Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Hahaha Chadema ndio ajenda ya ccm, muifute Chadema mtakuwa mmefuta siasa za vyama vingi.

Mnajua Chadema ndiyo chama pekee kilichobaki.
 
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 
Hizi sasa ndio siasa za ukweli. Sio zile siasa za kususa susa. Wakati Chadema wanaendelea kushupaza shingo, wenzao, wamepiga bao la kisigino.
Naendelea kusisitiza, "if you can't get what you want, then what you get". Yaani usipopata kile kikubwa unachokitaka, pokea hata kidogo ulicho patina!.
Na kwenye mapambano ya kupigania kitu, "if you can't beat them, join them". ACT Wazalendo wameipambania Zanzibar kwa kupigana na CCM, they couldn't beat them, now they have joined them.

Hongera sana ACT Wazalendo kwa kujitambua, hongera sana rais wa Zanzibar, Dr. Hussein Mwinyi kwa kuwa muungwana kama baba yako.
Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania..
P
 
Upinzani upo ndani ya mioyo ya watu na usitegemee kwa waliofukuzwa uawanachama basi chama kitakufa. Wakati mwl. Nyerere akiwa Rais wa nchi kuna watu kama wewe walitamka hakuna wa kumrithi awe Rais. Lakini nchi inaendelea kusonga mbele. Viongozi sio wanaubemba upinzani ila wanachama na watapatikana watu wengine katika kundi hilo na chama kitasimama tu
 
Nafanya tuu rejea.
P
 
Sasa mkuu Pascal unashauri watu ambao hawashauriki . Hawa wanajua kila kitu.Wanasiasa wao,wanaharakati wao,wanasheria wasomi wao ,madaktari wao,,mainjinia wao,wasomi wao,wachawi wao na kila kitu chao.Achana nao hao !
 
Hizi mamlaka za uteuzi sijui hawako jf?
Huyu mwana CCM anavyojitoa kuisema chadema halafu wanateuliwa warembo na waigizaji kuwa wakuu wa wilaya.
Hata usemaji wa wizara?
Jamaa unatumia nguvu nyingi Sana.
 
Spin doctor!Chadema is still live and kicking
 
CCM anaishauri CHADEMA jinsi ya kufanya ili kisife [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]


Acheni basi maigizo. Kama kweli kina Mdee kutimuliwa chama kitakufa, basi acheni kuwakumbatia ili CHADEMA ife.
 
Japo naunga mkono hoja, ya "ukisusa sie twala...," na siungi mkono hii tabia ya kususa susa.... Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto? na hapa Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! na Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA is almost dead, due to deadly mistakes! This is your only survival -- do or die. Msirudie kosa

Lakini kama wanasusa for genuine reasons za kutotendewa haki, kama tulivyo shauri hapa Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Najua by now wasoma trends wanajua the consequences za kutotenda haki kwenye uchaguzi, sisi washauri huru tuliisha shauri kabla Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! hivyo Shaka asijitape wakisusa kwa kutetendewa haki sisi twala, badala ya kula wakajikuta wao ndio wanaliwa vichwa!.

Karma haina mswalie Mtume, walishindwa kumlinda Blaza, karma ikafanya yake!, ili kumlinda Maza na karmic consequences, sisi tunao ijua karma, lazima tumsaidie Maza kwa kumweleza ukweli ili aepuke the consequences na yeye asije... hivyo kwa kuanzia tumemshauri Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
 
Hatimaye Chadema sasa imeacha kurudia kosa, its doing the right thing!. Keshokutwa Jumatano wanawasamehe wabunge wake 19!.
Update
Hatimaye Chadema wameacha kushupaza shingo na wamekubali matokeo!, kwa kuufuata ushauri wa bandiko hili CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao

Nimepokea taarifa, hii kutokea twitwani Kisha nikasoma na bandiko hili humu JF Tundu Lissu: CHADEMA tumeanza kupokea Ruzuku

Chadema wameufuata ushauri wa bandiko hili, waneacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo ya uchaguzi wa 2020!, sasa wameacha kushupaza shingo, wameyatambua matokeo kimya kimya!, wamewasamehe mashujaa hawa kimya kimya msamaha ambao utatangazwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 8 Machi na Mwenyekiti wa Chadema, mbele ya Rais Samia!.

Iliwa kusemwa kuwa hakuna mkate mgumu wowote mbele ya chai!, tayari Chadema imeisha anza kupokea ruzuku hivyo sasa ita survive!. Na ile kesi ya kina Halima Mdee na wale 19 iliyopo mahakamani itafutwa!.

