Kufika China kwa mara ya kwanza kama mfanyabiashara

Momosky

Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
13
Reaction score
10
Habari, samahani mimi ni mfanyabiashara mdogo wa accesories kofia miwani na pochi nataka kwnda China ninunue mizigo nije kuuza kwa jumla hasa yiwu lakini sina mwenyeji naomba ushauri? Na je kuna ma agent wakuja kukupokea airport na kukuzungusha af yiwu then unawalipa?

Au kama kuna yeyote anaweza kunisaidia nifanyaje tafadhali sijawahi fika China na sina wa kwenda nae, nmetafuta sana sijapata.
 
Wanakuja

Kila la kheri mpendwa.
 
Kwenda sio issue boss, ila issue ipo kwenye kupima Covid 19 kwa kipimo chao kipya walicho kigundua huko huko China juzi tu.

SWALI LA KUJIULIZA - Je, upo tayari kufanya hicho kipimo boss?
Kama upo tayari, basi nakutakia kila la heri boss. Ila ukirudi usisahau kuanzisha uzi wa kutupa mrejesho juu ya hicho kipimo chao kipya.

*Usisahau kuni tag katika uzi wako boss.
 
sasa hivi huwezi kuja China,ukiachana na corona ,sasa hivi wachina wanafunga maduka na viwanda kwa ajili ya sikukuu yao Chinese new year itakayo anza 12 February.Hadi maduka na viwanda kuanza kufanya kazi ni around march.Lakini pia corona bado inasumbua na wiki ilopita wameweka majina ya nchi 12 ambazo hawawezi pata visa ya China kwa sasa hivi.Kwa Afrika ni Ethiopia pekee,nchi zingine 11 ni za ulaya na Asia.Bado haieleweki hawa jamaa watafungua mipaka lini.Anyway mimi nipo Guangzhou,Yiwu nilikuwa 2 weeks ago soko la Futian.

 
Afrika nzima wanapita Ethiopia kwenda huko, wakipiga stop Ethiopia then ina maana hawataki mwafrika yeyote kwa sasa.
 
Muhimu tu uwe makini. Siku ukienda huko, usijaribu kabisa kumsaidia mtu yeyote yule mzigo wake! Uwe mkubwa au mdogo uwapo uwanja wa ndege wa Bongo au wa huko China

Akijitokeza mdada mzuri au jamaa fulani lenye six packs, mwambie Mzee wangu Tate Mkuu amenizuia kumsaidia mtu yeyote yule mzigo wake. China ni Wanyongaji wakubwa wa watu wanao ingiza madawa ya kulevya Nchini mwao.

Na usisahau aliyekamatwa na ngozi, ndiye mla nyama!
 
Jiandae kupimwa corona kwenye makalio hiyo ndio changamoto kubwa zaidi hasa kama marinda bado yapo [emoji28]mengine wadau watamalizia.
 
Kumbe Upo World wide
 
Wasiliana na kampuni ya kusafirisha mizigo kutoka China ya silent ocean. Wao huwa wanatoa hizo huduma unazotaka.
 
Mkuu si ununulie tu Alibaba unaangalia trusted supplier mwenye review nying na affordable price, alaf kusafrisha unatumia silent ocean, ya nini kujichosha kwenda huko , nauli ungeongezea kwenye mzigo.
 
Mkuu unataka kwenda kutalii au unataka kwenda kununua mzigo?Unajua ni mzigo gani unataka kwenda kuchukua? Unajua mzigo uko mji gani?Je umeshajua utafikia hoteli gani?Utakaa siku ngapi?

Unatfunga mzigo wa thamni gani?Utanunua kwa bei gani?Utasafirisha kwa kampuni/njia gani?Hayo ni baadhi ya maswali lazima ujijibu kabla ya kuamua kutafuta mtu wa kwenda naye kwani wa kwenda no wako wengi sana.
 
Naomba nikuulize Kama hautajali.

Nikitaka kuna kununua simu China nije kuuza Tz je million 5 itatosha kuanzia?

nijibu kwa experience yako sio Google.
 
Asante nimepata kitu
 
Mimi naona kwenda mwenyewe ndo vizuri zaidim.maana utajifunza vitu vingi na kuona mengi
Mkuu si ununulie Tu Alibaba unaangalia trusted supplier mwenye review nying na affordable price , alaf kusafrisha unatumia silent ocean , ya nini kujichosha kwenda huko , nauli ungeongezea kwenye mzigo
 
lini.Anyway mimi nipo Guangzhou,Yiwu nilikuwa 2 weeks ago soko la Futian.
Mkuu, hiko kipimo cha Corona ni kweli huko kinafanywa hivyo?!
 
Naomba nikuulize Kama hautajali.
Nikitaka kuna kununua simu China nije kuuza Tz je million 5 itatosha kuanzia?.
nijibu kwa experience yako sio Google.

Nakujibu kwa experience ya miaka yangu zaidi ya saba kuwa Guangzhou.Hiyo hela ina tosha lakini italingana na unanunua simu aina gani na umejitangaza vipi bongo.Kuna watu wanaagiza simu hadi 100 zikifika tu bongo kesho yake anaweka mpunga wa order nyingine.Kwa hiyo ina depend na market yako lakini kwa 5m tsh kama ni yakuagiza tu mzigo inaweza ikatosha kulingana na target yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…