Kufa ni kufanya nini?

na je ubongo(hii cpu ya mwili) umeacha kufanya kazi nitajuaje au hadi niwe mtaalamu(daktari) unapimwaje sasa kusema ubongo haufanyi kazi? je ubongo ukiacha kufanya kazi vyote vinasimama au?
 

Kufa is when the silver chord is snapped.
 
Safi sana mkuu nimekuelewa vya kutosha!good explanation.
 
Ni pale ambapo seli hazizalishwi tena mwilini.
 
ningependa sasa kujua hivyo viashiria ambavyo madokta wanatumia kusema huyu sasa kafa.



Death is an event that represents the permanent cessation of all biological functions that sustain a living organism. Brain death ndiyo inatumika kuthibitisha kifo cha binadamu.
 
Huyu mama anadai haki yake kuwa bado anaishi ingawaje kisheria inajulikana kuwa keshakufa.

Link BBC News - Indian woman's 24-year fight to prove she is alive

anadai yeye ana watu wengine ndio wanadai kwa niaba yake?
si kuna ruhusa ya dokta kumuua mgonjwa endapo nduguze watakubali kufanya hivyo inapotokea kuwa mtu huyo anauguua kwa muda mrefu na kwamba hawezi kupona tena? kumpunguzia maumivu hayo wanampiga sindano ya sumu.
 
Nakubaliana na wengi walio na wasiwasi kuhusu daktari kuthibitisha kuwa mtu fulani kafa. Ningependa kutoa maelezo ya ziada ili kuleta ufahamu zaidi kwa aliyeuliza swali.

Ili daktari awezi kutoa uthibitisho kuwa mtu amekufa anafuata mchakato huu:
Kwanza anaangalia kuwa je kuna juhudi zozote za mtu au mgonjwa kupumua bila ya msaada wowote?

Pili anaangalia mtoto wa jicho (pupil)ambalo litakuwa limepanuka sana kuashiria kuwa ubongo ulikosa oxygen.

Tatu ni kuangalia kwa kutumia kipimo cha stethoscope kuhakikisha kuwa kuna mapigo ya moyo na vile vile kama kuna sauti ya hewa inapoingia au kutoka kwenye mapafu.

Hivyo vyote vilivyotajwa hapo juu ni viungo (organs)tatu muhimu kwa uhai wa binadamu. Vinapogundulika kuwa havifanyi kazi basi daktari atatoa uthibitisho wa kifo.

Viashiria vingine vya kifo ni kuendelea kushuka kwa joto la mwili amblo huanza kuonekana baada ya nusu saa baada ya kufa. Vile vile baada ya masaa 6 hadi 12 mwili wa mtu aliyekufa huanza kukakamaa (rigor mortis).

BRAIN DEATH
Kwa kawaida ubongo ni kiungo (organ) ambacho kinatumia oxygen na glucose nyingi kwa ajili ya shughuli zake nyingi. Ubongo unatumia hadi asilimia 20 ya oxygen na glucose mwilini ili uweze kufanya kazi yake kikamilifu.

Hivyo basi unapokosa vitu hivyo japo kwa dakika tatu tu unasimama kufanya kazi hivyo ndivyo tunasema kuwa kuna brain death.

Kwa kuwa ubongo ndio unaoongoza na kuelekeza viungo vyote vya mwili in maana kuwa unaposimama tu kufanya kazi basi moyo, mapafu, fingo na vinginevyo navyo vitasimama. Wengi mmesikia kuwa fulani kapata brain death na hawa mara nyingi wapo ICU ambapo kuna mashine zinazoweza kusaidia moyo na mapafu vifanye kazi ya kusukuma damu na kuiongezea oxygen japo ubongo wa mtu huo umesimama kufanya kazi.

Kwa wale wanaosema kuwa unaweza kuthibitishwa kuwa umekufa wakati ambapo bado una uhai inawezekana, kwani sisi binadamu tunao uwezo tofauti wa kuweza kuishi katika mazingira magumu. Ndio maana kuna wazamiaji wanaoweza kuwa majini kwa muda wa dakika 20 bila ya kudhurika.
 

Nani alikudanganya kuwa alikufa kumbe alikuwa hajafa, je ulikuwepo mpaka ukajua kuwa ni uongo? How did you know kwamba alikuwa hajafa?
 
oi hii Majimoto a.k.a MAMA POROJO ameiona hii....!
 
Last edited by a moderator:
(Kwa maana ya kibaiolojia) Kufa ni Seli za mwili zinapoacha kufanya kazi. Period.
 
na kama soul ndio mtu na kauacha mwili basi pumzi inatakiwa kuwa ndio kitu cha kutazama na kusema kafa.


kwenye red! kama hivyo ndivyo! Jee wanaozama majini kwa mda, wanakuwa wamekufa kwa mda?
 

nimekusoma mkuu.
 
aiseeeeeee! speechless! heri yao watakaokuwa tayari muda na saa vitakapofika vya mwili kutengana na roho! Lord Have Mercy on us. AMEN!
 
mkuu unaweza kunidadavulia hapa ulikuwa una maana gani?

The loss of all evidences of life.
Namaanisha kwamba UHAI nikitu kilicho ndani ya kiumbe kinacho ishi. Kutokana na hilo uhai unapo toweka ndipo huwa tunaita kifo.

Na kiumbe chochote kilicho hai huwa nasifa zifuatazo ambazo pia huitwa evidences of life ambazo ni REPRODUCTION, GROWTH, EVOLUTION(ADAPTATION), EXCRETION, RESPONSIVENESS, FEEDING and BREATHING

Pindi sifa zote hizo saba tajwa hapo juu zinapo potea ndio huwa tunaita KUFA{LOSS OF ALL EVIDENCES OF LIFE}.
 
Ni pale ambapo seli hazizalishwi tena mwilini.

OK, ngoja niwape kisa ambacho nimekishuhudia Jumapili hii ya tarehe 9/9/12. Akina mama wawili walikuja church na mwili wa mtoto wa miaka kama 12 hivi, walikuwa wamemzungushia kanga na kumlaza kwenye kiti. Hakuna mtu aluyejua kulikuwa na nini kwenye nguo alizofunikwa nazo.

Pastor akaanza kufundisha na kuhubiri. Katika kuzunguka kwa audience huku akihubiri akaona huo mzigo lakini hakujua ni nini, akadhani kuna mtu kaleta mzigo na ameoccupy viti vingine. Akapita mara ya pili na kuuliza ni nini hicho. Akina mama wakasema ni mtoto wao (mmoja wao ni mwalimu wake shuleni). Pastor akawauliza kulikoni? Wakasema ni mtoto amefariki 7 days ago!!! Alikuwa shuleni anafanya assignment, ghafla akadondoka akafa.

Pastor akaomba watu wachukue ile maiti na kuipeleka madhabahuni, mahubiri yakasimama kwanza na kanisa zima tukaanza kuomba na kumuita yule mtoto arudi kwenye mwili wake KWA JINA LA YESU.

It took about 10 minutes yule mtoto akainuka, akafanyishwa mazoezi kidogo, then akaletewa chakula akala. Hiki ni kisa cha kweli ambacho nimekishuhudia mwenyewe, hapa hapa DSM.

Hata hivyo ni jambo linalotegemewa mahali ambapo watu wanamuabudu Mungu wa kweli, Yesu alisema (Math 10:8) Heal the sick, raise the dead, cleanse those who have leprosy, drive out demons. Freely you have received...
 

nani alikuwa na hakika kuwa yule mtoto alikufa. je kuna mtu aliyempima kusema kweli kafa? sio usanii wa wahubiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…