Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA inakaribia kufa, hii ndio njia yenu pekee ya kujinasua

Wakifukuza waliopo na kuteua tena wengine kwenda bungeni kwa yakini watakuwa wamethibitisha uchaguzi ulifanyika mwaka 2020, kwamba ulikuwa huru na haki na kwamba JPM alishinda kwa uhalali na mgombea wa CDM alishindwa hivyo atawajibika kwenda tume ya uchaguzi kusaini kukubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu. Hivyo wataomba radhi kwa kulalamika isivyo halali kwamba kulikuwa na uchafuzi na kura ziliibwa!!!
 

Paschal ni mtu wa hovyo
 
Mkuu Intelligence Justice , naunga mkono hoja hii, ila kwa taarifa nilizonazo, ni Chadema walipokubali kukaa mezani na CCM kwa breakfast ya pamoja na kukubaliana 2025 ,watagawana nusu mkate, nilisema humu, Siasa za Kijungu Jiko, Penye Uzia, Penyeza Rupia!. Hakuna Mkate Mgumu Mbele ya Chai!, Hata Uwe Mgumu Vipi, Mbele ya Chai/Rupia, Lazima Utalainika! mtu aliyekuja kutibua mambo ya nusu mkate ni huyu Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
P
 
Acha ujinga Pascal hauna uchungu na Hii nchi Katu unawaona Hawa mchwa ni halali wanayoyafanya??
 
Acha ujinga Pascal hauna uchungu na Hii nchi Katu unawaona Hawa mchwa ni halali wanayoyafanya??
Kuwa mchwa ni jambo moja na haki na halali ni jambo jingine!. Let's assume hao 19 ni kweli wamekosa, then waadhibiwe kwa haki!, wapewe haki ya kusikilizwa na kutimuliwa kwa haki!. Katiba ya Chadema iko wazi wide open na imeweka taratibu zote za nidhamu, kwanini hazifuatwi?.
P
 
Paskali, bado unawang'ang'ania tu mpaka sasa! Miaka yote unatuambia Chadema inakufa ili ufarajike ikifa, hii ni tabia ya wachawi wa kisukuma na sijui ikifa itacheza ngoma ya maswezi?
 
Kufanya kosa ni kosa na kurudia kosa ni kosa pia, provided mtu anayefanya kosa anajua kwamba anafanya kosa.
 
Kufanya kosa ni kosa na kurudia kosa ni kosa pia, provided mtu anayefanya kosa anajua kwamba anafanya kosa.
Mkuu Magobe T ,
It's presumed wakati unafanya kosa kwa mara ya kwanza ni hukujua kuwa ni kosa, hivyo unajifunza kwa makosa, hivyo kukosea mwanzo sio kosa, ila kurudia kukosea ndio kosa!.
P
 
Navyoona wewe utakufa na CHADEMA utaiacha
 
Haueleweki. Heri ungeandika kwa kiswahili.

Amandla...
 
Wanabodi,

Kitendo cha CHADEMA kususa kupeleka majina ya Wabunge wa Viti Maalum, ni kufanya kosa, ila kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa.

Paskali
Asante sana kwa taarifa hii, ushauri wangu ni atangaze chochote na alalakike vyovyote kuhusu hizi figisu figisu za uchaguzi wa serikali za mitaa, ila hala hala ,Chadema wasifanye kosa 2019 kususia uchaguzi wa serikali za mitaa,hivyo uchaguzi wa 2020 waliambulia jimbo moja tuu la ngama,wakasusia kuutambua uchaguzi,wakauita ni uchafuzi, baada ya maridhiano wakautambua na kuyatambua matokeo。

Kufanya kosa sii kosa,kosa kurudia kosa, Chadema wasirudie makosa,wasijitoe kwa kususia uchaguzi wa seikali za mitaa!。
P
 
Kweli kabisa, kususia uchaguzi kwa Chadema huku vyama vingine vikishiriki hakujawahi kuleta mabadiliko yoyote ya hizi chaguzi zinavyoendeshwa

Ila zaidi wanashiriki wakiwa pungufu uwanjani na sheria za mchezo hadi refa haziko upande wao.

Kingine viongozi wa juu hawana sauti ya pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…