Kufifia kwa taasisi za serikali: Mfano TANROADS

Kipaumbele ni Zanzibar kwanza
 
Wewe ni mtumishi wa TANROADS sio bure maana una uchungu nayo sana
Kuna haja ya kutazama mwendo tunaouendea, kule mbele tutakwamisha kizazi chetu na kitaba njia panda. Tupaze sauti zetu tunapoweza kuwap viongozi wetu mwelekeo mzuri. Siku raisi akiondoka madarakani anakuwa ametua mzigo wake lakini huo mzigo unabebeka kwa yule anamwachia/
 
TANROADS UGANDA (UNRA) imevunjwa mwezi uliopita!

Kimsingi serikali iamue kama inataka hizi agencies na authorities ilizoziunda ziendelee lazima wazipe uhuru (semi autonomy), la sivyo majukumu yarudi wizara mama 💯.

Hili ni zao la sera za mwendazake!
 
Hii nchi ina watu wajinga sn una TANROAD unaanzisha TARURA hapo hapo una TEMESA, ni akili au matope?
Kama vyote taasisi hizo zote, zilifanya kazi kwa ufanisi mkubwa , na ghafla zote zinakufa, hatuna sababu ya kulaumu uanzishwaji wake, ila tatizo ni mfumo wa kisiasa kuamua malengo, na miradi kulingana na mtawala anataka nini, wapi na kwa nini. Tungekuwa na mfumo Bora wa vipaombele, katiba, taasisi,, miradi na melengo ya kitaifa, haya yasingeikuta Tanroad au yeyote. Ila kwa kuwa tangu Nyerere aondoke, kila Rais anayeingia madarakani anajichotea mali atakavyo na kufanya lolote atakalo, tutegemee Zanzibar kujengwa kwa pesa za bara kwa miradi mikubwa kuliko Pato lao. Akitoka atakuja mfano wa kusini au magharibi naye anakimbizia miradi huko nk nk nk. Mpaka tuiwekeke sawa Tanganyika, Yesu atakuwa ameisharudi. My dear Tanganyika is collapsing and perishing.
 
Kama Tanroad ilianzishwa mwaka 2000 wakati wa Mkapa, Magufuli anahusikaje ? Kama ilifanya vizuri kwa Mkapa, Kikwete, na Magufuli kwanini ife ghafla leo. Chanzo cha fedha za Tanroad ni tozo kwenye mafuta, na bado ipo na mafuta yanauzwa kila uchao. Fedha za tozo hiyo zinachukuliwa na nani na zinafanya nini ? Tanroad wanaomba fedha mfano bilioni 300 lakini wanapewa bilioni 25, unategemea wafanye maajabu gani kwa pesa kiduchu mlizowapa. Ni sawa na ungeilaumu TRA inakufa wakati makusanyo yao yanapanda kila,tutakuuliza swali rahisi tu. Pesa anazokukusanyia umezipeleka wapi na umezifanyia nini ? Mashirika/viwanda yote wakati wa Nyerere yalihujumiwa makusudi ili kuwanufaisha watu binafsi au wazungu kwa mlango wa nyuma, kama kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi, tipper, kiwanda cha tairi za magari , general tire Arusha nk
 
Elewa hoja ya "muundo" aliyoileta mtoa mada, na autonomy niliyozungumzia!
 
Mishahara, magari na majengo? gharama za uendeshaji lazima ziwe kubwa, kwanini tusiwe na ofisi za ujenzi?
 
Goodbye TANROADS, killed by Awamu ya 6.
 
Magufuri na Mfugale ndio waliondoka na Tanroad
 

Tanroads ilifanya vizuri sababu ya kuwa na focus kwenye usimamizi wa ubora wa barabara.
Walipoa kufanya kila kitu wenyewe, wakaangukia pua.
Na sasa hivi karibu waajiriwa wengi wa Tanroads wana kampuni zao za ujenzi wanajigawia Tenders.
Safari njema huko taasisi inakokwenda. Wakishafika watatutumia salamu
 
Kweli asee tanroad hoi pia na ofisi za wizara ya maji
 
Uhaba wa fedha huku wenye mamlaka wananunua Vieite huko. Hii nchi ili tutoboe ni hadi madaraka yashikwe na vibwengo
 
Wewe ni mtumishi wa TANROADS sio bure maana una uchungu nayo s
Mdau Ameongea Point sana, Autonomous kwenye hizi Agencies ni Muhimu sana sana na Wizara Ibaki Kusimamia issue za Policies tu na Kutoa Roadmap the rest Taasisi izi ziachwe zi operate independently itasaidia sana Kuongeza efficiency
 
hela zote kwenye chaguzi, tena kwa hii samia infrastructure bond ndo itafund mwaka huu.....
 
Kuna taasisi zina kazi zinazofanana. Ndio maana zinakuwa mzigo usiobebeka wa gharama.

Na kwanini kazi nyingi wanajigawia wenyewe kwa wenyewe?
Siasa inaua TANROADS. Wanasiasa wanakipaumbele chao kumega 10% kwenye miradi.
Wengi hawaelewi msingi wa mgawanyo wa kazi za TANRIADSCnaTARURA.
TANROADS ni njia kuu kuunganisha miji, na TARURA iliyotengenezwa kutokana na idara za ujenzi halmshauri, kazi yake ni barabara za ndani ya miji na zile ndogo ndogo wilayani.

TARURA inaingiliwa sana na wanasiasa ukilinganisha na TANROADS.
Kwa mfumo aliotengeneza Rais Mkapa ulikuwa wa akili sana.
Mkapa alianzisha Road Fund taasisi ya kulishia fedha ujenzi wa barabara.
Hivyo TANROADS ilikuwa haikosi ingalau kutekeleza miradi mingi.
Sasa hivi Road Fund inaelekea inamegwa na haiendi TANROADS, na vile vile kwenye mdomo huo huo kuna TARURA, ambao uwezo wao kusimamia miradi ni mdogo.

Si muda mrefu tuaanza kuona kubomoka kwa njia kuu za kuunganisha miji, na wataalam kutimka TANROADS kwenda sehemu nyingine.

Mkapa alikuwa kichwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…