Nami nichangie kama huyu bwana aliyetoa ufafanuzi wa viumbe namna vinvyoweza kutambua yaliyopo mbele katika mazingira yake(natural setting) nikiwa mdogo enzi za kuchunga nilielekezwa na babu kuwa ikianza mvua ukaona kondoo anapiga vichwa miti na hataki kuondoka wewe mwache hapo hapo swaga ng'ombe ondoka! Sasa kuna matukio kama mawili hivi nayakumbuka, nikiwa machungoni, kulianza dalili za mvua na muungurumo wa radi, kukawa kunatokea ile hali ya kondoo kubadilika na kuwa mbishi na mara anajikunyata then anajirusha kwa staili ya kushambulia. Baadaye kidogo nilipoondoka mazingira hayo kwa mbali zilitokea sauti kuubwa zilizoambatana na miale ya radi Ambapo mti uliokuwepo eneo karibu na kondoo yule ulichanwachanwa vipande vipande lakini kondoo hakupata jeraha na alirejea mwenyewe baada ya muda mrefu tangu mvua kwisha.
Inaelezwa kuwa kichwa cha kondoo ukikipasua ambayo pia nimeshuhudia kuna wadudu wawili kwa lugha ya kawaida vijijini tunaita mafilifili ambao hawa wanamwezesha kuona mambo yaliyobeyond sayansi zetu za chemistry is a branch of...... Na kwa maelezo ya mchangiaji nikiunganisha na yale matukio naipata ile picha ya namna kondoo yule alivyokuwa akikusanya nguvu na kujitupa kwa kugonga kichwa kwenye mti, tukio la pili wakati anafanya hivyo kujitupatupa, ng'ombe dume alijipendekeza baaasi alipigwa kichwa kimoja akalala kifo cha mende hadi kifo! Kilichoendelea ni kwensa kutoa taarifa nyumbani! Hapo ni mkoa wa Iringa nayakumbuka haya!