, so tuache atakaye asimame asiye taka atembee?

Tatizo ni kwamba kuna vitu hata kama ni vizuri, ukivifanya peke yako havitatatua tatizo la msingi, ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mkono, masuala ya namna hiyo yanahitaji maamuzi ya kisera na kila mtu awajibike kufuata sera.
Walazamishe wabunge watoe!
Wabunge 309 wakikatwa Kodi kwenye package Yao hata kama ni 15% Tu itatosheleza kabisa kusaidia hao watu wako! Na kile kiinua mgongo cha hao wabunge cha 200+M wakikatwa Kodi 15%, watakuwa wamechanja zaidi!

Siyo ulazimishe watu tuliopigika tutoe! Kwa kutuletea tozo! Za kwenye soda na juice zinatosha!
 
Mkuu hili linaweza kuwa moja ya suluhisho, lakini kitu nisichokubali mimi ni utaratibu wa kila mtu kuhisi mwenzake ndio kwenye wajibu halafu yeye sana haki tu hilo ni tatizo kubwa. Yaani inapokuja suala la kuhurumiwa kila mtu anadhani yeye ndio anapaswa kuhurumiwa. Linapokuja suala la kupokea kila mtu hudhani yeye ndio hupaswa kipokea. Linapokuja suala la kubwa kila mtu hudhani mwenzake ndio hupaswa kutoa ni.k hii ni mbaya sana.

Kutatua tatizo la namna hii kwenye mada hii lazima kila mtu achangie/akatwe ki dizaini fulani.
Waanze kuchangia hao wabunge!
Ndiyo mje kwa wananchi!

Anzeni na mawazo ya wabunge kuchangia pato la taifa! Kupitia Kodi za mishahara yao.
 
Siku hizi umefanya nini unaandika utopia namna hii? Ni kutafuta ulaji au uko kwenye ulaji mpaka umevimbiwa? Wewe unadhani sh 20 kwa raia wa kawaida ni kitu kidogo? Ukiwa nazo wewe unadhani kila mtu naye anazo? Badala ya kusema serikali ipunguze matumizi ya anasa kama kusafiria bussiness class, kununua magari ya fahari, safari zisizo na lazima, idadi ya wabunge kubwa, kuwa na utitiri wa viongozi ngazi ya wilaya nk wewe unataka kukamua tena wananchi? Kweli waafrika tuna roho za kishetani zilizojaa ubinafsi!
Tunaiona dunia vile tulivyo.

Haiwezekani mtu aandike kitu, wewe mwenyewe ukiri kuwa ni cha ki 'utopia' halafu hapohapo umushutumu kwa 'ubinafsi wake'!!

Inaanza na wewe, ukishajiamini kuwa una roho nzuri au at least unaweza kuwa na roho nzuri ndio unaweza kuziona na roho nzuri zilizozagaa mitaani.

Ukiona huwezi kuamini mtu, jua kwamba na we umeshindwa kujiamini na ni matokeo ya ukoloni, matokeo ya kutoukataa ukoloni uliokuja na mbinu ya kutengeneza mistrust baina ya watu ili watawalike wasiungane
 
Walazamishe wabunge watoe!
Wabunge 309 wakikatwa Kodi kwenye package Yao hata kama ni 15% Tu itatosheleza kabisa kusaidia hao watu wako! Na kile kiinua mgongo cha hao wabunge cha 200+M wakikatwa Kodi 15%, watakuwa wamechanja zaidi!

Siyo ulazimishe watu tuliopigika tutoe! Kwa kutuletea tozo! Za kwenye soda na juice zinatosha!
Watu wangu tena? hahahahah! Mkuu yaani unaona uchungu sana kuchangia sh. 20 kwa kununua maji ya chupa kwa ajili ya kuchangia mlemavu au mtoto yatima? Kweli? Yaani hata ungekatwa 100, badala ya kununua maji 400 ununue 500 unadhani itakuathiri kihivyo? Halafu kama huna hela kabisa unabeba maji yako.

Naona unekoma na wabunge tu. Kuna mwingine kakomaa na walevi. Walevi nao wakiibuka watakomaa na wanywa soda. Hahahahah yaani mradi kukwepa wajibu tu. Mwisho wa siku unaweza kushangaa walevi ndio wanakubali kuchangia hahahahahah
 
Mkuu hili linaweza kuwa moja ya suluhisho, lakini kitu nisichokubali mimi ni utaratibu wa kila mtu kuhisi mwenzake ndio mwenye wajibu halafu yeye ana haki tu,hilo ni tatizo kubwa. Yaani inapokuja suala la kuhurumiwa kila mtu anadhani yeye ndio anapaswa kuhurumiwa. Linapokuja suala la kupokea kila mtu hudhani yeye ndio hupaswa kipokea. Linapokuja suala la kutoa,kila mtu hudhani mwenzake ndio hupaswa kutoa ni.k hii ni mbaya sana.

Kutatua tatizo la namna hii kwenye mada hii lazima kila mtu achangie/akatwe ki dizaini fulani.

