SoC04 Kufahamu ndoto na kipaji cha mtoto inasaidia kujenga wafanyakazi mahiri wa kesho

SoC04 Kufahamu ndoto na kipaji cha mtoto inasaidia kujenga wafanyakazi mahiri wa kesho

Tanzania Tuitakayo competition threads

dahasingh Suleysh

New Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
2
Reaction score
2
Hakuna kitu kizuri kama kufanya kazi ambayo ipo kwenye damu yako, uipendayo kwa muda mrefu. Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea ni kwamba mtoto huwa mtu huwa anaandaliwa kuwa mfanyakazi fulani tangu kipindi akiwa mdogo, ambapo wazazi huwa wanatazama mwenendo wa mtoto katika michezo ambayo anaanzisha akiwa na wenzie.

Hapo wanagundua mtoto anapendelea zaidi kitu gani na huchukuwa hatua ya kumkuza mtoto huyo kwenye hizo hadi anapokuwa mkubwa hivyo kuwa mtu ambae ni mzalishaji mzuri katika familia na nchi kwa ujumla.

Tofauti na nchini Tanzania watoto wengi huwa wanachanganyikiwa katika maamuzi ya kuwa nani baada ya kuwa mkubwa.

Kuna Amini ninayokwambia ndoto ya kwanza mtoto kukwambia kuwa anataka kuwa nani hicho ndiyo kitu pekee anaweza kukifanya kwa ubunifu wa hali ya juu pindi utakapompa nafasi ya kukifanya na unapomuwezesha kwa kumsapoti kwa kile afanyacho huja kuwa mfanyaji kazi mzuri sana.
Katika kuiandaa Tanzania ya kesho serikali inatakiwa kuanzisha programu maalumu kwa ajili ya kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kukuza vipaji vya watoto wao ili kuwaandaa wawe wazalishaji wazuri wa kesho.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom