Kuficha pesa Uswisi, ujinga wa kiwango cha juu

Umenisoma na michango ya wengine kabla hujachangia?
Umesoma post za BAK na Kafara? Chukua muda upite huko tafadhali

ningekuwa na uwezo ningemuamsha marehemu mobutu seseseko kuku wa zabanga aje amuelezee jamaa jinsi
waswisi walivyomnyima visa ya kuingia uswiss kufuata pesa na mali yake. hatimaye mobutu ilibidi akahifadhiwe morocco.
 
ningekuwa na uwezo ningemuamsha marehemu mobutu seseseko kuku wa zabanga aje amuelezee jamaa jinsi
waswisi walivyomnyima visa ya kuingia uswiss kufuata pesa na mali yake. hatimaye mobutu ilibidi akahifadhiwe morocco.

Na zilikuwa zake lakini za wizi, ukinipa kitu cha wizi nikufichie huna haki ya kisheria kukidai, kukurudishia itategemea huruma yangu tuu

Mara zote watu wanafikiri hizi ni stori za kufikirika na kwamba ni kitu kisichowezekana, lakini watu wamepigwa za uso na waswisi na bado wataendelea kupigwa

Ishu ya Escrow kulikuwa na uwezekano kabisa wa kwenda kufanyia ile miamala Uswisi ambako hakuna kelele wala hatari ya kujulikana kwa urahisi, lakini wanajua fika nini kingetokea! Hivyo wakaamua kujitoa ufahamu na kujilipua hapahapa nchini LIWALO NA LIWE lakini kila mtu achukue chake hapahapa
NB:Nazungumzia ile miamala mikubwa kuanzia USD million moja
 

waswisi inapokuja suala la pesa ni hatari sana. ngoja jamaa wapigwe halafu washindwe hata mahali pa kushitaki.
 
In May 2014, Rostam Azizi sold a 17% stake in Vodacom Tanzania, the country's largest mobile phone operator, to South Africa's Vodacom Group for $250 million. He still owns nearly 18% of Vodacom Tanzania through Cavalry Holdings, an investment company registered in Jersey, a known tax haven. His other assets include Caspian Mining, the largest contract mining firm in Tanzania, which performs work forMore »


Sometimes wanaweka hela nje legally,bongo makodi kibao
 

Illegal money deposited legally! Sidhani kama among all people Rostam anaweza kuclaim kwamba utajiri wake wote kaupata kihalali...! NEVER
 
mshana jr wengine wameficha huku hela,kamwambie mkuu abadilishe noti fasta maana mzunguko wa hela ni mdogo saaana
 
ningekuwa na uwezo ningemuamsha marehemu mobutu seseseko kuku wa zabanga aje amuelezee jamaa jinsi
waswisi walivyomnyima visa ya kuingia uswiss kufuata pesa na mali yake. hatimaye mobutu ilibidi akahifadhiwe morocco.
SAFI SANA,,,,,,,Dhulma huwa mwisho wake ndo huo!!!
 
Tokyo40 tuonyeshe weledi na hekima zetu katika kuchangia, tuepuke kutumia lugha ngumu na za kuudhi
TUMSAMEHE BURE. hao ndiyo WATZ wezi wanatetea wizi wao. Mtu aliyechuma hela yake kihalali hawezi ihifadhi Uswisi kwenye masharti magumu namna hiyo. wezi wa mali za umma huwa nio wakali. Nadhani unakumbuka jinsi walivyopambana kuhakikisha wanahalalisha wizi wao mpaka kwenye ile katiba ya Chenge na Sita
 
Acha porojo, mkulima gani wa kahawa/chai/mahindi ataweka pesa zake Uswizi kunakonyima wanafamily urithi? Msitufanye mazuzu, ndiyo maana tunadharaulika, kwa ujinga huu. Halafu kesho asb, unaenda na bakuli kuomba msaada huko. Kama busara yako ndiyo iko hivi, ni moja ya hasara kwa nchi
 

Kama hufahamu jinsi benki za kimataifa zinazofanya kazi, uliza.

Sio kila mtu ameishia darasa la saba hapa. Labda wewe hufahamu au hujatembea nje ya Tanzania lakini kama kawaida ya wengi hapa JF, unafikiri kila kitu kwa akili ya Kijamaa na Kujitegemea. Sio kosa lako, ni elimu uliyoipata Tanzania. Watu kama nyinyi mnafikiri kila benki ni kama NBC kwa sababu ndio dunia mnayoijua.

Nina uhakika hujawahi hata kuisikia Wegelin & Co., mpaka uliposoma hapa, lakini unajitia unajua kila sharia za benki za kimataifa.

