Kuepusha majengo kuanguka hivyo; Itungwe Sheria ya nyumba na kanuni za ujenzi

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Sheria zilizopo za maendeleo ya miji si mahususi kama Kanuni za Ujenzi, Wakati sheria zilizopo zinahitaji tu jengo kupewa cheti cha kufuata taratibu baada ya kukamilika, Kanuni zinataka jengo lipate uthibitisho kama linastahili kwa makazi ya binadamu au la.

Sheria zilizopo ambazo ni pamoja na Kanuni za Upangaji wa Miji na Viwango vya Nafasi za Mwaka 2011, Sheria ya Upangaji wa Miji ya Mwaka 2007, na Sera ya Taifa ya Makazi ya Binadamu.

Kanuni za Ujenzi zitajumuisha masuala manne muhimu ambayo sheria zilizopo hazishughulikii, ambayo ni: afya, usalama, ustawi, na ulinzi.

Kanuni hizo zinataka wamiliki wa viwanja kupanda miti na bustani zinazochukua angalau asilimia kumi ya eneo la kiwanja chao.

Kama tungekuwa na Kanuni hizi, kusingekuwa na haja ya kuwa na kampeni za muda mfupi za kupanda miti, Kanuni hizo pia zinapinga milango yenye nondo na badala yake zinapendekeza uzio wa miti badala ya uzio wa tofali.

Katika wilaya za Ilala, Kinondoni, na Temeke, wakazi wanasikitishwa na ukiukwaji mbalimbali wa sheria za ujenzi unaohitaji kushughulikiwa.

Utafiti huo ulibaini kuwa majengo mengi yamejengwa karibu sana na mengine, hayana nafasi za kuegesha magari, yana mifumo duni ya maji taka, na hayazingatii mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Viwango vya majengo mengi ni vya chini. Haiingii akilini, inakuwaje jengo lililojengwa miaka mitano tu iliyopita linaanza kuwa na nyufa?.

Nashangazwa na hatua ya serikali kubomoa majengo Jangwani lakini kuyaacha yale ya Kariakoo, ambapo mengi yalijengwa bila kufuata sheria zozote zinazotoa mwongozo wa maendeleo ya miji.
 
Tatizo hakuna uchunguzi watu wanachimna misingi kiholela holela
 
Sheria nzuri na mikakati inaweza kuwepo, lakini kama utekelezaji hauzingatiwi, ni kazi Bure.

Kingine hatuna utaratibu wa kupanga mipango ya kujihami na mambo, utasikia mawazo mengi sana baada ya janga kutokea, baada ya mwezi hakuna mtu anagusia hilo jambo Hadi janga litokee tena.
 
Wamiliki wengi wa majengo wanapendelea kutumia mafundi wa jadi na wasio na usajili badala ya wale waliosajiliwa, wakidai kwamba wa mwisho ni ghali sana. Hata hivyo, changamoto ni kwamba wengi wa mafundi wasiosajiliwa hawajui sheria za upangaji wa miji na maendeleo ya mali isiyohamishika. Na mafundi wengi wanawashauri wamiliki wa majengo kupuuza kutumia huduma za wasanifu majengo kwa sababu hiyo hiyo ya gharama,

Wakati huohuo, halmashauri za manispaa zinashindwa kufanya ukaguzi wa maeneo ya ujenzi kama sheria zinavyowataka kufanya. Halmashauri hizo pia zinashutumiwa kwa kuajiri watu wasio na sifa na uzoefu wa kusimamia miradi ya ujenzi.
 
Hivi unajua ukitaka kujenga chochote au kuongezea chochote lazima upate building permit ? Na hio permit inabidi usipewe mpaka uwe umekidhi vigezo vyote na kama ni nyumba au ghorofa umefanya test zote soil test n.k. na vilevile kama ni structure amekwambia cha kuweka na contractor na structure kucheki katika kila hatua ya ujenzi ?

Sasa kama sheria hizo zipo na hazifuatwi na watu wanakula mlungula hata kuwaongezea sheria ni kama umewapa vyanzo zaidi vya rushwa...

Kinachotakiwa kubadilika sio sheria zaidi (hizo zipo) bali utamaduni wa kufuata sheria na kuacha ulafi na umimi wa kula mlungula (watu kuwajibishwa)
 
Kama mwananchi amekumbana na ukiukwaji wowote wa sheria za ujenzi, anapaswa kuripoti ukiukwaji huo kwa halmashauri ya manispaa ili hatua stahiki zichukuliwe.
 
Hata zikitungwa Sheria na Sheria mafundi wezi Zege linachakachuliwa Cementi inaibiwa Nondo zinachakachuliwa nk.
Lazima kwenye sheria kuwe na namna ya ku deal na wanaokiuka sheria. Hata kama kutakuwa na uchakachuaji lakini itapunguza maafa kwa kiasi fulani
 
Hivi unajua ukitaka kujenga chochote au kuongezea chochote lazima upate building permit ? Na hio permit inabidi usipewe mpaka uwe umekidhi vigezo vyote na kama ni nyumba au ghorofa umefanya test zote soil test n.k. na vilevile kama ni structure amekwambia cha kuweka na contractor na structure kucheki katika kila hatua ya ujenzi ?

Sasa kama sheria hizo zipo na hazifuatwi na watu wanakula mlungula hata kuwaongezea sheria ni kama umewapa vyanzo zaidi vya rushwa...

Kinachotakiwa kubadilika sio sheria zaidi (hizo zipo) bali utamaduni wa kufuata sheria na kuacha ulafi na umimi wa kula mlungula (watu kuwajibishwa)
Ni bora iwepo kuliko hii situation ya mtu anajijengea tu bila taratibu.

