Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Pesa za tasaf tu zunaenda kwa walioshiba

Ova
 
Hoja nzuri lakini wenye uhitaji ni wengi mno na hiyo tozo haiwezi kutosha kabisa.

Ila kumbuka kuna ule upande nao ni ombaomba kuliko hawa na ukizingatia hawana uhitaji wowote. Hawa watapata kiasi gani kwenye hiyo tozo.


Lakini sio kesi. Kama kodi zetu zingekuwa zinatumika sehemu kwa usahihi, kila mtu angejivunia na kuilipa. Zingekuwa msaada mkubwa sana.
 
Wanataka kumkamua Ng'ombe maziwa ikiwa pumba hapewi, sasa sijui yatatoka maziwa au damu!
 
Wazo zuri, Tatizo inaonekana wananchi wamezichoka tozo mpya ikiwa za zamani hawajui zinafanyia nini, mleta mada boresha wazo then lipeleke sehemu husika.

Sisi kwa sisi ndio wakuifanya dunia sehemu salama ya kuishi, sisi ndio wenye uwezo wa kuwapa tabasamu wasio na tabasamu, naunga mkono hoja.
 
Nimetoa lakini 3 wamekata elf 8500, halafu mtu anaminya pua tozo kwenye maji!
 
Wakatwe tu watu wenyewe badala ya kuchangia hoja wanaruka sarakasi, mwingine eti uwanja wa ndege ubadilishwe jina, mwingine eti wanawake wanabinuka sana makalio wanapopanda kwenye bodaboda[emoji3][emoji3][emoji3] wakatwe hao
 
Badala kila kitu kukimbilia kupendekeza kuingiza tozo, unajua ukiachana na hao wenye uhitaji maalum ni maeneo mangapi hayapewi attention ya kutosha? maana tutotoka kwenye wenye uhitaji maalum, tutakuja na tozo ya wagonjwa wasio na msaada, tutakuja tozo ya yatima, wasioweza kupata mlo kwa siku etc.. mlolongo hauwezi kuisha, na je hizo tozo zitatumika kama ilivyokusudiwa? Au ndo tutazidi kuwaonyesha watawala ni jinsi gani hii fursa ya ni njia bora zaidi ya kukamua wananchi!
Kwanini tusianze kuhamisisha kila mtu kwa nafasi yake, aanze na kuwasaidia wanaomzunguka japo kwa kidogo tu alichonacho!? Maana sioni sababu ya kushabikia tozo ambazo hatuna imani kuwafikia walengwa, wakati hata wao wenye uhitaji maalumu wa mtaani kwako, huwezi hata kusave hizi sh 20 kila mwezi ukajenga utaratibu wa kuwapelekea(kumpelekea japo mmoja tu) japo mafuta ya kupaka!? Kila mmoja akifanya kwa nafasi yake....
 
Fedha itaishia kwa watu fulani tu
Hakuna chochote kitakChowafikia
Bongo as usual upigaj jadi yetu

Ova
Sasa tufanyeje mkuu? Maana wabongo wengi ndio hiyo ni wapigaji
 
Mkuu, unazungumzia wale wa tuma na yakutolea? Wale tulishakubaliana watu wanakuja kuchukulia nyumbani hahaha
 
Good observations. Ni kweli mkuu changamoto unazosema zipo.
 
Masikini hawaweZi kuishaz

Marekani wenyewe wana masikini mafukara lakini wana finance nchi zingine na kupeleka masilaha

Nature ndio ipo hivyo
 
Masikini hawaweZi kuishaz

Marekani wenyewe wana masikini mafukara lakini wana finance nchi zingine na kupeleka masilaha

Nature ndio ipo hivyo
Sio kumaliza maskini mkuu, ishu ni kupunguza maumivu kwa watu wenye mahitaji maalum ambapo wana hali za kimaumbile au kimazingira ambazo zinawafanya washindwe kusimama wenyewe bila ya kupata msaada maalum.
 

Mambo ya kufanya ya msingi ni kukomesha kuwa na serikali yeye mafisadi na hiyo haiwezi kupatikana kwa Katiba inayoelekezwa na Kikwete!!! Rasimu yenye maoni ya watu ilisha tengenezwa kwa fedha nyingi na tume ya Warioba; kwa Sababu zake Mwenyewe Kikwete na genge lake wanataka eti MUKANDALA ndio atuandikie Katiba ambayo pasipo shaka haitakidhi matakwa ya wananchi Kwani hilo genge halikuchaguliwa na wananchi!! Mambo ya msingi yatafanyika tukipata katiba ya wananchi na sio ya HANGAYA/KIKWETE!
 
Mkuu, katiba mpya kwenye jamii corrupt haiwezi kusaidia sana. Kwa mfano una jamii inayoamini kuwa wizi ni ujanja, katiba mpya itasaidiaje?
 
Mimi nimekaa New York nimeona mtu mwenye utindio wa ubongo ambaye kwa Tanzania angefungiwa ndani au kuwa ombaomba lakini New York huyu mtu alikuwa anafanya kazi supermarket kupanga vitu.

Alikuwa anafanya kazi yake, anapata mshahara wake, ana dignity yake.

Kwenye basi kila siku asubuhi watu walikuwa wanampenda sana stories zake, ingawa mtu mwenyewe hata kusema vizuri hawezi inabidi umjulie.

Lakini alifanya kazi aliyokuwa na uwezo nayo, ikampa ujira wenye dignity.

Ndiyo maana wenzetu wameendelea, wanajua kumpa kila mtu nafasi ya kufanya kazi kwa uwezo wake.

Sisi tunataka kuharakisha hawa hawawezi kazi wasaidiwe, inaondoa hata dignity ya maisha yao.

Wapeni kazi, most ya hao walemavu wana ulemavu wanaoweza kusaidiwa kufanya kazi, aliyeumia mguu apewe wheelchair afanye kazi.

Habari za tozo kila kukicha ni ujima wa kugawana umasikini.

Tuongeze uzalishaji, tusiongeze tozo.
 
K
Ajabu Sana. Huoni shida kung'ang'aniza watanzania wengine kuchangia, unaona shida wabunge kuchangia!

Wazo lako nalikataa binafsi.
Zipo Wizara na taasisi zinzazoshughulikia hao wasiojiweza, taasisi za kidini, NGO, watu binafsi. Hahitajiki Kodi ya kipekee Kwa ajili hiyo!

Mtakuja na tozo Kwa ajili ya chaki na ubao wa shule za kata, mara mtakuja na tozo za ununuzi wa vifaa vya maabara, TUACHENI JAMANI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…