Unaweza kuweka kithibitisho chako kinachoonyesha kuwa wanafamilia hawapati urithi katikai benki za Uswisi?
Nitasubiri kithibitisho chako na kama hutaleta, WEWE ndiyo utakua unaleta porojo za Vijiweni.
.
 
Wewe jamaa una akili sana. Contrary hao wanoficha pesa huko wana ujinga uliotukuka, yaani ni bora ufungue akaunti hata 200 kwenye nchi tofauti tofauti then uwe unawekeza kidogo kidogo kwenye miradi nchini kwako ili nao wainuke kiuchumi, yaan roho mbaya tu!
 

mwakaboko,

Nilijua tu hutaweza kuleta kithibitisho cha wanafamilia kunyimwa urithi kiatika benki za Uswisi.

WEWE ndio mwenye porojo na hadithi za vijiweni.

Ukipenda kujua jinsi wanafamilia wanavyoweza kupewa urithi wao katika benki za kimataifa, niulize tu, nitakufahamisha process BURE.
 
Hatuzungumzii benki za kimataifa, twazungumzia Benki za Uswisi. Kiukweli kuweka pesa nchi za nje, ni ujinga wa Kitanzania. Rais wa Marekani hana akaunti huku Bongo. Ni ujinga tu, kujenga taifa la mwenzako huku la kwako likibaki ombaomba.
 
Waambie wazi wazi labda wataelewa, ni ujinga unaharibu kwenu unahamia kwa wenzako waliojenga kwao.
 
Hatuzungumzii benki za kimataifa, twazungumzia Benki za Uswisi. Kiukweli kuweka pesa nchi za nje, ni ujinga wa Kitanzania. Rais wa Marekani hana akaunti huku Bongo. Ni ujinga tu, kujenga taifa la mwenzako huku la kwako likibaki ombaomba.

Wewe ni ombaomba wa akili.

Benki za Uswisi ni za Kimataifa, kwa kuwa hujui unaonyesha jinsi gani ilivyo mweupe kichwani.

Nasubiri utuonyeshe chanzo kuwa hawatoi pesa za urithi kama ulivyodai katika bango lako.

Nenda nchi zote zenye uchumi wa kati na kuendelea, utakuta benki za Uswisi na za nchi nyingine. Kutojua hilo inaonyesha wazi hujui kitu chochote kuhusu biashara za kibenki za kimataifa.

Maisha ya Obama na pesa zake hazinihusu. Maamuzi ya kuweka pesa benki yoyote duniani ni ya binafsi.

Hata matajiri wa Marekani na ulaya wanaweka pesa nje ya nchi ili kupata riba bora na kuepuka kulipa kodi kubwa. Sidhani kama ulijua hili.

Kila mwaka raia wa Marekani zaidi ya 1000 wanaukana uraia wao ili wapunguze kodi katika mapato yao nje ya nchi.

Mmoja wao ni bilionea Edward Saverin wa Facebook. Kaukana uraia wa Marekani na kwenda Singapore ambapo pesa zake zitatozwa kodi ndogo.

Ni ujinga wa hali ya juu kutegemea wananchi waweke pesa zao katika nchi ambayo ina historia ya kunyanga'anya mali za watu, kutaifisha mabenki na biashara na kutoheshimu demokrasia.

Kama unasubiri benki za Tanzania kujaa pesa za Watanzania na akina Obama, utasubiri sana.

Mambo ya uzalendo ni katika vitabu vya siasa za kijamaa tu. Binadamu kwanza anajishibisha yeye, awe Tanzania, Marekani au Japan.

Hata Nyerere hakuishi Kijamaa kama alivyotaka wananchi wake waishi. Nguo zake zilitoka nje (China) wakati wananchi vijijini wanatembea uchi, alijitibu nje ya nchi na kufia kwa Mkoloni badala ya kuonyesha "uzalendo" wa kutibiwa Muhimbili kama wananchi wake.

Na hii tabia ya jinsi gani binadamu anafanya maamuzi ya maisha yake, inafundishwa katika vyuo vyote bora duniani. Kama umefundishwa kuwa uzalendo unakuja mwanzo, umeongopewa.

Nakushauri ujisomee kabla ya kuandika vitu ambavyo huvielewi.
 
Takukuru yetu inasema itafuatilia pesa iliyofichwa uswisi sidhani kama watazipata
 
ningekuwa na uwezo ningemuamsha marehemu mobutu seseseko kuku wa zabanga aje amuelezee jamaa jinsi
waswisi walivyomnyima visa ya kuingia uswiss kufuata pesa na mali yake. hatimaye mobutu ilibidi akahifadhiwe morocco.
Jamaa wako very strategic. Wana pesa yako, afu wanakunyima VISA! Daah, lazima ufe kwa pressure ama uwehuke!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…