Hongera sana Chadema, for doing the right thing!, mtabarikiwa, viongozi wenu watabarikiwa, chama chenu kitabarikiwa na Tanzania Itabarikiwa!.
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki CCM kwa kukubali reconciliation
Mungu ibariki Tanzania
Paskali
 
Nimeisoma hukumu, 1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CCM ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!.
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?.
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!.
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team!.
A Way Forward
1. Kwa vile Chadema imefanikiwa kuwatimua hao 19 sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu , ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.

2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue Halima Mdee, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, kitagharimia vikao vyote viwili, na Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.
Paskali.
 
Akili Huna ,pumbavu
 
Unakosea vingi sana kwenye andiko lako hili.

- Mahakama kutotoa maamuzi kwenye jambo ambalo halikuombwa sio kosa la mahakama, kwasababu wao husema mahakama sio mama yako ikupe kile ambacho hukuiomba.

- Unakosea pia unaposema wale wanawake walivuliwa uanachama kwa kutosikilizwa, wakati walitakiwa kufika siku waliyoambiwa waende kujitetea kisha wao wakaamua kuingia mitini kwa kisingizio cha usalama wao, sijui kwanini hawakwenda na walinzi binafsi.

- Kuita kikao cha Chadema "kangaroo court" wakati hiyo Katiba ilipitishwa na msajili wa vyama, unajionesha ulivyojaa ujuaji, au unaficha udhaifu wa msajili kwasababu ni zao la CCM wenzio.

- Wakina Mdee walipewa taarifa ya kuhitajika kujitetea kwenye kikao cha KK hawakwenda, na wala utetezi wao haukuwa hawakupewa hati ya mashtaka, utetezi wao ulikuwa ni usalama wao, hebu tuwekee hapa ile taarifa waliyotumiwa na Chadema ili tuone kama haikuwa na vigezo vya kuitwa hati ya mashtaka? Vinginevyo usilazimishe maoni yako ndio yawe sheria kufuatwa na kila mtu.

- Wakina Mdee waliitwa kwenye kikao baada ya kupewa taariga ya kuhitajika kujitetea, hawakwenda, hiyo maana yake taarifa iliwafikia, hii hoja yako nayo ni void, ajabu unasema jambo hili halikufanyika.

- Unadai baada ya kina Mdee kuapishwa Chadema walipaswa kufanya a due process ya nidhamu, sijui hapa umejigeuza nani kuwaamrisha Chadema nini wafanye, ndio maana kule juu nimekwambia punguza ujuaji.

- Wakati wa kuitisha kikao cha baraza kuu, ndipo Covid 19 ilipopamba moto, hapo wasingeweza kuitisha kikao kuwajaza wajumbe wengi toka karibia mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani. Hili lingeenda kinyume na protocal za kujikinga na Corona, ndio maana time taken ilikuwa ndefu, hapakuwa na sababu ya emergency, hivyo hii hoja yako nayo ni potofu.

- Suala la Halima Mdee kutimuliwa na KK halikuwa na tatizo, ndio maana hata judge jana hajaona popote penye tatizo kwenye maamuzi ya KK, again punguza ujuaji bro.

- Again, suala la baraza kuu kubariki maamuzi ya KK kwa kutofanya mapitio ya maamuzi hili nalo halikuhusu, ni ujuaji wako na mawazo yako tu, unless utuambie kama kuna kifungu cha sheria kilichovunjwa kwa hilo hapo juu kutofanyika, lakini sio kusema Chadema ni chama kichanga...

Na mengine yote uliyoandika binafsi sioni uzito wake, ni mawazo yako binafsi yasiyo na ushahidi kisheria ndio umeyatumia kutoa hili hitimisho lako, jambo ambalo kwangu naona sio sahihi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu zipo nyepesi kwamba umewahi kuwa mwajiriwa katika moja ya barozi zetu nje ya nchi , je hizi tetesi zipo na ukweli gani au ni majungu tu
 
Mkuu denoo JG, kwanza asante, kwa objectivity yako, kwasababu ni wana Chadema wachache sana wenye analytical skills and abilities to read in between the lines. Asante kwa hili.
Mengine nitaendelea nayo mdogo mdogo
P
 
Mkuu denoo JG, kwanza asante, kwa objectivity yako, kwasababu ni wana Chadema wachache sana wenye analytical skills and abilities to read in between the lines. Asante kwa hili.
Mengine nitaendelea nayo mdogo mdogo
P
Hii ndio tofauti ya Pascal Mayalla na wajuaji wengine wa mboga mboga. Paskali akichemka, akipata mtu wa ku expose anachutama. Mimboga mboga mingine kazi kushupaza shingo tu! Shwain!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…