Kufanya mazoezi barabarani hasa kukimbia sio hatari kiafya?

Bakulutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2011
Posts
2,557
Reaction score
1,787
Miaka ya nyuma nilikuwa nafanya mazoezi ya kukimbia barabarani mara kwa mara siku moja tukiwa tunapiga stori na rafiki yangu yeye ni “Dental Specialist” pale Muhimbili akaniambia hadhani kama kukimbia barabarani hasa hizi barabara zetu magari mengi, unavuta punzi ya moshi wa magari, unapisha na magari kwa ukaribu sana ambapo pia sio salama sana mfano ukijikwaa bahati mbaya unaweza angukia barabarani na ukakanyagwa na gari.

Nini maoni yako?
 
Mwaka huu early July i think kama kumbukumbu zangu ziko sawa Mwanza walikufa watu 3+ kwa kugongwa na gari wakati wakifanya mazoezi barabarani.

Huwa naona ni kama watu kutafuta sifa tu maana nchi yetu barabara mbovu zipo kila mahali kwanini wasiende kukimbia huko wanaenda kupishana na magari barabarani kwenye lami kuwaonyesha wanaopita na magari yao kwamba hata wao wana magari yao ila wameamua kuyapaki ili kupunguza mafuta.
 
Masikini anakimbia barabarani na sinia la ndizi ili kujipatia kipato tajiri anakimbiza kitambi barabarani kupunguza mafuta na magonjwa ya moyo...

This world is not our home 🤔🤔🤔
Daaahhh!!! Huu ni ukweli mchungu. 🤭
 
Ni kweli barabarani ni hatari kwasababu ya magari. Mwanariadha Simon Robert akiwa kwenye kiwango chake cha juu alipoteza maisha mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa kugongwa na gari huko Arusha wakati akifanya mazoezi. Pia mazoezi ya kwenye lami yanaleta injuries kirahisi sana kwenye miguu. Kwa mlioko mijini ninawashauri nendeni viwanjani muwe mnazunguka uwanja. Wale wa Dar mnaweza kwenda beach pia. Mazoezi ya uwanjani ni mazuri kwasababu pia mnakutana wengi hivyo kunakuwa na mambo ya networking. Mimi nilikuwa naendaga Gym fulani maeneo ya Ilala ila nikaacha baada ya kuchukizwa na kitendo cha kina dada fulani kuja gym wamevaa mavazi ya kujifunika badala ya yale yaliyozoeleka.
 
Ndio ni hatari, kwa sababu.

Inasabibisha wamiliki wa nyumba( landlords) wapandishe kodi.
 
Miaka ya nyuma nilikuwa nafanya mazoezi ya kukimbia barabarani mara kwa mara siku moja tukiwa tunapiga stori na rafiki yangu yeye ni “Dental Specialist” pale Muhimbili akaniambia hadhani kama kukimbia barabarani hasa hizi barabara zetu magari mengi, unavuta punzi ya moshi wa magari, unapisha na magari kwa ukaribu sana ambapo pia sio salama sana mfano ukijikwaa bahati mbaya unaweza angukia barabarani na ukakanyagwa na gari.

Nini maoni yako?
Mkuu nina zaidi ya miaka ishirini nakimbia road still niko fit.
 
Ni kweli barabarani ni hatari kwasababu ya magari. Mwanariadha Simon Robert akiwa kwenye kiwango chake cha juu alipoteza maisha mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa kugongwa na gari huko Arusha wakati akifanya mazoezi. Pia mazoezi ya kwenye lami yanaleta injuries kirahisi sana kwenye miguu. Kwa mlioko mijini ninawashauri nendeni viwanjani muwe mnazunguka uwanja. Wale wa Dar mnaweza kwenda beach pia. Mazoezi ya uwanjani ni mazuri kwasababu pia mnakutana wengi hivyo kunakuwa na mambo ya networking. Mimi nilikuwa naendaga Gym fulani maeneo ya Ilala ila nikaacha baada ya kuchukizwa na kitendo cha kina dada fulani kuja gym wamevaa mavazi ya kujifunika badala ya yale yaliyozoeleka.
Mkuu walikuwa wanakuja wamevaa mavazi ya kujifunika🤔 kila mtu akivaa nguo si kajifunika, au
 
Ile barabara ya kuelekea mweka wildlife college ni nyembamba sana ila watu wanafanya mazoezi huko. Ni risk sana.
 
Barabara kubwa ni hatari
Mnooo.... Mi nakimbiaga barabara za mitaani nikikunja Kona zangu kadhaa nikazungula block narudi ...nilishakoswakoswa kipindi nipo chuo SAUT kwenye Ile Kona pale kama unashuka karibu na nyegezi seminari ATM kwenda malimbe hatari sana ,nyingine nikakoswa na gari ikaingia mtaroni pale bondeni..... Nilimheshimu barabara sikurudia Tena ...nkajisemea tu mara ya tatu "ntapandwa mbegu au kilema"....
 
Pole sana mkuu, kuzunguka uwanja nayo ni nzuri pia kwa wale ambao wapo karibu na viwanja vya mpira.
 
Napokaa mpaka ground ni kama km4-5 uzuri mji umepangwa so nakimbia tu barabara za kitaa alfajiri na usiku nilipata gap ....
 
Back
Top Bottom