Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Kuepuka laana, tuweke tozo angalau ya Tsh. 20 kwa kila chupa ya maji ya kunywa kuwanusuru wenzetu wenye mahitaji maalum

Mkuu, katiba mpya kwenye jamii corrupt haiwezi kusaidia sana. Kwa mfano una jamii inayoamini kuwa wizi ni ujanja, katiba mpya itasaidiaje?

Katiba mpya itasaidia kwa kuwaadhibu wezi bila upendeleo kama ilivyo sasa!! Athabu zitakazotolewa kama ile Katiba ya wananchi ikipitishwa ni kwamba haitajali kama ni matoto wa Kikwete au wa Masanja wakikamatwa na NGADA wote wataadhibiwa kufuatana na sheria.
 
Hoja nzuri lakini wenye uhitaji ni wengi mno na hiyo tozo haiwezi kutosha kabisa.

Ila kumbuka kuna ule upande nao ni ombaomba kuliko hawa na ukizingatia hawana uhitaji wowote. Hawa watapata kiasi gani kwenye hiyo tozo.


Lakini sio kesi. Kama kodi zetu zingekuwa zinatumika sehemu kwa usahihi, kila mtu angejivunia na kuilipa. Zingekuwa msaada mkubwa sana.
Ripoti ya CAG imeonesha ubadhirifu mkubwa wa hela za umma.

Kabla ya kuweka tozo mpya kwa nini watu wasiangalie mianya ya ubadhirifu iko wapi na inazibwa vipi?
 
Hoja nzuri ila watakao pewa dhamana yakuratibu Jambo hili akina mwigulu jamuari na nape nadhan zile toza za miamala zimenunua DTB FC

HIZ za masikini zitanunua marefa na tff

CCM tuitoe Kwanza madarakani halafu leta hoja hii

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Ndio raha ya kuwa kiongozi Tanzania.

Unafuja mapesa ila kwakua watu wananufaika na huo ufujaji hakuna kinachoendelea.

Ndio aina ya maisha ambayo jamii zetu imezikubali.

Na inaheshimu sana watu wenye fedha zenye vyanzo vya aina hii.
 
Back
Top Bottom