Kuficha pesa Uswisi, ujinga wa kiwango cha juu

Kuficha pesa Uswisi, ujinga wa kiwango cha juu

Anachokifanya Zitto ni michezo ya kisiasa hana mandate yeyote ya kudai zile pesa wala kuzirudisha sio zake hana asili nazo na hajaweka yeye! Yeye ni political opportunist anayejua vema udhaifu wa media za Tanzania! Hazihoji zinaandika tu kwakuwa kaongea Fulani

Utaratibu ni mgumu mno jamani na wenye gharama kubwa! Imagine Sani Abacha alithibitika pasipo shaka kuwa aliweka mabilioni kule lakini kuipata ile pesa Wanaigeria wameisotea kwa miaka 16!!!! Umri wa mtu huo, MIAKA 16; SIO MIAKA 6
...Inauma. Pesa ambayo ingewasaidia kwa namna Fulani wanaijeria wanayohusika nayo imeishia kueasaidia Waswisi...kwa sababu tu ya Ujinga na Uroho wa Viongozi wake!
Hivi kwa nini we we no kiongozi unayefanya mema kwa wananchi unaowaongoza kwa nini had I ufikie pa kujiona kuwa una Haki ya kuwaibia Wananchi wako na kutunza hela za wizi wako kwenye Mabenki ya Nje??
 
Hii in Uzi Mzuri sana hapo unaoumiza sana, Mkuu Mshana.
Nitakushukuru sana ukiufanya Mwema zaidi ukitueleza baadhi ya mitihani ambayo Mficha hela anayokumbana nayo Akitaka kudraw kwa mfano dola Milioni Moja take mwenyewe aliyoificha huko...ama tabu inaanza tu pale anapokufa?
 
Dah nimemkumbuka putini aliwahi kusema waafrika benki yao ni uswisi ,wanajenga USA,wanawekeza uk ,matembezi ni France ila wakifa wanazikwa afrika kwaiyo afrika ni makaburini inashangaza Sana.
 
Waulize wote walioficha kule kama waliweza ku draw hata dola laki 5 kwa mara moja...
Kuweka vigezo ni rahisi sana...! Nenda katoe sasa zittatumika taratibu zote za bank pamoja na IMTA (international money transfer act)
. Ni lazima ustate unaenda kuzifanyia nini
. lazima kuwe na mtu unayefanya naye biashara
. ni lazima kuwe na kitu kama proforma invoice
. ni lazima kuwe na kiwango maalum
Hapo ndipo wengi hugundua wamepigwa
Huwezi kufanya manunuzi makubwa wakati huna background ya biashara
Huwezi ku draw cash halafu ukaondoka nayo.. Kuna sheria za kimataifa za kiwango cha kutembea na cash
mbaya mbaya zaidi zile pesa hazina mrithi

Jr[emoji769]
 
PUTIN: AFRIKA HAITOKAA IWE HURU

"Afrika haitokaa iwe HURU. Waafrika wanawaamini Wazungu, Wamarekani na Wachina zaidi kuliko wanavyojiamini wao wenyewe....hawajiamini wao wenyewe hata kidogo.

Mzungu au mtu mweupe anafanya makosa Afrika tena makosa ya jinai ila hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu mamlaka za Afrika zinatutazama sisi weupe kama miungu, jambo ambalo liko mbali sana na ukweli.

Mtu mweusi (Mwafrika) anaweza kuteswa, kunyanyaswa na hata kuuawa kinyama Ulaya lakini hakuna mamlaka yoyote ya Afrika inayoweza kuuliza wala kuhoji.

Waafrika wamejikubali na kuamini kuwa wao ni watu DHAIFU wasio na tumaini haswa linapokuja suala la kupambana na Wazungu, Wamarekani na Wachina. Mzungu, Mmarekani au Mchina anaweza kumdhalilisha, kumtukana, kumpiga na hata kumuua Mwafrika katika ardhi ya Afrika tena kwenye nchi yake au nje ya Afrika na Viongozi wa Afrika wataliona hilo na kila mmoja atajiweka kana kwamba hakuona wala kusikia.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.

Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."

Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
Je ni kipi unaweza kuongeza kuhusu Afrika?

