Kufanya scrub kuna shida yoyote kiafya?

Observer2010

Senior Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
195
Reaction score
44
Kwenye salun nyingi siku hizi kuna hii huduma ya scrab. Tukiangalia kwa upande wa afya mara nyingi mtu akitoka kunyoa especially ndevu kunakuwa na vijimichubuko flani, baada ya kunyoa akienda kufanyiwa scrab na wale mabinti ambao majority huwa ni mapepe. Sasa kama huyo anayekufanyia scrub ana vijimichubuko mkononi, hv maambukizi ya magonjwa kama ngoma si ni more likely kutokea ?

Wadau tusaidiane katika hili.
 

Mimi Scrab ananifanyiaga Wife na wewe Makushauri kama ni Mpenzi wa Mambo hayo basi Mwambie wife wako akusaidie
 
Mambo ya kuiga ni mabaya sana, mazingira ya Berber Shops zetu hapa Bongo yanaendeshwa kienyeji na pia vi-binti ambavyo hata vifaa vya kufanyia scrub havina hata afya zao tuu............ inaonyesha kwa 'culture' ya sasa hivi wanaofanya scrub ni mabinti waliokosa kazi na mwelekeo wa maisha.

Mpe uso mkeo au-Scrub vinginevyo hizi Berber Shop ni Kiama.........................MDONDO HUOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
 
mapoudaaa....scrub fanya mwenyewe wewe, nunua kopo tumia taratiiib.
 
Kuuliza si ujinga ndugu zangu wana JF, kufanya scrub kuna shida yoyote kiafya?
[h=2]
[/h]
 
Scrub si mbaya kama unatumia vitu halisia vya kufanya hivyo kama parachichi, ila zile products tunazonunua angalia zimetengenezwa na nini epuka chochote chenye kemikali mbaya kama hydoquinone.. pia scrub usipende kujisugua kupitiliza ifanye kama massage, na usikae nayo sana mwilini isizidi dk 5.
 

namanisha hizi za kwenye masaluni za chenga chenga
 
Tumia vitu asili kama liwa ni nzuri haina madhara

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Kuuliza si ujinga ndugu zangu wana JF, kufanya scrub kuna shida yoyote kiafya?
Mkuu Amavubi,

Kitendo cha kufanya scrub kibaolojia kinaitwa exfoliation yaani to remove dead skin from the surface of a skin. Kila siku cells za ngozi ya juu zinakufa na kuwa replaced na cells mpya za ngozi, hivyo scub ndio kitendo cha kuondoa hiyo hizo dead cells.

  1. Kwanza inatakiwa kufanywa na natural products ambazo ni rich in protein, Wazaramo kiasili waliifanya kwa kutumia mapumba!. binti akiishapata mchumba, aliwekwa ndani na kusiguliwa kwa mapumba. Watu wa Pwani kama Wanzanzibari, wao walitumia machicha ya nazi. Product maarufu sana ni apricot, cocoa, karanga, pera, parachichi, papai bichi, soya, asali mbichi, etc. Nyingi ya products katika hizi saloon zetu sio!. Lengo la matumizi ya hizi natural products ni ku replenish skin mara baada ya kuibandua hiyo dead skin, ngozi iliyobaki inahitaji virutubisho kubaki na rich skin, heathy, radiant skin.
  2. Inabidi ifanywe gently, softly and with a defined patten, scrub ikifanywa kwa nguvu mho baada ya kuibandua dead skin ile new skin ni very sensitive to scratch, hivyo wengi hujikuta wameichubua na ngozi mpya, ukisafishwa utasikia muasho kama wa mchubuko. Wengi wa wale wadada kwenye nyingi ya saloon zetu sio wataalamu kivile, hivyo wengi wetu tunaishia kuchubuliwa, na wengine wanatufanyia scrubs za kiwizi wizi tuu ili sio tuu watuibie hela, bali hadi "kuibiwa!".
  3. Exfoliation ni process inayotokea kwenye mwili mzima, ila wengi wetu wana concentrate na usoni tuu!. Ukienda saloon za massage, au nyumba za massage, unaweza kufanyiwa full body scrub, hivyo mwali mzima kufanyiwa exfoliation.
  4. Inatakiwa kufanywa after a certain period of time kama once a month, ili kuipa nafasi ngozi iliyopo ikufe na sio kuifanya weeky. watu wanaa overdo scrub wanapata madhara na hawana tofauti na wanaojichubua!.
  5. Moja ya saloon ambayo I highly recommend kwa wanaume kwa kufanya proper scrub kutumia natural products ni BM pale Kinondoni. Fullbody scrub ni ile nyumba ya massage pale Kinondoni opposite Muslim, Traquilizer. Kuna Saloon ya G2 pale Sinza nao wanajitahidi kiasi chake, tatizo la Sinza ni "wadada wezi!".
Pasco
 
Pasco, epuka wizi, nenda kwa professionals. Na wasiwasi wangu wa huko knondoni na sinza ni usafi. Hiyo process ya exfoliation inafungua pores zote na ni rahisi sana kupata infections. Na katika ulivyovitaja hapo, umesahau sea salt scrub. Asante kwa somo zuri rafiki.
 
Last edited by a moderator:
King'asti, asante kwa hii, hiyo sea salt inafanywa wapi?.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…