Kuepusha majengo kuanguka hivyo; Itungwe Sheria ya nyumba na kanuni za ujenzi

Kuepusha majengo kuanguka hivyo; Itungwe Sheria ya nyumba na kanuni za ujenzi

Tatizo sio Sheria mkuu,lakin wanaosimamia hzo Sheria mfano mtu anataka kujenga kaenda kuchukua hyo permit siku ya mwanzo kapewa lakn hao wanao mpa hyo permit wako ofisin na hata wakija site wanakuja cku moja2 hawanawez kurud tena Kufatilia huyu hilo jengo kuwa limejengwa kulingana na makubaliano au vigezo vilivyowekwa.hvo nn kifaynike n kila mtu anae husika kuwajibika Kwa upande wake kulingana na taaluma yake
 
Tatizo sio sheria tatizo ni utayari wa vyombo vya kusimamia hizo sheria.
Mfano sheria inavitaka vituo vya mafuta viwe katika umbali fulani na ipi inajulikana.
Lakini vituo vya mafuta vimekaribiana kabisa.
Mfano bunju sokoni kuna vituo 4 vya mafuta vimezidiana mita kadhaa tu.
Kuanzia Bunju Mianzini hadi daraja la Mapinga linalotenganisha mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ni kilometres 6, lakini kuna vituo 9 au 10 vya mafuta. This is terrible
 
Sheria ipo. Soma humu nimeiattach sheria na kuchambua

 
Sheria zilizopo za maendeleo ya miji si mahususi kama Kanuni za Ujenzi, Wakati sheria zilizopo zinahitaji tu jengo kupewa cheti cha kufuata taratibu baada ya kukamilika, Kanuni zinataka jengo lipate uthibitisho kama linastahili kwa makazi ya binadamu au la.

Sheria zilizopo ambazo ni pamoja na Kanuni za Upangaji wa Miji na Viwango vya Nafasi za Mwaka 2011, Sheria ya Upangaji wa Miji ya Mwaka 2007, na Sera ya Taifa ya Makazi ya Binadamu.

Kanuni za Ujenzi zitajumuisha masuala manne muhimu ambayo sheria zilizopo hazishughulikii, ambayo ni: afya, usalama, ustawi, na ulinzi.

Kanuni hizo zinataka wamiliki wa viwanja kupanda miti na bustani zinazochukua angalau asilimia kumi ya eneo la kiwanja chao.

Kama tungekuwa na Kanuni hizi, kusingekuwa na haja ya kuwa na kampeni za muda mfupi za kupanda miti, Kanuni hizo pia zinapinga milango yenye nondo na badala yake zinapendekeza uzio wa miti badala ya uzio wa tofali.

Katika wilaya za Ilala, Kinondoni, na Temeke, wakazi wanasikitishwa na ukiukwaji mbalimbali wa sheria za ujenzi unaohitaji kushughulikiwa.

Utafiti huo ulibaini kuwa majengo mengi yamejengwa karibu sana na mengine, hayana nafasi za kuegesha magari, yana mifumo duni ya maji taka, na hayazingatii mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Viwango vya majengo mengi ni vya chini. Haiingii akilini, inakuwaje jengo lililojengwa miaka mitano tu iliyopita linaanza kuwa na nyufa?.

Nashangazwa na hatua ya serikali kubomoa majengo Jangwani lakini kuyaacha yale ya Kariakoo, ambapo mengi yalijengwa bila kufuata sheria zozote zinazotoa mwongozo wa maendeleo ya miji.
Kabla ya kujenga nyumba, (gororora), udongo hupimwa wa eneo husika na kuchunguza uhimilivu wa jengo kwa mahesabu ya mchoro wa jengo, zoezi linatakiwa lifanywe na wataalamu waliosomea kwa muda mrefu
 
Kabla ya kujenga nyumba, (gororora), udongo hupimwa wa eneo husika na kuchunguza uhimilivu wa jengo kwa mahesabu ya mchoro wa jengo, zoezi linatakiwa lifanywe na wataalamu waliosomea kwa muda mrefu
Absolutely
 
Back
Top Bottom