Quote
Dah nimemkumbuka putini aliwahi kusema waafrika benki yao ni uswisi ,wanajenga USA,wanawekeza uk ,matembezi ni France ila wakifa wanazikwa afrika kwaiyo afrika ni makaburini inashangaza Sana.
Uswizi: Mali za mtoto wa Rais wa Equatorial Guinea kupigwa mnada - JamiiForums

Jr[emoji769]
 
Waswisi ni wezi werevu, wanaishi kama peponi kwa pesa za wezi na kuhalalisha wizi wao wamejitungia sheria za kujilinda na kubariki wizi huo.

Wana mabilioni ya dola wanayafanyia biashara na miamala mbalimbali huku wamiliki wao wakiwa kimya tuli kabisa, hawaulizi kuhusu riba wala faida itokanayo na mapesa yao! Wataanzia wapi nao ni wezi?

Mtu anayesumbukia pesa yake, mfanyabiashara mwenye biashara zake halali kamwe hawezi kwenda kuficha pesa zake kule! Anajiamini kazipata kwa halali.

Waswisi wajanja wana utaratibu mzuri na salama sana unapotaka kuwapelekea pesa za wizi, hawashindwi kukodisha ndege kufuata mzigo popote ulipo, customer care yao ni nzuri sana kwenye hilo! Lakini kimbembe ni siku utakapotaka kuzichukua, utaambiwa kuna sheria za kimataifa za kusafirisha pesa utapewa utaratibu mgumu mno na wenye gharama kubwa wa kutoa hizo pesa

Pesa nyingi huishia mikononi mwao, ni pesa ya wizi kwahiyo hata kuhifadhi kwake ni kwa siri
Pesa ya Uswisi Haina mrithi
Signatory ni mmoja tu (muwekaji)
Haina mashahidi
Hizi pesa nyingi huishia huko huko kama mmiliki akifa au akifungwa

Na ikitokea nchi husika ikajua kuwa kiongozi/viongozi wake wameficha hela huko na wakadai hiyo hela utaratibu wake was kuipata nao ni mgumu mno tuneyaona kwa Sani Abacha wa Nigeria na wengineo

Hapa nchini tunaambiwa kuna watanzania kama mia hivi wameficha mapesa Kule! Hao imekula kwao nyingi zitaishia huko! Na hakuna mtu mwenye uwezo wa kwenda kuzirudisha ni porojo za kisiasa tuu
Sasa hapa mimi ninaona kama waswisi ni wazuri kwa yule aliyeibiwa na ni wabaya kwa yule aliyeiba! Maana kama wangelkuwa na utaratibu mzuri kwa aliyeiba, tungekuwa hatuna kitu sasa hivi, maana wezi wawili tu wanaweza wakafilisi Nchi milele. Waendelee na utaratibu huo kutusaidia sisi wanyonge ili tusiwe tunaibiwa kirahisi
 
PUTIN: AFRIKA HAITOKAA IWE HURU

"Afrika haitokaa iwe HURU. Waafrika wanawaamini Wazungu, Wamarekani na Wachina zaidi kuliko wanavyojiamini wao wenyewe....hawajiamini wao wenyewe hata kidogo.

Mzungu au mtu mweupe anafanya makosa Afrika tena makosa ya jinai ila hakuna hatua za kisheria zitakazochukuliwa dhidi yake kwa sababu mamlaka za Afrika zinatutazama sisi weupe kama miungu, jambo ambalo liko mbali sana na ukweli.

Mtu mweusi (Mwafrika) anaweza kuteswa, kunyanyaswa na hata kuuawa kinyama Ulaya lakini hakuna mamlaka yoyote ya Afrika inayoweza kuuliza wala kuhoji.

Waafrika wamejikubali na kuamini kuwa wao ni watu DHAIFU wasio na tumaini haswa linapokuja suala la kupambana na Wazungu, Wamarekani na Wachina. Mzungu, Mmarekani au Mchina anaweza kumdhalilisha, kumtukana, kumpiga na hata kumuua Mwafrika katika ardhi ya Afrika tena kwenye nchi yake au nje ya Afrika na Viongozi wa Afrika wataliona hilo na kila mmoja atajiweka kana kwamba hakuona wala kusikia.

