Miaka 70 kuanzia leo yaani 2110.
Sisi Sote tutakuwa
makaburini
pamoja na
jamaa zetu na marafiki zetu
. Watu tusiowajua wataishi katika majumba
na maeneo yetu.
MALI
zetu zooote zitamilikiwa na watu tusiowajua. Watu hao wala hawatotukumbuka. Hivi ni wangapi kati yetu wanaowakumbuka
mababu wa
mababu zao?.
Majumba yetu ya Goba na Masaki yatakuwa yanamilikiwa na watu wengine kabisa; Drea house yako uliyozika ndugu yako ili mtu asiuze hilo kaburi litahamishiwa Kimbiji na nyumba itavunjwa kufanuywa night club.
Tutabaki kuwa
historia kwa vizazi vyetu na wakati huo huo watu
watatusahau hata
majina yetu na maumbile yetu.
Wakati huo tutakuja kugundua jinsi tulivyokuwa
wajinga na jinsi tulivyojidanganya kutaka kupata kila kitu kwa njia yeyote
.
Tutaomba angalau tupewe
uhai kwa
muda mfupi ili
tutubie ikiwa ni pamoja na kutoa sadaka
lakini itakuwa haiwezekani.
Zingatia kuwa, Leo
tuna nafasi kutenda
wema kwa ajili ya faida yetu
wenyewe na wengine. Kitu pekee kitakachobaki milele ni
matendo yetu mema katika Dunia hii na maisha baada ya kifo. Muda bado tunao.
Fanya matendo mema kabla hujachelewa sana
*Mungu atusaidie katika hili.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kutenda wema na kupata mwisho mwema.
--