Building permit ni sheria tofauti na hii ninayopendekeza inayoitwa Building Code
 
Sheria zilizopo za maendeleo ya miji si mahususi kama Kanuni za Ujenzi, Wakati sheria zilizopo zinahitaji tu jengo kupewa cheti cha kufuata taratibu baada ya kukamilika, Kanuni zinataka jengo lipate uthibitisho kama linastahili kwa makazi ya binadamu au la.

Sheria zilizopo ambazo ni pamoja na Kanuni za Upangaji wa Miji na Viwango vya Nafasi za Mwaka 2011, Sheria ya Upangaji wa Miji ya Mwaka 2007, na Sera ya Taifa ya Makazi ya Binadamu.

Kanuni za Ujenzi zitajumuisha masuala manne muhimu ambayo sheria zilizopo hazishughulikii, ambayo ni: afya, usalama, ustawi, na ulinzi.

Kanuni hizo zinataka wamiliki wa viwanja kupanda miti na bustani zinazochukua angalau asilimia kumi ya eneo la kiwanja chao.

Kama tungekuwa na Kanuni hizi, kusingekuwa na haja ya kuwa na kampeni za muda mfupi za kupanda miti, Kanuni hizo pia zinapinga milango yenye nondo na badala yake zinapendekeza uzio wa miti badala ya uzio wa tofali.

Katika wilaya za Ilala, Kinondoni, na Temeke, wakazi wanasikitishwa na ukiukwaji mbalimbali wa sheria za ujenzi unaohitaji kushughulikiwa.

Utafiti huo ulibaini kuwa majengo mengi yamejengwa karibu sana na mengine, hayana nafasi za kuegesha magari, yana mifumo duni ya maji taka, na hayazingatii mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Viwango vya majengo mengi ni vya chini. Haiingii akilini, inakuwaje jengo lililojengwa miaka mitano tu iliyopita linaanza kuwa na nyufa?.

Nashangazwa na hatua ya serikali kubomoa majengo Jangwani lakini kuyaacha yale ya Kariakoo, ambapo mengi yalijengwa bila kufuata sheria zozote zinazotoa mwongozo wa maendeleo ya miji.
Tatizo la nchi hii sio sheria, ni wale wanaopewa kuzisimamia
 
Lazima kwenye sheria kuwe na namna ya ku deal na wanaokiuka sheria. Hata kama kutakuwa na uchakachuaji lakini itapunguza maafa kwa kiasi fulani
Kwa Watanzania ni vigumu sana,wewe angalia Mchina akija Tanzania kwenye ujenzi huwa lazima wasimamie kwenye kuchanganya Zege na kwenye kusuka Nondo lazima wawepo wakati wa kumimina Zege lazima wawepo baada ya hapo ndio wanamuachia Mtanzania ni kwamba wameshatusoma tunapenda kuiba hatujali kitakachotokea halafu kikitokea tunaanza kulaumu sana na wengine kufikia kusema Gorifa limelogwa.
 
Sheria zilizopo za maendeleo ya miji si mahususi kama Kanuni za Ujenzi, Wakati sheria zilizopo zinahitaji tu jengo kupewa cheti cha kufuata taratibu baada ya kukamilika, Kanuni zinataka jengo lipate uthibitisho kama linastahili kwa makazi ya binadamu au la.

Sheria zilizopo ambazo ni pamoja na Kanuni za Upangaji wa Miji na Viwango vya Nafasi za Mwaka 2011, Sheria ya Upangaji wa Miji ya Mwaka 2007, na Sera ya Taifa ya Makazi ya Binadamu.

Kanuni za Ujenzi zitajumuisha masuala manne muhimu ambayo sheria zilizopo hazishughulikii, ambayo ni: afya, usalama, ustawi, na ulinzi.

Kanuni hizo zinataka wamiliki wa viwanja kupanda miti na bustani zinazochukua angalau asilimia kumi ya eneo la kiwanja chao.

Kama tungekuwa na Kanuni hizi, kusingekuwa na haja ya kuwa na kampeni za muda mfupi za kupanda miti, Kanuni hizo pia zinapinga milango yenye nondo na badala yake zinapendekeza uzio wa miti badala ya uzio wa tofali.

Katika wilaya za Ilala, Kinondoni, na Temeke, wakazi wanasikitishwa na ukiukwaji mbalimbali wa sheria za ujenzi unaohitaji kushughulikiwa.

Utafiti huo ulibaini kuwa majengo mengi yamejengwa karibu sana na mengine, hayana nafasi za kuegesha magari, yana mifumo duni ya maji taka, na hayazingatii mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Viwango vya majengo mengi ni vya chini. Haiingii akilini, inakuwaje jengo lililojengwa miaka mitano tu iliyopita linaanza kuwa na nyufa?.

Nashangazwa na hatua ya serikali kubomoa majengo Jangwani lakini kuyaacha yale ya Kariakoo, ambapo mengi yalijengwa bila kufuata sheria zozote zinazotoa mwongozo wa maendeleo ya miji.
Hakuna town planning
Kama ipo imesahauliwa
Tunajenga kiholela kama uyoga
 
Tatizo sio sheria tatizo ni utayari wa vyombo vya kusimamia hizo sheria.
Mfano sheria inavitaka vituo vya mafuta viwe katika umbali fulani na ipi inajulikana.
Lakini vituo vya mafuta vimekaribiana kabisa.
Mfano bunju sokoni kuna vituo 4 vya mafuta vimezidiana mita kadhaa tu.
 
Back
Top Bottom