Kufariki na Kufariki Dunia

Kufariki na Kufariki Dunia

Makoye Matale

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2011
Posts
6,491
Reaction score
2,104
Wana JF nawasalimu sana katika Jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya salamu hizo leo nimekuja na kamada kadogo kabisa katika hili jukwaa la lugha.

Watu wengi wamekuwa na maswali mengi, mtu anapokufa wasemeje; wengine wamekuwa wakisema 'amefariki', wengine wanasema 'amefariki dunia', kwa kuangalia makundi haya baadhi ya watu wameshindwa kufahamu hasa ni kundi lipi liko sahihi.

Nimefuatilia na kugundua kuwa: Neno 'kufariki' chanzo chake siyo 'kufa' bali ni 'faraka' yaani kuachana na ...; mfano marafiki wawili waliopendana wakaamua kuvunja urafiki basi huitwa 'wamefarakana' yaani wameachana! Hivyo basi mtu anapoishi duniani anakuwa ameambatana na dunia, pale mtu huyo anapoachana na dunia basi anakuwa 'amefarakana' na hiyo dunia au ametengana na hiyo dunia hivyo ni sahihi kusema 'amefariki dunia' na siyo kuishia tu kwamba 'amefariki' ambapo huacha swali kwamba 'kafariki nini'?

Kwa upande mwingine neno 'kufariki' linaweza kutumiwa kwa mtazamo huu: Mtu ambaye ameishi Dar es Salaam na sasa ameuhama Dar es Salaam anaenda mji mwingine; atakapokuwa ameuhama Dar es Salaam haitakuwa makosa kusema mtu huyo 'amefariki Dar es Salaam'.
 
Wana JF nawasalimu sana katika Jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya salamu hizo leo nimekuja na kamada kadogo kabisa katika hili jukwaa la lugha.

Watu wengi wamekuwa na maswali mengi, mtu anapokufa wasemeje; wengine wamefukuwa wakisema 'amefariki', wengine wanasema 'amefariki dunia', kwa kuangalia makundi haya baadhi ya watu wameshindwa kufahamu hasa ni kundi lipi liko sahihi.

Nimefuatilia na kugundua kuwa: Neno 'kufariki' chanzo chake siyo 'kufa' bali ni 'faraka' yaani kuachana na ...; mfano marafiki wawili waliopendana wakaamua kuvunja urafiki basi huitwa 'wamefarakana' yaani wameacha! Hivyo basi mtu anapoishi duniani anakuwa ameambatana na dunia, pale mtu huyo anapoachana na dunia basi anakuwa 'amefarakana' na hiyo dunia au ametengana na hiyo dunia hivyo ni sahihi kusema 'amefariki dunia' na siyo kuishia tu kwamba 'amefariki' ambapo huacha swali kwamba 'kafariki nini'?

Hiyo ina furahisha. Mtu anahama Tanzania, unasema amefariki Tanzania.

Ila sasa tukirudi kwenye kufariki dunia, Je neno dunia maana yake nini?
Ni pamoja na huu udongo kwenye ardhi tunamoishi?
Kama ndivyo, mtu akizikwa humu humu duniani, basi hajafariki dunia. Kwa sababu bado yupo duniani.

[/COLOR]

Ukizikwa ndugu yangu bado unakuwa umefariki dunia,kwani maisha duniani hutakuwa nayo tena, hakuna maisha chini ya ardhi ( kwa sisi wenye imani ya dini). Kwa hiyo kufariki ni kuondoka sehemu unayoishi kwenda sehemu nyingine,lakini kufariki dunia ni kukosa uhai.
 
Asante bwana Nyamanoro.
Hapo kwenye blue, ina maana kwa sisi tuanoamini mizimu, na kuamini kuwa ukizikwa bado unakuwepo hai kwa namna fulani, basi sisi HATUFARIKI DUNIA, hii ni kwa mujibu wa imani yangu..
 
Hata kwa imani yako ukifa utakuwa umeifariki dunia...! Hiyo imani ya kusema kuwa mizimu huja duniani kutembelea jamaa si kweli, ila watu huwa wanakwenda aidha makaburini au kwenye mapango, au kwenye miti mikuwa ambapo wana amini kuwa hapo ndipo mizimu ipo, yaani ni sawa na kwenda kibanda cha simu na kuwasiliana na mtu aliye upande wa piili wa dunia.
 
