Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
kuna mshikaji wangu yupo TAMISEMI,,ameniomba nimtrain kunywa MNAZI manake asilimia 75 ya kamshahara kake kanaishia kulipa madeni ya MASANGA bar!TAMISEMI aidha uwe muadilifu wa kiwango cha SGR Ili ustaafu salama au tamaa za kula vizuri, kupata usafiri bora na kupeleka watoto private school zikupande uishie jela...
Hivi ukisema Tamisemi unazungumzia Wizarani au Kwenye halmshauri au manispaa au mahospitalin maan kwa navyojua Tamisemi ndo wizara yenye ukubwa sana maana ofisi nyingi ziko chini yake.TAMISEMI huku kumejaa uchawi,kusemana na kuingizana mkenge
Halimashauri,elimu na mahospitalini. Zogo.Hivi ukisema Tamisemi unazungumzia Wizarani au Kwenye halmshauri au manispaa au mahospitalin maan kwa navyojua Tamisemi ndo wizara yenye ukubwa sana maana ofisi nyingi ziko chini yake.
Sasa wapi kwenye shida na wapi kwenye afadhali, iwe mashuleni huko, kwenye maofisi ya kata huko
Tamisemi ni Halmashauri kimsingi. Ambapo kuna idara za afya, mahospitalini, Elimu ni shule zote, mifugo na kilimo maafisa kilimo na mifugo na uvuvi si unasikia Ulega juzi kala kichwa Kigoma huko.Hivi ukisema Tamisemi unazungumzia Wizarani au Kwenye halmshauri au manispaa au mahospitalin maan kwa navyojua Tamisemi ndo wizara yenye ukubwa sana maana ofisi nyingi ziko chini yake. Sasa wapi kwenye shida na wapi kwenye afadhali, iwe mashuleni huko, kwenye maofisi ya kata huko
Ni mungu tu atupiganie mpaka mwenyekiti wa kijiji, mtendaji wa kitongoji ni boss wako na anakufanya atakalo, aisee hii nchi ngumu sana, ni kudra za mungu tu.TAMISEMI aidha uwe muadilifu wa kiwango cha SGR Ili ustaafu salama au tamaa za kula vizuri, kupata usafiri bora na kupeleka watoto private school zikupande uishie jela.
TAMISEMI hata ukiiba elfu 50 jiandae kufukuzwa kazi au kufungwa.
TAMISEMI ukifanya kazi kuwa makini, unaweza kuingizwa mkenge bila kujua dk yoyote.
TAMISEMI kuna kuna mabosi wengi na kila bosi ni spy . Yaani wa juu kazi yake kubwa ni ku mzoom wa chini Ili ampeleke jela.
Serikali boresheni maslahi ya watumishi wa TAMISEMI, wana hali ngumu sana.
Rafiki yangu yuko huko TAMISEMI kasimamishwa kazi kwa vikesi uchwara hajui afanye nini.
Hakuna sehemu zenye wachawi, wanafiki, watu wa roho mbaya, kijicho, husda, fitina kama watu wa halmashahuri, ndio maana nyuso zao zimekosa nuru kwa unafiki na uchawi, kufanya kazi tamisemi ni sawa na kujivisha boom muda wowote linaweza kukulipikia, huku ndio wanasiasa wanapotafutia umaarufu, utasikia daktari fulani tumemfukuza kzazi, mara mwalimu mkuu tumemfukuza kwa kuimba wimbo wa zuchu n.k.....mambo ni mengi...Kufanya kazi halmashauri inabidi uwe na roho ngumu sana na ujitoe akili kama wafuasi wa ccm
Majizimbona hawana ufanisi wowote na huo u spy wao
tofautisha u spy na umbea, huko wengi wambea na wanafiq wanao ficha upumbavu wao kwenye mgongo wa u spy,
EhehheheChangamoto ya kazi nyingi hasa hizi ambazo njaa nyingi ni mifumo uchwara ambayo unakuta imeundwa ili kumnufaisha fulani na chawa wake
Kwa hiyo unakuta kila ofisi ina kigenge fulani ambacho bosi na baadhi ya wafuasi wake wamejiundia kamfumo, hapo ndio watajipangia fursa na ulaji kisha walio nje ni kalenda na kupishana na maokoto
Hapo hata kama wanafanya ndivyo sivyo usithubutu kuhoji au kuwakosoa, watatumia kila nyenzo utolewe ndani ya mchezo
Ukiwa kwenye ofisi fulani ridhika na mshahara na nafasi uliyonayo, ukiwaza cheo, posho, marupurupu, vikao, semina na safari utapata ugonjwa wa moyo maana kuvipata lazima uwe chawa kichizi na kujipendekeza kupitiliza kitu ambacho wenye kujielewa wengi hawawezi kufanya.