Kufa ni kufanya nini?

Kufa ni kufanya nini?

hili la brain kutofanya kazi, ikiacha kufanya kazi athari nje ya mwili kunakuwa na nini?
 
the secret of death is as myth as the concept of god it is self.
ni kweli mtu ni soul na since soul hatuwezi kuithibitisha kwa kuishika coz soul ni pumzi , basi kuthibitisha kifo cha mtu kwa pumzi kutokuwapo pekee yatosha?
 
na kama soul ndio mtu na kauacha mwili basi pumzi inatakiwa kuwa ndio kitu cha kutazama na kusema kafa.
 
if the whole issue of proving someone is dead is debatable,then all those who are already dead,were they real dead?
 
kwa mtindo huu, mimi natamani nikifa nisizikwe waniweke tu sehemu hadi nitakapoharibika basi ndio wanizike.maana nafikiri umestuka upo kaburini au frijini hv inakuwaje haya ni mateso sana.
 
hili la brain kutofanya kazi, ikiacha kufanya kazi athari nje ya mwili kunakuwa na nini?

ukirejea post ya nuyma anasema kuwa kuacha kufanya kazi kwa brain sio sululisho la mtu kufa ndio maana madaktari bingwa wanaweza kukufanyia operation ya ubongo..
 
kwa mtindo huu, mimi natamani nikifa nisizikwe waniweke tu sehemu hadi nitakapoharibika basi ndio wanizike.maana nafikiri umestuka upo kaburini au frijini hv inakuwaje haya ni mateso sana.

hii inakuwa kama habari ya bibi wa kichina ambaye alikuwa amekufa lakini mwili wake bado ni wamoto na aharibiki hii hali amekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 20+

labda na wewe unaweza fanya hivyo ili tujue kama utakuwa umekufa au la..
 
Chochote kwenye mwili wako kinapokosa uhai kinakuwa kimekufa, lakini kifo chako ni umauti, wewe ni nafsi. Kiwiliwili na viungo vyake vyake vyote ni vyako na vinaweza kufa lakini wewe hujawa maiti. Kila nafsi itayaonja mauti.
 
kwa mtindo huu, mimi natamani nikifa nisizikwe waniweke tu sehemu hadi nitakapoharibika basi ndio wanizike.maana nafikiri umestuka upo kaburini au frijini hv inakuwaje haya ni mateso sana.

unaonaje ukiwekewa sensor za bei rahisi.Kama ukiamka hata kama kw aunyonge basi iwasiliane na waliopo katk surface?Au pia inaweza kuwa hasara wakikutoa halfua ufe kweli?

Hata wazee wetu kabla ya kuja tamaduni za Kigeni walikuwa wakizeeka sana,au wakiumwa ugonjwa usiojulikana walikuwa wakitupwa misituni,katik misitu iliyopigwa marufuku watu kuenda.Imagine....walivyokuwa wakiliwa na fisi, au wanyama wengine wasioona haja ya kuua kwanza viumbe wasiojiweza..wengine walikuwa wakiachwa na chakula cha siku kadhaa aktik vijumba vya muda kama vya masai...Kweli alivyosema Mwenyewe aliye Mwenyewe.."...watu wangu wanaangamia kwa kukos amaarifa..."

walioweza survive kwa siku kadhaa wengine walibaki ili wajifie kwa kile walichoamini wakiwa wazima kuwa mtu ukishaenda huko ni mbaya kurudi uraiani.....wengine waliporudiwa na fahamu walipambana na kuweza jipatia chakula na madawa na baadaye kuanza maisha mapya,ama huko porini ama kwa kwenda katik jamii nyingine wasipojulikana na kuanza maisha.hawa ndio waliokuwa kama outcast na waliishi porini walihofiwa kama mizimu.Kwa bahati mbaya kaburini ahkuna hizo chance.
 
