Ulweso
JF-Expert Member
- May 24, 2016
- 23,111
- 28,020
Wanakusanya kisha wanaenda kujenga maisha yao wenyeweHalafu wenye mamlaka wakishakusanya, wanazitapanya tu kadiri wawezavyo! Jambo hili linakatisha watu tamaa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanakusanya kisha wanaenda kujenga maisha yao wenyeweHalafu wenye mamlaka wakishakusanya, wanazitapanya tu kadiri wawezavyo! Jambo hili linakatisha watu tamaa.
Pesa za tasaf tu zunaenda kwa walioshibaUpuuzi mtupu, picha ulizopost wala siyo Bongo,
Matatizo yepi!?
Serikali inakusanya Kodi ina Wizara na taasis zinazoshughulikia matatizo, haitoshi.
Mnawaza kutoza zaidi, mle zaidi! Kwanini usiseme wabunge wakatwe Kodi zielekezwe huko Kwa wahitaji!?
TASAF, MKURABITA, BARAZA LA UWEZESHAJI, NGO kibao zinazosaidia wenye uhitaji!
Nikisikia tozo nasikia kichefuchefu mixed na kiungulia.
Shangaa hata weweUnaandika hawana mikono, lakini picha zinaonesha wamekinga mikono kuomba.
Wanataka kumkamua Ng'ombe maziwa ikiwa pumba hapewi, sasa sijui yatatoka maziwa au damu!Siku hizi umefanya nini unaandika utopia namna hii? Ni kutafuta ulaji au uko kwenye ulaji mpaka umevimbiwa? Wewe unadhani sh 20 kwa raia wa kawaida ni kitu kidogo? Ukiwa nazo wewe unadhani kila mtu naye anazo? Badala ya kusema serikali ipunguze matumizi ya anasa kama kusafiria bussiness class, kununua magari ya fahari, safari zisizo na lazima, idadi ya wabunge kubwa, kuwa na utitiri wa viongozi ngazi ya wilaya nk wewe unataka kukamua tena wananchi? Kweli waafrika tuna roho za kishetani zilizojaa ubinafsi!
Nimetoa lakini 3 wamekata elf 8500, halafu mtu anaminya pua tozo kwenye maji!Saidia wewe kama wewe kuepuka hiyo laana!
Msaada haulazimishwi. Unafikiri Baraka itatoka wapi Kwa hao so called wahitaji. Kama watoaji wana manung'uniko na malalamiko na mahangaiko mioyoni mwao!??
Umejaliwa toa wewe na jamaa zako. Watanzania niwaache kwanza, tumeshatoa vya kutosha, nimetoa laki 6 wamenikata ,elfu nane na ushee! Tozo my foot!
Wakatwe tu watu wenyewe badala ya kuchangia hoja wanaruka sarakasi, mwingine eti uwanja wa ndege ubadilishwe jina, mwingine eti wanawake wanabinuka sana makalio wanapopanda kwenye bodaboda[emoji3][emoji3][emoji3] wakatwe haoWalazamishe wabunge watoe!
Wabunge 309 wakikatwa Kodi kwenye package Yao hata kama ni 15% Tu itatosheleza kabisa kusaidia hao watu wako! Na kile kiinua mgongo cha hao wabunge cha 200+M wakikatwa Kodi 15%, watakuwa wamechanja zaidi!
Siyo ulazimishe watu tuliopigika tutoe! Kwa kutuletea tozo! Za kwenye soda na juice zinatosha!
Sasa tufanyeje mkuu? Maana wabongo wengi ndio hiyo ni wapigajiFedha itaishia kwa watu fulani tu
Hakuna chochote kitakChowafikia
Bongo as usual upigaj jadi yetu
Ova
Mkuu, unazungumzia wale wa tuma na yakutolea? Wale tulishakubaliana watu wanakuja kuchukulia nyumbani hahahaHoja nzuri lakini wenye uhitaji ni wengi mno na hiyo tozo haiwezi kutosha kabisa.
Ila kumbuka kuna ule upande nao ni ombaomba kuliko hawa na ukizingatia hawana uhitaji wowote. Hawa watapata kiasi gani kwenye hiyo tozo.
Lakini sio kesi. Kama kodi zetu zingekuwa zinatumika sehemu kwa usahihi, kila mtu angejivunia na kuilipa. Zingekuwa msaada mkubwa sana.
Good observations. Ni kweli mkuu changamoto unazosema zipo.Wazo zuri, Tatizo inaonekana wananchi wamezichoka tozo mpya ikiwa za zamani hawajui zinafanyia nini, mleta mada boresha wazo then lipeleke sehemu husika.
Sisi kwa sisi ndio wakuifanya dunia sehemu salama ya kuishi, sisi ndio wenye uwezo wa kuwapa tabasamu wasio na tabasamu, naunga mkono hoja.
Masikini hawaweZi kuishazunajua misaada ambayo nchi zilizoendelea hutoa kwa nchi maskini ni sehemu ya kodi ya raia wa nchi husika ambazo wanatozwa na serikali zao ili kusaidia maskini kwenye nchi nyingine?
Kwenye jamii yetu kuna watu wenye mahitaji maalum ikiwemo walemavu, Watoto mayatima, waliotelekezwa n.k ambapo watu hawa hawawezi kujinusuru wenyewe mpaka wasaidiwe.
