Kufanya masters/PhD vs kusoma vitabu kipi Bora?

Nlichojifunza kwa hii mada yako ni kwamba, unaweza kuwa chochote duniani wakati wowote, hata kama unahisi umekosea huko nyuma whether katika elim mfano level ya elimu au aina ya fani uliyoisomea etc iwapo tu utatambua unataka nini na kuamua kubadili gia angani ,na unaweza huwa geek katika uwanja mpya mara 100 ya walio kutangulia ,even a sky is not a limit...period.
 
Exactly
 
aisee LIKUD umesema kitu cha ajabu mno...Mimi nasoma vitabu kadhaa kwa mwezi labda sita au saba vya page 600-700 aisee najua vitu hadi najiogopa.
ngoja nikupe mfano, kuna bidhaa moja ni chemical nilikua nataka kutengeneza maana niliishtukia inatengenezwa na watu wachache mno na inauzika kikirtimba mno,nikawafata manufacture kama nane tu ndo wapo hapa dar aisee sikuambulia kitu pamoja na offer yangu ya milion na laki tano kwa formula tu

nikaingia online nikapata wahindi flani aisee jamaa wanauza kitabu ila kiukweli kina formula nyingi zenye msaada usd 800,tamaa ikaniingia nikasema hapana siezi toa hela nyingi hv big no,aisee nilihaha online,soma majournal ya chemistry,ingia maforum ya chemistry download vitabu ilinichukua whole week nikawa na formula kama nane ila haziko wazi yaani kama ni percentage wanakwambia 10%-40% wakati mi nataka single digit

nikazinarrow down mpaka nikapata fomula yenyewe aisee nikaingia mzigoni bado changamoto ikawa raw material zinafanya production cost ziwe juu baadae nikairekebisha product moja % yake ndo ikakaa sawa nikaingia sokoni

ningekua mvivu watoto wasingeenda shule,sa hv nina bidhaa 20 za chemical natengeneza na nyingine najua ila sina tu mtaji, sasa basi hapo ni kwenye chemicals nasoma fani nyingine kama sasa hv naanza kusoma electromagnetic sijui kabisa ila nimevutiwa,pia naanza kichina mwakani na nataka nijifunze kuhusu markets and stocks in deep

usisahau nipo vizuri kwenye ujenzi 80%
nipo vizuri biashara na mauzo na utawala 60%
nipo vizuri space and 30%
nipo poa kwenye inteligence

lakini nilisomea architecture...

kusoma nakubaliana na ww LIKUD ni silaha ya hatari sana hulali njaa,sasa hv najikita kusoma vitabu vya kunipa hela tu yaani nakisoma nakigeuza hela

tujitahidi kusoma vitabu
 
A na B yote Ni sawa kwa sababu hata Mimi sijasoma vitabu vya mathematics pekee. Nimesoma pia vitabu vya fields kuanzia " intelligence" ( ujasusi) mpaka female anatomy. In addition to that Kama mwanaume hauja master somo la female anatomy both in theory and practice basi jua kwamba hauna uwezo wa kumridhisha kingono mwanamke yoyote yule duniani.. uki master somo Hilo linakupa uwezo wa kuujua mwili wa mwanamke Kama unavyo ujua mwili wako wewe mwenyewe..
 
Ur the true son of ur father. Personally nimejifunza vitu vingi sana katika maisha yangu kupitia usomaji wa vitabu.
 
Hahaha, mleta mada ni muongo sana probably atakuwa na stress ama kabaniwa kuhitimu masomo yake sasa anamaliza stress.

Mkuu katika jambo ambalo haliwezekani ni kusoma vitabu 400 vya wana mahesabu alafu ukakosa angalau 100 vyakukosoa na kwa nature ya uandishi wako lazima ungekuja kuwakosoa humu humu JF.

Mkuu haihitaji kuwa nguli wa hesabu ili ujenge nyumba 3 kwa mwaka mmoja hii argument yako ni kichekesho sana mkuu.

Jambo lililo wazi ni elimu yoyote inahitaji foundation hauwezi ukaponda shule alafu ukadhani utapata elimu bora sehemu tofauti na shule, kumbuka shule inaweza kuwa sehemu maalumu yenye majengo yake au kutoka kwa kiongozi wako wa maarifa.

Nadhani utakubaliana na mimi kuwa kujifunza na kusoma kunahitaji nidhamu.
 
Hapo inategemea na lengo lako binafsi ni nini kama kuajiriwa au kusaka maarifa
 
IMEKAA VIZURI..MWAKA JANA NILISOMA VITABU KAMA 60 HIVI NON FICTION..VILINIFUNGUA SANAA
 
Ameelezea upande wake..wewe waweza chagua wako
 
Kweli kabisa
 
LIKUD nakuunga mkono kwa 100% kuhusu kusoma vitabu kuliko kuwa hata na PHD. Mie nimesoma chuo fulani hapa TZ masomo ya Engineering. Kuna Tutorial Ass mmoja mstaafu kwa maana alikuwa na Degree moja tu ya Engineering alikuwa anatufundisha. Yeye katika maisha yake anakwambia mbali na kula kila siku lazima asome hesabu kila siku. Yaani na degree yake moja lakini wenye PHD walikuwa wanamkimbia kabisa. Maana masomo aliyokuwa anayakata ni yale ambayo wengine wanakimbia.
Na siyo hesabu tu, yeye anasoma vitu vyote ambavyo vipo kwenye tasnia yake. Kwakifupi anakwambia ana maisha mazuri sana kupitia kujisomea tu kwakuwa ana solve problems nyingi sana.
 
Mathematics is a sacred knowledge
 
Nin haja ya kujua namba kiasi hiko na unaishia kujenga tu nyumba? Maana kama nyumba hata ambao hawajasoma vitabu wanazo zaidi ya hapo. Nazan wote ni utumwa kusoma vitu vya watu hata kuongeza elimu. Njia bora iliyobaki ni kutuminisha uwezo wako hadharan kwa vitendo na kufanya yale wanaojua hesabu walifanya. Tengeneza formula zako au zilizopo boresha au saidia kwa lolote vile watu wajue hesabu. E=mc2 aliwah kusema kujuwa kama unawezo mkubwa ni pale unaweza mfundisha mtoto wa miaka sita na akakuelewa bila shiida yoyote.
 
Mkuu siwezi kupingana na wazo lako bt ukweli unabaki palepale kwamba hesabu ndio mama wa maarifa yote duniani
 
Kaka kujenga nyumba tatu Kali jijini darusalama ndani ya mwaka mkoja only kwa kujua hesabu wewe unaona ni kitu kidogo hicho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…