Wana JF nawasalimu sana katika Jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya salamu hizo leo nimekuja na kamada kadogo kabisa katika hili jukwaa la lugha.Watu wengi wamekuwa na maswali mengi, mtu anapokufa wasemeje; wengine wamefukuwa wakisema 'amefariki', wengine wanasema 'amefariki dunia', kwa kuangalia makundi haya baadhi ya watu wameshindwa kufahamu hasa ni kundi lipi liko sahihi.Nimefuatilia na kugundua kuwa: Neno 'kufariki' chanzo chake siyo 'kufa' bali ni 'faraka' yaani kuachana na ...; mfano marafiki wawili waliopendana wakaamua kuvunja urafiki basi huitwa 'wamefarakana' yaani wameacha! Hivyo basi mtu anapoishi duniani anakuwa ameambatana na dunia, pale mtu huyo anapoachana na dunia basi anakuwa 'amefarakana' na hiyo dunia au ametengana na hiyo dunia hivyo ni sahihi kusema 'amefariki dunia' na siyo kuishia tu kwamba 'amefariki' ambapo huacha swali kwamba 'kafariki nini'? Kwa upande mwingine neno 'kufariki' linaweza kutumiwa kwa mtazamo huu: Mtu ambaye ameishi Dar es Salaam na sasa ameuhama Dar es Salaam anaenda mji mwingine; atakapokuwa ameuhama Dar es Salaam haitakuwa makosa kusema mtu huyo 'amefariki Dar es Salaam'.
Bukibuji amegariki kitanda......Means Bujibuji kakiacha kitanda chake na kuingia kwenye purukushani, Kiswahilii bwana iz vele entelestingi langweji
 
Japo kusema "kufariki dunia" ndio sahihi, lakini matumizi ya muda mrefu na ya watu wengi ya "kufariki" yamekwishajihalalisha.

Hivyo kihalisia Kufa = Kufariki dunia = kufariki.
 
Hata kwa imani yako ukifa utakuwa umeifariki dunia...! Hiyo imani ya kusema kuwa mizimu huja duniani kutembelea jamaa si kweli, ila watu huwa wanakwenda aidha makaburini au kwenye mapango, au kwenye miti mikuwa ambapo wana amini kuwa hapo ndipo mizimu ipo, yaani ni sawa na kwenda kibanda cha simu na kuwasiliana na mtu aliye upande wa piili wa dunia.

Mkuu ekspata, mbona unatoa tafsiri tofauti ya imani yangu?
Mimi naamini mtu ukifa roho yako bado ipo hai, na unaendelea kuwepo hapa duniani. Si lazima iwe pale ulipozikwa, hata nyumbani ulipokuwa unaishi, unaendelea kuwepo tu. Ila unakuwa free zaidi kwenye movement.
 
Asante bwana Nyamanoro.
Hapo kwenye blue, ina maana kwa sisi tuanoamini mizimu, na kuamini kuwa ukizikwa bado unakuwepo hai kwa namna fulani, basi sisi HATUFARIKI DUNIA, hii ni kwa mujibu wa imani yangu..

Kumbe nyie mnaoamini mizimu dunia yenu iko chini ya ardhi?
 
Dunia ni nini na ardhi ni nini? unaweza kutenganisha ardhi kutoka kwenye dunia? Kwa mtazamo wangu ni hapana. Kwa hiyo hata nikizikwa ardhini, ninakuwa bado nipo duniani.
 
Mkuu ekspata, mbona unatoa tafsiri tofauti ya imani yangu?
Mimi naamini mtu ukifa roho yako bado ipo hai, na unaendelea kuwepo hapa duniani. Si lazima iwe pale ulipozikwa, hata nyumbani ulipokuwa unaishi, unaendelea kuwepo tu. Ila unakuwa free zaidi kwenye movement.
Mkuu, unakuwa kwenye dunia nyingine kabisa, si hii tena.
 
Wana JF nawasalimu sana katika Jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya salamu hizo leo nimekuja na kamada kadogo kabisa katika hili jukwaa la lugha.

Watu wengi wamekuwa na maswali mengi, mtu anapokufa wasemeje; wengine wamefukuwa wakisema 'amefariki', wengine wanasema 'amefariki dunia', kwa kuangalia makundi haya baadhi ya watu wameshindwa kufahamu hasa ni kundi lipi liko sahihi.

