Hatuzungumzii benki za kimataifa, twazungumzia Benki za Uswisi. Kiukweli kuweka pesa nchi za nje, ni ujinga wa Kitanzania. Rais wa Marekani hana akaunti huku Bongo. Ni ujinga tu, kujenga taifa la mwenzako huku la kwako likibaki ombaomba.
Wewe ni ombaomba wa akili.
Benki za Uswisi ni za Kimataifa, kwa kuwa hujui unaonyesha jinsi gani ilivyo mweupe kichwani.
Nasubiri utuonyeshe chanzo kuwa hawatoi pesa za urithi kama ulivyodai katika bango lako.
Nenda nchi zote zenye uchumi wa kati na kuendelea, utakuta benki za Uswisi na za nchi nyingine. Kutojua hilo inaonyesha wazi hujui kitu chochote kuhusu biashara za kibenki za kimataifa.
Maisha ya Obama na pesa zake hazinihusu. Maamuzi ya kuweka pesa benki yoyote duniani ni ya binafsi.
Hata matajiri wa Marekani na ulaya wanaweka pesa nje ya nchi ili kupata riba bora na kuepuka kulipa kodi kubwa. Sidhani kama ulijua hili.
Kila mwaka raia wa Marekani zaidi ya 1000 wanaukana uraia wao ili wapunguze kodi katika mapato yao nje ya nchi.
Mmoja wao ni bilionea Edward Saverin wa Facebook. Kaukana uraia wa Marekani na kwenda Singapore ambapo pesa zake zitatozwa kodi ndogo.
Ni ujinga wa hali ya juu kutegemea wananchi waweke pesa zao katika nchi ambayo ina historia ya kunyanga'anya mali za watu, kutaifisha mabenki na biashara na kutoheshimu demokrasia.
Kama unasubiri benki za Tanzania kujaa pesa za Watanzania na akina Obama, utasubiri sana.
Mambo ya uzalendo ni katika vitabu vya siasa za kijamaa tu. Binadamu kwanza anajishibisha yeye, awe Tanzania, Marekani au Japan.
Hata Nyerere hakuishi Kijamaa kama alivyotaka wananchi wake waishi. Nguo zake zilitoka nje (China) wakati wananchi vijijini wanatembea uchi, alijitibu nje ya nchi na kufia kwa Mkoloni badala ya kuonyesha "uzalendo" wa kutibiwa Muhimbili kama wananchi wake.
Na hii tabia ya jinsi gani binadamu anafanya maamuzi ya maisha yake, inafundishwa katika vyuo vyote bora duniani. Kama umefundishwa kuwa uzalendo unakuja mwanzo, umeongopewa.
Nakushauri ujisomee kabla ya kuandika vitu ambavyo huvielewi.