Kufa ni opposite ya kuishi. Ukifa mwili hauna uhai tena unaoza tu na utendaji wa ubongo unakoma, haupo tena ni kama jiwe tu hapo barabarani.
Wengine wanasema eti mwili tu ndio unakufa lakini vingine vinaishi!

Nadhani labda ni kwa namna ya kitamadhali (figurative) kwamba kama uliacha matendo mazuri yatakumbukwa na bado yatatumika kuwapa watu nguvu (encouragement) na mbinu/maarifa ya suluhisho fulani.

Kama vile akina Isaac Newton na Galileo wamekufa lakini theory zao bado zipo hai, labda tunaweza kusema tu bado wapo hai kwa kukumbukwa kwa mazuri na kutumia theory zao mpaka leo.
 
maana daktari mmoja alikuwa akieleza swala zima la kufa nikaogopa kidogo maana alisema asilimia 60 ya watu wanaowapima watu na kukamilisha kuwa wamekufa huwa wanakosea kwani mtu anaweza zimia hata kwa siku 3 na bado akawa hajafa akaenda kufia kaburini kwa kukosa hewa na joto na vitu vingine.
hii kuna siku nilijiuliza sana, baadae nikadhani kuwa labda nimepatwa na uchungu mkubwa ndo maana nikafikia kujiuliza hivyo, nikaishia kumwomba msamaha Mungu na maisha yakaendelea. hiyo siku nilimpoteza mtoto wa mdogo wangu, alikuwa 6 months, sikuwepo wakati wa tukio, ila nilipofika home nilimgombeza sana dada yetu mmoja ambaye alikuwa hospitali na mdogo wangu wakati mtoto anafariki, nikamwuliza alikubalije wamchukue mtoto na kumpeleka mochwari? alithibitisha vipi kama kweli yule mtoto alikuwa amekufa?
kumbe haya mambo huwa yanatokea kweli....... nimesikitika sana
 
kwa mtindo huu, mimi natamani nikifa nisizikwe waniweke tu sehemu hadi nitakapoharibika basi ndio wanizike.maana nafikiri umestuka upo kaburini au frijini hv inakuwaje haya ni mateso sana.
ukiwa huwezi kusema tena, hakuna wa kukutetea, watakuweka tu kwa friji. nadhani huku kuogopa mtu aliyekufa kunasababisha kuwapoteza wapendwa wetu kabla hawajafa. maana utakuta mtu kahangaika kidogo, mwisho kimya, dr. anasema ameshakufa, ndani ya nusu saa tayari yupo kwenye friji
 
hii inakuwa kama habari ya bibi wa kichina ambaye alikuwa amekufa lakini mwili wake bado ni wamoto na aharibiki hii hali amekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 20+

labda na wewe unaweza fanya hivyo ili tujue kama utakuwa umekufa au la..
nadhani wengi wetu tungetamani hili, lakini nani atakubali kukaa na mtu ambaye anadhani amekufa ndani ya nyumba? hata "sweetheart" hapo hakutaki tena
 
Fixed point,
ahaa natamani wasiniweke katika nyumba ambayo wao wanaishi wanipeleke katika sehemu mbali na home labda wajenge kanyasi huko porini halafu wanilaze humo ndani wao waende zao, nikizinduka badae heri. nikiwa nimekufa kweli basi heri pia.

Mimi naogopa sana hii kitu na nimeanza kukosa imani na hawa wanosema kuwa sasa huyu kafa kamzikeni au kamekeni mochwari.
 
hii inakuwa kama habari ya bibi wa kichina ambaye alikuwa amekufa lakini mwili wake bado ni wamoto na aharibiki hii hali amekuwa nayo kwa zaidi ya miaka 20+

labda na wewe unaweza fanya hivyo ili tujue kama utakuwa umekufa au la..

mkuu,
sasa hiyo ni china,wamekubali kuendelea kukaa na mtu huyu for 20yrs je ingekuwa bongo yetu wangeshasema tumzike na huyu mtu angezikwa mzima.
 
Naomba kuelimishwa juu ya hiki kitu kufa.

