Kufikia mwaka 2110 sisi wote hapa JF tutakuwa tumekufa

Zingatia ukweli kwamba hutakuwepo, kipindi hicho CCM itakuwa imesahaulika, kigamboni imemezwa na bahari, hakuna muungano tena wa upande wa pili na sisi, kila mwanamke atakuwa mwanaharakati akitaka haki sawa kwa asilimia 70, sasa givi wanataka 50/50.
Nakataa.Mimi nitakuwepo.Weye ndiye utakufa.Pumzika kwa amani ndugu yangu.Mola akurehemu.
 
Nakataa.Mimi nitakuwepo.Weye ndiye utakufa.Pumzika kwa amani ndugu yangu.Mola akurehemu.

Zaburi 90:10 BHN - Bible.com​

https://www.bible.com › BHN

Miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini; lakini yote ni shida na taabu! Siku zapita mbio, nasi twatoweka mara.

Sasa wewe unapingana na Biblia?
 
Ni kweli, siku ikifika marafiki watatumiana ujumbe unaoanza na 'Nina habari mbaya'

Ila Maandishi yako humu JF yatabaki kwa miaka mingi mbele na hutaweza kuedit.
 
Wekeza kwenye vitu vya maana utakumbukwa, mother alikuwa mgao wake wa Banda la Babu walilouza kkoo akatupatia na sisi in migao tukafanya mtaji kwanini Babu tusimkumbuke? Hadi mwanangu nimempa jina la Babu yake, maana bila Babu sijui ingekuwaje
 
Nawaza miaka hiyo mjukuu wangu ambaye ni mtoto wa mwanangu wa kwanza naye anapita humu kusoma comments za babu yake[emoji23][emoji23]

Nawaza kwa haya maendeleo ya sciemce na techonology ukiachana na hawa watoto kamilu tunaowazaa hivi hakutakua na viumbe wa ajabu ajabu kama Aliens nao wanaishi kama binadamu wengine. Huyu mzungu hata simuamini kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea kitu kigumu mno na chenye ukweli mchungu ambao wengi hatupendi kuusikia.....
Tumewekewa kifo, hivyo tuombe neema za Mungu kukumbuka kwamba duniani tunapita......

Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima- Zaburi 90:12
 
Nina miaka 15 jumlisha 70 nitakuwa na 85,, bado nitakuepo hivo si ajabu nitakuwa mmiliki wa jf baada ya waasisi kukufa

Naomba mnipe uongozi kwa maana hamjui kesho yenu
 
Mi saizi Nina miaka 25,Sasa ukiongeza hyo 70 nitakuwa nimefikisha 95...hapo nitakuwa nimebaki na miaka mingine kumi ya kuishi.Tena nitakuwa bado nipo humu jf Kama active member.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…