Wana JF wenzangu, kuna kipindi nilipokuwa likizo nilitembelea mikoa ya Dodoma,Singida,Manyara na Arusha,nilichokigundua ni kuwa wafugaji karibu wote wa Ng'ombe wanakuwa na kundi la Kondoo, nilipouliza niliambiwa kuwa Kondoo wanasaidia kuzuia Radi,mwenye ufahamu wa kina naomba anifafanulie utaalamu uliopo nyuma ya hii kitu.
Naam niliiona hiyo kitu Shinyanga vijijini. Kwamba radi huja kama jogoo, na inapokutana na kondoo hupigana sana na mara nyingi radi hushindwa.
Halafu mtu kama wewe unajisifu umeenda shule!?
Teh teh teh teh!
Afadhali nimedaka hapa unaandika utumbo! Ntauhifadhi huu utumbo siku nyingine ukileta yale majigambo yako ya kusema wewe msomi!
Radi ya jogoo my foot!
Makanyaga huyo Nyenyere anaonekana anatumia yale majani yalioharamishwa.Hapana, usimkatalie. Vitu spiritual mara nyingi nimekuja kugundua kuwa havikubaliani na sayansi ya kawaida na mara nyingi vinakuwa havina logic!
Makanyaga huyo Nyenyere anaonekana anatumia yale majani yalioharamishwa.
Sasa akishakula ile maneno anaona vitu vya ajabu ajabu. Juzi hapa alisema kaenda kumpoke yesu! Nikamuuliza je kaja kwa basi au treni. Akaanza matusi!
Huyu jamaa wazee wake wameshapata hasara kubwa sana!.
Faida hakuna kazi kujaza choo tu.
Una Elimu gani mkuu?