Adui wa Mwafrika ni Mwafrika. Mwafrika mpe silaha, pesa au ahadi ya madaraka madogo tu kwa sharti moja tu la kumuua Mwafrika mwenzake, atamuua kinyama kuliko ulivyotarajia. Adui wa Mwafrika sio mzungu, sio Mmarekani wala sio mchina. Adui wa Mwafrika ni AKILI na fikra zake na ndio maana leo Wazungu, Wamarekani, Waarabu na Wachina wameitawala tena Afrika kwa kutumia dini, Elimu, uchumi, teknolojia, siasa na utamaduni.

Waafrika ni watu wanaochukiana na wasioaminiana na ndio maana Afrika haiwezi kuungana na haitokaa iungane kuwa na dola imara. Chuki ya wenyewe kwa wenyewe na utengano ndio inayowapa wakoloni wao nguvu ya kuendelea kunyonya rasilimali za Afrika."

Je unakubaliana na Rais Vladmir Putin?
Je ni kipi unaweza kuongeza kuhusu Afrika?

Quote
...Ukweli unaomiza Sana kwa Wana wa Nchi...lakini unaooneka kutowaumiza ama japo kuwafikirisha tu Viongozi wake Kiafrika. [emoji848][emoji848]
 
Sasa hapa mimi ninaona kama waswisi ni wazuri kwa yule aliyeibiwa na ni wabaya kwa yule aliyeiba! Maana kama wangelkuwa na utaratibu mzuri kwa aliyeiba, tungekuwa hatuna kitu sasa hivi, maana wezi wawili tu wanaweza wakafilisi Nchi milele. Waendelee na utaratibu huo kutusaidia sisi wanyonge ili tusiwe tunaibiwa kirahisi
Wangetusaidia sasa tukidai chetu michakato isiwe mirefu na yenye gharama kubwa

Jr[emoji769]
 
Wangetusaidia sasa tukidai chetu michakato isiwe mirefu na yenye gharama kubwa

Jr[emoji769]
Hivi zile Mali za Mugabe zilizopo Malaysia, UK na hongkong na za mobutu zilizopo ubelgiji,France na Swiss yakifa haya madikteta huwa zinakuwa Mali za watoto wao au za nchi.
 
Hivi zile Mali za Mugabe zilizopo Malaysia, UK na hongkong na za mobutu zilizopo ubelgiji,France na Swiss yakifa haya madikteta huwa zinakuwa Mali za watoto wao au za nchi.
Inategemea wamewekeza kwa majina ya nani na kama wosia unasemaje... Ninachojua ni zile za uswiss kuwa hazina mrithi

Jr[emoji769]
 
[emoji144][emoji144][emoji144]ila wametuibia

Jr[emoji769]
Hapana, wao hawajatuibia sisi ila tumejiibia sisi wenyewe halafu tukawapeekea wao watutunzie. Kwenye sheria za Nchi yetu kwa mfano, ukiingia mkataba wa kuuziana bang na mtui halafu akakudhulumu, ukienda kumshtaki mahakamani unakuwa wa kwanza kufungwa wewe uliyeenda kushtaki mahakamani!
 
Pesa ya Sani Abacha dola za marekani zinazozidi 250milioni zilikuwa kule, Gaddafi wa Libya ana mapesa yake kule mengi sana mtoto wa Wade naye pia anazo zinazofikia usd 220 hawa wote imethibitika pasi na shaka kuwa pesa ni zao, lakini serikali zao zimekuwa na wakati mgumu kuzidai au kurudishiwa

Uswisi wameweka taratibu ngumu mno, ni pesa ambazo hazina mrithi wala mirathi, wanazifanyia miamala wannazifanyia biashara wanapata faida kubwa lakini mwenye nazo hafaidiki chochote sanasana analipia gharama ya kuzitunza

Na inapotokea wakaamua kuzirudisha kwa serikali husika sio cash bali huzirudisha kwa njia ya miradi mbali mbali kama Barbara elimu na afya na makandarasi hutafutwa na wao wenyewe, mwisho wa Siku bado faida kubwa hurudi kwao, mradi ambao kwa mfano ungegharimu USD laki5 wao huleta makadirio ya milioni

Tunaitajirisha uswisi kwa rohombaya zetu na uchoyo uliopitiliza, Wananchi wetu wanakufa kwa kukosa huduma muhimu viongozi wanakimbizia mabilioni uswisi kuyaficha
Jamaa wana akili sana hawa
 
Back
Top Bottom