Kwa sasa watu hawa huomba omba mtaani wakitegemea kupewa 200 kotoka kwa raia wachache wenye huruma, wengine wakiomba wakikosa huamua kugeuaka kuwa wezi.
Badala ya kuacha hali hii iwe itakavyokuwa, Ni muhimu tuweke Tozo angalau ya Tsh. 20 kwa Kila chupa ya maji ya kunywa, Fedha itakayopatika itumike kujenga safe house ambazo zina kila huduma (bure) kwa ajili ya makundi haya maalum huku wakifundishwa fani mbalimbali, wanaoweza kujitegemea wanaachwa wanaanza kujitegemea, wanaoshindwa wanalelewa hadi mwisho wa Maisha yao.
Watu hawa hawajapenda kuwa walemavu n.k hivyo ni sahihi na ubinadamu kutumia kodi ya raia wazima kusaidia wenye uhitaji maalum. Hili ni jambo muhimu kiuchumi, Kijamii, Kiusalama na ki ubinadamu. Tunganeni kupigania jambo hili kwa kuwa ni muhumu kwa Taifa na ustawi wa mwanadamu.
Sio kumaliza maskini mkuu, ishu ni kupunguza maumivu kwa watu wenye mahitaji maalum ambapo wana hali za kimaumbile au kimazingira ambazo zinawafanya washindwe kusimama wenyewe bila ya kupata msaada maalum.Masikini hawaweZi kuishaz
Marekani wenyewe wana masikini mafukara lakini wana finance nchi zingine na kupeleka masilaha
Nature ndio ipo hivyo
Mkuu suala la kukosena uadilifu na baadhi ya watu kutumia vibaya kodi za watu nakubaliana nawe kuwa ni tatizo lakini tunatakiwa kuendelea kupambana nalo huku tukifanya mambo ya msingi. Yaani hatuwezi kuacha mambo ya msingi kwa sababu ya wezi.
Ni sawa na kusema kwa kuwa kuna panya road basi tusimiliki mali ili wakose cha kuiba. Unadhani utakuwa uamuzi sahihi?
Hapana mkuu, tusiwe negative kiasi hicho. Wakati fulani tujilazimishe kuangalia vitu kwa jicho positivwKuna kafursa kanatafutwa.....
Mkuu, katiba mpya kwenye jamii corrupt haiwezi kusaidia sana. Kwa mfano una jamii inayoamini kuwa wizi ni ujanja, katiba mpya itasaidiaje?Mambo ya kufanya ya msingi ni kukomesha kuwa na serikali yeye mafisadi na hiyo haiwezi kupatikana kwa Katiba inayoelekezwa na Kikwete!!! Rasimu yenye maoni ya watu ilisha tengenezwa kwa fedha nyingi na tume ya Warioba; kwa Sababu zake Mwenyewe Kikwete na genge lake wanataka eti MUKANDALA ndio atuandikie Katiba ambayo pasipo shaka haitakidhi matakwa ya wananchi Kwani hilo genge halikuchaguliwa na wananchi!! Mambo ya msingi yatafanyika tukipata katiba ya wananchi na sio ya HANGAYA/KIKWETE!
Mimi nimekaa New York nimeona mtu mwenye utindio wa ubongo ambaye kwa Tanzania angefungiwa ndani au kuwa ombaomba lakini New York huyu mtu alikuwa anafanya kazi supermarket kupanga vitu.Mkuu Kiranga la kuongeza uzalishaji na kupunguza ukosefu wa ajira nakubaliana na wewe kabisa. Na nilishaleta mjadala hapa namna ya kupunguza ukosefu wa ajira na kuongeza uzalishaji kwa lufanya reformations kwenye mfumo wa elimu na mfumo wa mikopo miongoni mwa hatua nyinginezo.
Lakini hili sio mbadala wa wazo hili la kuweka katozo mahali ili kuwasaidia wale wasiojiweza kabisa.
Nchi zilizoendelea zimeenda hatua moja mbele, zinatoza kodi kwa wanaofanya kazi na kuwalipa kama cha Chini wasio na ajira. Ila hii Afrika hatuwezi kufanya maana ukifanya hivi watu watachagua kutofanya kazi makusudi. Lakini hakuna anayeweza kuchagua kuwa mtoto yatima au kuwa mlemavu.
Ajabu Sana. Huoni shida kung'ang'aniza watanzania wengine kuchangia, unaona shida wabunge kuchangia!Watu wangu tena? hahahahah! Mkuu yaani unaona uchungu sana kuchangia sh. 20 kwa kununua maji ya chupa kwa ajili ya kuchangia mlemavu au mtoto yatima? Kweli? Yaani hata ungekatwa 100, badala ya kununua maji 400 ununue 500 unadhani itakuathiri kihivyo? Halafu kama huna hela kabisa unabeba maji yako.
Naona unekoma na wabunge tu. Kuna mwingine kakomaa na walevi. Walevi nao wakiibuka watakomaa na wanywa soda. Hahahahah yaani mradi kukwepa wajibu tu. Mwisho wa siku unaweza kushangaa walevi ndio wanakubali kuchangia hahahahahah