Kufahamu mambo yako hapa: Ramli ya kutizama mambo unayotaka

asante pia
Mkuu Rakims naomba unisaidie maono haya kama itawezekana, nilikuwa nimepitiwa na kausingizi lakini naamini sikuwa nimelala kidogo ikaja picha fulani kama ya Allien kwa ile sura tunayoaminishwa na wazungu nikataka nisituke nikajizuia mpaka akaja kabisa nikawa naongea naye huku nina akili zangu timamu kabisa na sio za usingizi nikaamuambia naomba unisaidie nipate kazi akakaa kama sekunde kadhaa akiwa anapiga mahesabu nafikiri alikuwa anatumia kompyuta mana nilikuwa nasikia kelele fulani kama mtu anayechezea keyboard baadaye akanijibu haitowezekana nikamuuliza kwanini akanijibu tena vile vile.

Baadaye kidogo akapotea huku nikiwa bado kwenye maono nikaangalia juu kwenye dali nikaona wadudu wengi mfano wa panya si panya, popo si popo, bundi si bundi. Hayo maono nimeyapata mchana huu huu.

Naomba unisaidie hii ina maana gani na je nifanye nini hapo mkuu Rakims
 
Ni muda gani unatafuta kazi ni kwa kiasi gani swala la kupata kazi limekukaa kichwani?

Rakims

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Ni mwaka wa pili huu na hili suala lipo kichwani kwa kiasi kikubwa kusema ukweli.
Kwa nafasi kubwa mkuu kutolea hukumu hii njozi kama ni ya kimwili au kiakili au kiroho inaleta ugumu, pia kwa wakati ambao umeota mchana utawala wake mkubwa nap huwa ni akili sasa kiroho ina maana kimwili ina maana lakini pia kiakili ina maana sasa nipe details kamili ili nikupe jibu sahihi maana kwa majibu hayo ndio umezidi kuifanya kuwa complicated

Rakims

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Sawa mkuu ila sijajua nikupe details gani kiongozi.
 
Habari mkuu,
Kwa hapo kidogo nimepata picha lakini kwa ndoto uliyoota ni ishara kuwa kuns roho tofauti ambayo inakuharibia maisha ikiwa ni pamoja na kukukosesha kazi na msisitizo umeonekana humo kwenye ndoto nikushauri kwanza upitie thread yangu ya maradhi ya kiroho jijue kama umerogwa ili upate picha ninachozungumzia

Rakims

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Naomba link ya huo uzi mkuu.
 
Nikihjtaji kujua mlango na 2 utaratibu upoje mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…