Nimefuatilia na kugundua kuwa: Neno 'kufariki' chanzo chake siyo 'kufa' bali ni 'faraka' yaani kuachana na ...; mfano marafiki wawili waliopendana wakaamua kuvunja urafiki basi huitwa 'wamefarakana' yaani wameacha! Hivyo basi mtu anapoishi duniani anakuwa ameambatana na dunia, pale mtu huyo anapoachana na dunia basi anakuwa 'amefarakana' na hiyo dunia au ametengana na hiyo dunia hivyo ni sahihi kusema 'amefariki dunia' na siyo kuishia tu kwamba 'amefariki' ambapo huacha swali kwamba 'kafariki nini'?

Kwa upande mwingine neno 'kufariki' linaweza kutumiwa kwa mtazamo huu: Mtu ambaye ameishi Dar es Salaam na sasa ameuhama Dar es Salaam anaenda mji mwingine; atakapokuwa ameuhama Dar es Salaam haitakuwa makosa kusema mtu huyo 'amefariki Dar es Salaam'.

Upo sahihi mkuu ila hapo kwenye red hawezi kuwa amefariki Dar es Salaam hadi ithibitike kuwa mtu huyo hatarudi Dar es Salaam kamwe. Kwa maelezo zaidi ni kuwa "Kufariki eneo fulani" ni kuhama eneo hilo na kwenda eneo lingine pasipo kurudi kamwe eneo la awali.
 
Japo kusema "kufariki dunia" ndio sahihi, lakini matumizi ya muda mrefu na ya watu wengi ya "kufariki" yamekwishajihalalisha.

Hivyo kihalisia Kufa = Kufariki dunia = kufariki.

Hii ni 'common mistake'.
 
Nadhani kufariki kunatokea hapa DUNIANI kwa hivyo nionavyo mimi kusema kufariki yatosha.
Mfano nitakaokupigia ni Kukoga na kukuga maji (Kwa kawaida binadamu wote ninaowafahamu huwa wanatumia maji katika kutimiza adhma yao ya kujiswafisha mwili mzima....kukoga ni sahihi).
Kuna mtaalamu wa totologi aweza akatoa mwnga zaidi
 
Upo sahihi mkuu ila hapo kwenye red hawezi kuwa amefariki Dar es Salaam hadi ithibitike kuwa mtu huyo hatarudi Dar es Salaam kamwe. Kwa maelezo zaidi ni kuwa "Kufariki eneo fulani" ni kuhama eneo hilo na kwenda eneo lingine pasipo kurudi kamwe eneo la awali.

nafahamu sote sisi tulihama toka matumboni mwa mama zetu, na hatutorudi tena huko. kwa tafsiri hii manake, badala ya kutumia kuzaliwa tunaweza sema mtoto amefariki toka tumboni kwa mama yake na sote tukaelewa kuwa amezaliwa?
 
Hiyo ni sawa tu. Unaweza ukatumia tungo hasi kuelezea hali chanya. Mfano mtu mmoja akisema: "Mkeshaji hana roho mbaya" na mwingine akasema "Mkeshaji ana roho nzuri", hawa wote watakuwa wamezungumza kitu kimoja kwa kutumia maneno tofauti; mmoja ametumia sentensi hasi na mwingine ametumia sentensi chanya.
Mfano mwingine ni ule wa haki na wajibu. Haki ya mtu mmoja huwa ni wajibu wa mtu mwingine, na wajibu wa mtu huyu huwa ni haki ya mtu mwingine. Ni kitu kimoja chenye maana moja kwa pande mbili tofauti.

Unapofariki eneo moja ni kuwa unazaliwa eneo jingine. Mtu anayefariki tumboni mwa mama yake ni kuwa anazaliwa duniani (endapo tu atoka akiwa hai), vinginevyo atakuwa amefariki tumboni mwa mama yake na atakuwa amefariki dunia vilevile.
 
Mkuu kwa hiyo ni sawa nikisema mwanangu amefariki toka tumboni kwa mama yake salama? hapo ntaeleweka kuwa mwanangu kazaliwa akiwa hai na afya njema? nadhani sikubaliani sana na maana hiyo, hata kama ni maana hasi. sidhani kama hata ntaeleweka. nadhani ntaonekana chizi au namchulia mwanangu kifo
 
Back
Top Bottom