Tukisema mtu kafa kinachokufa ni nini? Je, kutopumua ni kufa? Brain kutofanya kazi ni kufa? Mapigo ya moyo yakiacha kufanya kazi ndio kufa au roho kutoka ndio kufa?

Napata shida mno nisaidieni maana naanza kuhisi watu wanaweza kuwa wanazikwa wazima.

Sure, watu wengi wanazikwa wakiwa wazima kwa sababu kufa sio kazi rahisi kama wataalam wetu wanavyofikiri au vyombo vyao vinavyothibitisha.

MAANA HALISI YA KUFA NI KUUACHA MWILI, SO SWALI NI JINSI GANI MTU ANAUACHA MWILI NI MPAKA UJUE MTU NI NINI NA MWILI NI NINI maana hivi ni vitu viwili vyenye uhusiano lakini havifanani OTHERWISE TUTAKESHA NDUGU KUDISCUSS HII MADA.

Kuna watu tunasema wamewahi kufikia karibu na kifo(near the death experience) yaani vifaa vya kitaalam vilishafeli kufanya kazi na kuthibitisha mtu amekufa then baadae anaamka au kuanza kupumua, na katika hali kama hii watu wengine wakathubutu kutudanganya eti walikufa na kufufuka na kuanza kutoa ushuhuda wa uongo na tukawaheshimu na hata kuwapa utukufu.

kufa ni process ndefu thats why watu wengi hufia chumba cha maiti a.k.a montually kama si kaburini kama unavyohisi!!
 
kwa kuwa kuna mwili ubongo na roho, na mtu ni roho. na mwili unauhusiano na mtu(roho) mwili ukipata matatizo mtu anaumia. hivyo basi kufa kwa vile kuna uhusiano na mwili moja kwa moja therefore mtu anapokuwa hajafa na akazikwa hai mwili ukaathirika mojakwamoja mtu anapata maumivu na kufanya afe vibaya sana.

kwani mtu (soul) haumiiii? tukisema roho inauma pale hauumii mwili but ni mtu(soul)
au ndio mambo ya cfibers are burning?
 
Sure...watu wengi wanazikwa wakiwa wazima kwa sababu kufa sio kazi rahisi kama wataalam wetu wanavyofikiri au vyombo vyao vinavyothibitisha...MAANA HALISI YA KUFA NI KUUACHA MWILI,SO SWALI NI JINSI GANI MTU ANAUACHA MWILI NI MPAKA UJUE MTU NI NINI NA MWILI NI NINI maana hivi ni vitu viwili vyenye uhusiano lakini havifanani OTHERWISE TUTAKESHA NDUGU KUDISCUSS HII MADA...Kuna watu tunasema wamewahi kufikia karibu na kifo(near the death experience) yaani vifaa vya kitaalam vilishafeli kufanya kazi na kuthibitisha mtu amekufa then baadae anaamka au kuanza kupumua...na katika hali kama hii watu wengine wakathubutu kutudanganya eti walikufa na kufufuka na kuanza kutoa ushuhuda wa uongo na tukawaheshimu na hata kuwapa utukufu...kufa ni process ndefu thats why watu wengi hufia chumba cha maiti a.k.a montually kama si kaburini kama unavyohisi!!

uko sahihi mkuu. ndio maana mimi nilisema naomba sasa kujua hivyo viashiria ambavyo tutasema sasa mtu kauacha mwili.na mwili sasa hauna tena thamanituuzike tuuchome au tuufanya chochote. nini kitakuwa kitakachotufanya tujue sasa process ya kufa imekamilika.sasa mwili umekufa?
 
maana hapo juu tumeshaona kuwa ubongo kuacha kufanya kazi sio kufa,mapigo ya moyo kuacha kufanya kazi sio kufa,mwili kutokuwa na joto sio kufa,kutopumua sio kufa pengine vyote vikiwa havipo ndio kufa.
 
Back
Top Bottom