Wananchi wanachangia kupitia KODI lukuki wanazolipa!! Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wanalipa kodi nyingi sana; tatizo sio watu kuchangia bali ni jinsi hiyo michango kupitia kodi inavyotumika!!!
 
Kwenye malipo ya umeme kuna tozo zisizo za lazima au zinazoweza kupunguzwa bila athari.
Hivyo basi tunaweza kupata thumni [senti 50] au shilingi 1:00 kwa kila uniti ya umeme.
Hapa namaanisha tusiongeze gharama bali pesa hizi zipatikane muno huko kwenye tozo/makato yaliyomo.
 
Hiyo ni kazi ya NGO's, wanaweza kuweka mabox kwenye kaunta za supermarket ambapo watu wanaweza kuweka chenji zinazobaki wakishalipia manunuzi, huko majuu inatumika sana hata kuchangia pesa za tafiti mbalimbali, mfano saratani za kina mama..........wale wahudumu pale kaunta za malipo wanakuwa wanawa alert wateja kama watachangia kwenye box ambalo linakuwa pembeni....
 
unajua misaada ambayo nchi zilizoendelea hutoa kwa nchi maskini ni sehemu ya kodi ya raia wa nchi husika ambazo wanatozwa na serikali zao ili kusaidia maskini kwenye nchi nyingine?

Kwenye jamii yetu kuna watu wenye mahitaji maalum ikiwemo walemavu, Watoto mayatima, waliotelekezwa n.k ambapo watu hawa hawawezi kujinusuru wenyewe mpaka wasaidiwe.

Kwa sasa watu hawa huomba omba mtaani wakitegemea kupewa 200 kotoka kwa raia wachache wenye huruma, wengine wakiomba wakikosa huamua kugeuaka kuwa wezi.

Badala ya kuacha hali hii iwe itakavyokuwa, Ni muhimu tuweke Tozo angalau ya Tsh. 20 kwa Kila chupa ya maji ya kunywa, Fedha itakayopatika itumike kujenga safe house ambazo zina kila huduma (bure) kwa ajili ya makundi haya maalum huku wakifundishwa fani mbalimbali, wanaoweza kujitegemea wanaachwa wanaanza kujitegemea, wanaoshindwa wanalelewa hadi mwisho wa Maisha yao.

Watu hawa hawajapenda kuwa walemavu n.k hivyo ni sahihi na ubinadamu kutumia kodi ya raia wazima kusaidia wenye uhitaji maalum. Hili ni jambo muhimu kiuchumi, Kijamii, Kiusalama na ki ubinadamu. Tunganeni kupigania jambo hili kwa kuwa ni muhumu kwa Taifa na ustawi wa mwanadamu.
Mambo yetu tumeyamaliza?

Nikajua unawazungumzia wenye mahitaji maalumu wa Tanzania.
 
Wananchi wanachangia kupitia KODI lukuki wanazolipa!! Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wanalipa kodi nyingi sana; tatizo sio watu kuchangia bali ni jinsi hiyo michango kupitia kodi inavyotumika!!!
Mkuu suala la kukosena uadilifu na baadhi ya watu kutumia vibaya kodi za watu nakubaliana nawe kuwa ni tatizo lakini tunatakiwa kuendelea kupambana nalo huku tukifanya mambo ya msingi. Yaani hatuwezi kuacha mambo ya msingi kwa sababu ya wezi.

Ni sawa na kusema kwa kuwa kuna panya road basi tusimiliki mali ili wakose cha kuiba. Unadhani utakuwa uamuzi sahihi?
 
Hiyo ni kazi ya NGO's, wanaweza kuweka mabox kwenye kaunta za supermarket ambapo watu wanaweza kuweka chenji zinazobaki wakishalipia manunuzi, huko majuu inatumika sana hata kuchangia pesa za tafiti mbalimbali, mfano saratani za kina mama..........wale wahudumu pale kaunta za malipo wanakuwa wanawa alert wateja kama watachangia kwenye box ambalo linakuwa pembeni....
Good point ila bongo hawatachangia.halafu hela itakayochangwa kwa mfumo huo bongo haitakuwa na accountability kabisa, wataila walioweka maboksi.
 
Hapo sawa,kwa sababu tuna wizara ya makundi maalumu inahitaji pesa kuondoa watu ombaomba mitaani,walemavu,wagonjwa makubwa,wazee nk ..
Sahihi kabisa mkuu. Yaani ile ya kusema tu kuanzia kesho hatutaki mtu mtaani haiwezi kufanya kazi ispokuwa kama kuna namna ya kuwanusuru wahusika. Kuna watu wamekata tamaa mkuu, hawana matumaini yoyote, hata ukisema uwapeleke jela wala hata hawajitetei.
 
Hizo tozo watozwe hao wanaoruka sarakasi badala ya hoja na wanapata posho bila hiyana, tozo kibao lakini kinachofanyika hakionekani
 
Fedha itaishia kwa watu fulani tu
Hakuna chochote kitakChowafikia
Bongo as usual upigaj jadi yetu

Ova
 
Back
Top Bottom