aisee LIKUD umesema kitu cha ajabu mno...Mimi nasoma vitabu kadhaa kwa mwezi labda sita au saba vya page 600-700 aisee najua vitu hadi najiogopa.
ngoja nikupe mfano, kuna bidhaa moja ni chemical nilikua nataka kutengeneza maana niliishtukia inatengenezwa na watu wachache mno na inauzika kikirtimba mno,nikawafata manufacture kama nane tu ndo wapo hapa dar aisee sikuambulia kitu pamoja na offer yangu ya milion na laki tano kwa formula tu
nikaingia online nikapata wahindi flani aisee jamaa wanauza kitabu ila kiukweli kina formula nyingi zenye msaada usd 800,tamaa ikaniingia nikasema hapana siezi toa hela nyingi hv big no,aisee nilihaha online,soma majournal ya chemistry,ingia maforum ya chemistry download vitabu ilinichukua whole week nikawa na formula kama nane ila haziko wazi yaani kama ni percentage wanakwambia 10%-40% wakati mi nataka single digit
nikazinarrow down mpaka nikapata fomula yenyewe aisee nikaingia mzigoni bado changamoto ikawa raw material zinafanya production cost ziwe juu baadae nikairekebisha product moja % yake ndo ikakaa sawa nikaingia sokoni
ningekua mvivu watoto wasingeenda shule,sa hv nina bidhaa 20 za chemical natengeneza na nyingine najua ila sina tu mtaji, sasa basi hapo ni kwenye chemicals nasoma fani nyingine kama sasa hv naanza kusoma electromagnetic sijui kabisa ila nimevutiwa,pia naanza kichina mwakani na nataka nijifunze kuhusu markets and stocks in deep
usisahau nipo vizuri kwenye ujenzi 80%
nipo vizuri biashara na mauzo na utawala 60%
nipo vizuri space and 30%
nipo poa kwenye inteligence
lakini nilisomea architecture...
kusoma nakubaliana na ww LIKUD ni silaha ya hatari sana hulali njaa,sasa hv najikita kusoma vitabu vya kunipa hela tu yaani nakisoma nakigeuza hela
tujitahidi kusoma vitabu